Watanzania tunaiona elimu ya MEMKWA kama haina msaada kabisa kwetu lakini ifike mahali tukumbuke kwamba mwalimu Nyerere alipigana kufa na kupona kuhakikisha tunafuta ujinga nchini na mbinu kubwa aliyotumia ni kuhakikisha walikosa elimu wanapata elimu bila kujali umri wao na akafanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.
tofauti iliyopo sasa serikali na wanajamii hawaichukulii elimu hiyo kama ukombozi wa kututoa kwenye ujinga tena na mwisho wa siku tunaendelea kuzalisha taifa la wasiojua kusoma na kuandika
kwa pamoja tupaze sauti na kusema TUKIWEKEZA KWENYE ELIMU YA MEMKWA TUTAFUTA UJINGA NCHINI
harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu