|
Mwenyekiti wa kamati ya shule pamoja na diwani |
|
Ramani ya choo inavyoonekana |
|
Wajumbe wakimsikiliza diwani |
katika kile kinachoonekana kutokuyathamini majukumu halisi ya kamati za shule wajumbe wa kamati ya shule ya msingi Nyang'omboli walikataa ujenzi wa choo cha shule hiyo licha ya kutokuwa na choo chakavu kisichokidhi mahitaji.
wajumbe hao wa kamati ya shule kabla walisikia taarifa za uwepo wa shilingi milioni 17 kwa ajili ya ujenzi wa choo katika shule hiyo , licha ya kusikia taarifa hizo kwa baadhi ya wadau tu lakini wajumbe hawakuwa na taarifa rasmi za fedha hizo, baada ya siku kusonga ndipo mwalimu mkuu wa shule hiyo aliwaeleza wajumbe rasmi juu ya uwepo wa fedha hizo na kuwataarifu wajumbe kuwa pesa hizo zimepitia katika mfuko wa kata,
na wajumbe wa kata pamoja na diwani wameshakaa na kupanga matumizi ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kumtafuta mjenzi wa choo hicho bila kamati kuwa na taarifa.
|
Diwani akifafanua jambo |
hapo ndipo wanakamati wa shule hiyo walipoamua kutoa tamko kuwa hawako tayari kuona ujenzi wa choo hicho ukiendelea mpaka washirikishwe, kwa bahati diwani wa kata hiyo ya Kigera alizipata taarifa hizo za kamati na kuamua kuitisha kikao na kamati hiyo na kuwaeleza juu ya kile kinachoendelea na kutoa nafasi moja kwa moja kwa wajumbe wa kamati hiyo kukagua ujenzi wa choo hicho kitakapokuwa kinaendelea na kuomba kutoa ushirikiano wa kutosha
kutokana na kauli hizo wajumbe waliafikiana kwa pamoja ujenzi wa choo hicho uanze na kuafikiana kusimamia ipasavyo .
picha kwa hisani ya mjumbe wa kamati ya shule hiyo JUMA RICHARD OKUMU