Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumanne, 29 Mei 2018

Mkutano wa marafiki wa elimu Musoma






 Marafiki wa elimu musoma mapema siku ya jumamosi walikutana na kujadili changamoto zinazokabili elimu katika manispaa ya Musoma Mjini,

katika mkutano huo wa marafiki wa elimu, waliweza kubaini uwepo wa mimba nyingi kwa wanafunzi hasa wa sekondari ambazo haziripotiwi kwenye vyombo vya dora.
aidha marafiki hao wa elimu kwa pamoja waliaziamia kuanzisha mpango mahususi wa kutoa elimu kwa wanajamii, kwani imegundulika wazazi wengi wamekuwa chanzo cha mimba hizo kwa kuficha ukweli pindi watoto wao wapatapo ujauzito wakiwa shule.

.
picha matukio na, CIV Juma Okumu






Ijumaa, 20 Januari 2017

Pakua mpango mkakati wa haki elimu 2017/2021

Nadharia ya mabadiliko katika mpango Mkakati wa HakiElimu wa miaka mitano (2017- 2021). Nadharia hii inaonesha Dira tuliyonayo, matarajio tunayotegemea na jinsi ya kufika huko. Jipatie nakala ya mpango huu kwa lugha ya Kiswahili kwa kupakua kutoka katika link ifuatayo http://bit.ly/2iIzT2P

Jumanne, 17 Mei 2016

walimu 35,411 kuajiliwa mwaka wa fedha 2016/2017

Walimu 35,411 nchini wataajiriwa katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Watakaokaidi kwenda kuripoti katika mikoa ya pembezoni, hawataajiriwa na serikali.
 
Hatua hiyo imeelezwa kwamba imetokana na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu, ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.
 
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jaffo alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni, ikiwemo Lindi na kwingineko, lakini hawakuripoti.
 
Jaffo alisema ni kweli kuna walimu wengi ambao hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni. Alisema si Lindi peke yake, bali na mikoa mingine, ikiwemo Katavi na Kigoma.
 
Alisema kwa mwaka huu, wataajiri walimu 35,411, lakini ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini tu, hawataajiriwa tena serikalini, kama wanavyoomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi

Ijumaa, 15 Aprili 2016

marafiki wa elimu musoma wasaidia jamii

kutokana na uhitaji wa jamii marafiki wa elimu musoma tumeona ni nafasi nzuri kujichangisha na kuweza kusaidia wanafunzi vifaa vya shule tazama picha za matukio pale marafiki tulipojumuika na jamii kuchangia tulichokuwa nacho
rafiki wa elimu Juma okumu akielezea dhana ya marafiki wa elimu

mwenyekiti wa mtandao wa marafiki wa elimu musoma Bi perus Masokomya akikabidhi vifaa hivyo







picha ya pamoja marafiki wazazi na wanafunzi




Alhamisi, 31 Machi 2016

marafiki wa elimu musoma kutoa msaada kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu

kutokana na dhana ya marafiki wa elimu ya kuhakikisha elimu bora kwa wanafunzi wote wa kitanzania, hivi karibuni mtandao wa marafiki wa elimu wameamua kujichangisha ili kuweza kukusanya vifaa vya shule kwa ajili ya kuweza kusaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.

mpango huo wa marafiki wa elimu umelenga kusaidia wanafunzi 25 vifaa vya shule kama madaftari,kalamu mabegi na sare za shule.
mpango huo utatekelezwa tarehe 15/04/2016
kwa mdau atakaeguswa na mpango huu anaweza kuwasiliana na marafiki wa elimu musoma kwa nambari 0755 650 075
katibu msaidizi wa marafiki wa elimu Kaseja january akisoma machapisho

rafiki wa elimu Juma okumu pamoja na Godfrey Mjaya wakisoma machapisho kabla ya kikao kuanza

mwenyekiti mpya wa mtandao wa marafiki wa elimu musoma Bi Perus masokomya

rafiki elimu Daniel Richard akipokea michango ya marafiki

Kaseja January akihakiki vifaa vilivyopatikana

katibu wa marafiki wa elimu musoma Bi Rose Olimo

mlezi wa mtandao wa marafiki wa elimu musoma thomas bega aliyesimama

marafiki wakimsikiliza mwenyekiti wa mtandao

mwenyekiti wa mtandao akizungumza na marafiki

Jumatatu, 1 Februari 2016

Haki elimu yakusanya maoni kuhusu lugha ya kufundishia

shirika la Haki elimu linakusanya maoni ya wananchi kupitia mtandao wake wa twitter juu ya mapendekezo ya lugha ya kufundishia kama iwe KISWAHILI au KIINGEREZA unaweza kushiriki kwa kuwafuata kwenye ukurasa wao wa twitter kwa anwani ya  @hakielimu 

shiriki kwa kupiga kura yako je lugha ipi ungependa itumike kufundishia?

Jumatatu, 25 Januari 2016

shule ya msingi Mwisenge B yafanikiwa kupata darasa la tehama

darasa la tehama shule ya msingi Mwisenge B
wakati serikali ikiwa imetangaza na kuanza kutekeleza mpango wake wa kutoa elimu bure nchini shule ya msingi Mwisenge B ni moja kati ya shule zilizopata bahati nyingine tena ya kuweza kuboresha kiwango chake cha elimu kwa kuendana na mfumo wa kisasa zaidi wa kutumia computer tofauti na shule nyingi za msingi manispaa ya musoma mjini.
baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye chuma cha tehama
awali shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu liliweza kuichukua shule ya Mwisenge A na B na kuiingiza katika mipango yake na kuifanya shule ya mfano na kuweza kujenga Maktaba ya kisasa kabisa shuleni hapo pamoja na kukarabati madarasa ya awali (chekechea ( kwa kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kuwapeleka walimu wa madarasa ya awali mafunzo.
mwalimu wa tehama shule ya msingi Mwisenge B
licha ya hayo shirika hilo pia limekuwa likitoa motisha kwa baadhi ya wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni hapo hasa katika mpango uliouanzisha shuleni hapo wa vilabu vya masomo,ambapo vilabu hivyo vya masomo vimekuwa vikisaidia sana kuhakikisha vinamaliza kabisa tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika shuleni hapo.
baada ya jitihada kubwa za shirika la Haki Elimu hivi karibuni wadau wengine wa elimu wamejitokeza na kuweza kuisaidia shule hiyo kwa kuipatia computer 17 pamoja na projector 3 na kuifungia shule hiyo huduma ya internet ya uhakika  jambo linaloonyesha nia ya kuitoa shule hiyo ilipokuwepo na kuipaisha zaidi kitaaluma .hivi karibuni kumekuwepo na mipango mbalimbali ya kuifanya shule hiyo kuwa kituo cha tehama kwa shule za msingi musoma mjini ,jambo litakalo kuwa zuri ikizingatiwa kuwa shule ya msingi Mwisenge ndipo aliposoma baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.pamoja na iongozi wengine wakubwa kama kina jaji Sinde Joseph Warioba.