harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania
Ijumaa, 22 Machi 2013
Mara nyingi tumeliona suala la upatikanaji wa elimu bora kama ni suala la serikali peke yake na kusahau kuwa jamii nzima inajukumu la kusimamia elimu
tunajiuliza maswali mengi sana juu ya kuzidi kudolola kwa elimu nchini mara nyingi tumemtafuta mchawi bila kumpata na hata tunasahau kuwa wachawi wa tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu ni sisi wenyewe
hapo ulipo kama wewe ni mzazi ,mlezi ,au mwanajamii jiulize umewahi kufanya nini kusaidia sekta ya elimu umewahi kufuatilia na kutaka kujua juu ya elimu inayotolewa shuleni?
Juma richard ni mjumbe wakamati ya shule ya msingi hapa musoma anasema tangu amekuwa mjumbe wa kamati ya shule hajawahi kukutana na mzazi au mwanajamii aliyewahi kumuuliza juu ya mapato na matumizi ya shule pia hajawahi kuulizwa juu ya ruzuku za wanafunzi na hata ruzuku za maendeleo.
halii hii inamaanisha kwamba wengi wa wanajamii hawana muda wa kukaa na kutafakari juu ya elimu na mwisho wa siku huachia serikali peke yao na walimu ndiyo watoe elimu bora lakini pale tunapogundua kwamba tumefanya vibaya katika mitihani hapo utawasikia wazazi wengi wakilalamika kutaka kujua ni kwa nini.
wazazi wengi hawana muda wa kukagua madaftari ya watoto wao hawana muda wa kuzungumza na familia zao. walimu pia wanakatishwa tamaa na mazingira magumu ya kufundishia hivyo upelekea kutoa elimu isiyo bora na kuwaaminisha watoto kuwa elimu bora upatikana kwa masomo ya ziada yaani tution.
Kwa upande wake serikali inachukulia kushuka kwa elimu kama kitu cha kawaida na kusahau kuwa kuna wakati ruzuku za wanafunzi ucheleweshwa shule makusudi pia upelekwa zikiwa pungufu serikali usahau kwamba walimu wanaishi katika mazingira magumu sana ,shule hazina nyezo za kujifunzia na kufundishia
bajeti ya wizara ya elimu pia ni ndogo haikizi mahitaji bajeti kubwa uelekezwa kwenye utawala yaani posho za semina na kukarimu wageni.
lakini suala la kubadilika kwa mitaala limekuwa sugu na upelekea walimu kutokuielewa vizuri kwani hawana mafunzo juu ya mibadiliko hiyo.
kila mmoja ubaki akivutia kamba upande wake tujiulize ni wapi tumekosea tujisahihishe tufanye vema .
Alhamisi, 21 Machi 2013
Jumamosi, 16 Machi 2013
Marafiki wa elimu katika picha tofauti
Marafiki wakimsikiliza kwa makini mwalimu Byabato toka serengeti |
Mwalimu Byabato rafiki toka wilaya ya serengeti akielezea juu ya dhana ya marafiki wa elimu ni nini! |
Rafiki wa elimu Anastazia Richard akijitambulisha katika mkutano wa marafiki wa elimu |
Rafiki wa elimu akichangia mada katika mkutano wa marafiki wa elimu musoma |
marafiki wa elimu wakijadiliana katika makundi juu ya mbinu za kuboresha elimu |
Ijumaa, 15 Machi 2013
Ukeketaji mkoa wa Mara
UMEWAHI KUSIKIA JUU YA UKEKETAJI
MKOA WA MARA NDIYO HUU
![]() |
Mtoto akifanyiwa unyama wa ukeketaji |
ukeketaji ni moja ya mila na tamaduni za baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mara hasa maeneo ya Tarime ,Serengeti na baadhi ya maeneo ya jirani na wilaya tajwa hapo juu.
makabila ambayo yamejikita zaidi katika suala la ukeketaji ni wakurya ambao wameienzi hii mila tangu miaka mingi.
mara nyingi wamebaki wakiamini na kuaminisha kwamba kumkeketa mwanamke ndo kukamilika kwa mwanamke na kufikia wakati mwingine kukataza hata vijana wao kuoa mwanamke ambae aja keketa
Juma mohammed ni mkazi wa mkoa wa mara na msanii wa filamu anazungumzia suala hili kama ni uelewa mdogo wa baadhi ya wazee wa mila pia anabainisha kuwa wakurya uamini kwamba mwanamke ambae ajakeketwa ana mikosi na astahili kuonekana kama mwanamke mbele za watu.
upande mwingine Amosi Taratasi mkazi wa butiama kazungumza na mwandishi wa blog hii na kusema kwamba suala la ukeketaji limejikita kwenye makabila yao ya wakurya tangu enzi na analizungumzia kwa mapana na kusema kwamba thamani ya mwanamke iko pale pale akeketwe au asikeketwe
pia anasema si suala la ukeketaji tu bali kuna mambo na vitendo vingi vinavyoashiria kumnyima mwanamke uhuru wake wa kuwa mwanamke kamili
wadau wa blog hii wengine wamejikita zaidi kwa kusema kwamba kuna upungufu mkubwa wa elimu juu ya ukeketaji na kuonelea kwamba wakeketaji(mangariba) wapewe elimu ya kutosha juu ya matatizo yanayowapata wanawake waliyokeketwa na si kuishia kusema ni kosa kukeketa bila kumpa mtu elimu ya kutosha.
marafiki wa elimu tunaamini kwamba kumkeketa mwanamke ni mila zilizopitwa na wakati na azistahili katika jamii tuliyonayo tutaendelea kutoa elimu hii katika blog hii pamoja na mikutano ya marafiki wa elimu mkoa wa Mara
Jumapili, 10 Machi 2013
UMUHIMU WA ELIMU YA AWALI NA DARASA LA KWANZA ILIVYO SASA NA ZAMANI
Watanzania wenzetu tunapaswa kujiuliza juu ya elimu yetu ya darasa la awali na darasa la kwanza miaka ya 80 mpaka 90 mwanafunzi wa darasa la kwanza alikuwa anafundishwa masomo matatu tu yaani Kusoma,Kuhesabu na Kuandika.
nyakati hizo mwanafunzi wa darasa la kwanza alikuwa na uwezo mzuri wa kuweza kuandika mwandiko mzuri kusoma vizuri kwa kuungaunga manene kama mama baba kaka nk.
pia waliweza kuhesabu moja mpaka mia vizuri kabisa
waliweza kusoma hadithi fupi fupi vizuri japo kwa kusitasita lakini hali hiyo ilikuwa ikionyesha matumani kwamba wafikapo darasa la pili basi wangejimudu vizuri.
baada ya kuizungumzia elimu ya darasa la kwanza sasa niizungumzie elimu ya darasa la awali kabla hatujaiona hali ya elimu ya sasa ilivyo.
darasa la awali kwa kipindi hicho ilikuwa ni lazima kabla ya mwanafunzi kuingia darasa la kwanza hii ilikuwa inampa mwanafunzi uwezo wa awali wa kuyazoea mazingira ya shule kuzielewa stadi za awali na kuweza kujimudu aingiapo darasa la kwanza.
TANZANIA YA LEO
Mwanafunzi wa darasa la kwanza anafundishwa masomo manne hadi matano umuhimu wa elimu wa awali authaminiwi tena walimu wa kuwamudu wanafunzi wa madarasa ya awali na darasa la kwanza ni wachache sana .
Mwanafunzi wa darasa la kwanza hana tofauti hata kidogo na mwanafunzi wa darasa la awali hali hii upelekea watoto kusukumwa na kuamini kwamba wataelewa mbele kwa mbele lakini mara nyingi huko mbele tunapotegemea wataelewa tu ndipo tunapofika mahala ambapo hakuna mitihani ya kujipima tena .
na mwisho wa siku tunazalisha taifa la watoto wanaomaliza darsa la saba bila kujua kusoma wala kuandika
yatupasa kwa dhati ya mioyo yetu kuhakikisha kwamba mitaala haibadilikibadiliki wanafunzi wa darasa la kwanza wanajifunza kuandika kusoma na kuhesabu(kkk) na si kulundikiwa masomo mengi tofauti na uwezo wao hatuwezi kumfundisha mwanafunzi wa darasa la kwanza kiingereza wakati mazingira halisi ya anapotoka ni waswahili hucheza na watoto wa kiswahili masaa yote.
ni lazima tumfundishe stadi za awali kwanza tangu darasa la awali mpaka darsa la tatu na afikapo darsa la 3 ndipo aanze kuchanganyiwa masomo kwani hukuta sasa hata akili yake inaanza kupanuka
NI JUKUMU LETU SOTE TUTAFAKARI KWA PAMOJA
Jumapili, 3 Machi 2013
ELIMU YETU INATUPELEKA MBELE AU INATURUDISHA NYUMA
Leo ni siku nyingine tena ambapo tunapaswa kujiuliza maswali mengi sana mioyoni mwetu
tujiulize ni wapi tulipotoka
wapi tulipo na wapi tunapoelekea
tulipotoka ni pale tulipopata uhuru wetu mwaka 1961 elimu kwa wengi ilikuwa haina umuhimu wengi hawakuelewa elimu inaweza kuyasaidia maisha ya mwanadamu kwa njia ipi
juhudi za mwalimu Nyerere na uongozi wake uliwajengea watanzania moyo wa kujua elimu ni nini faida za elimu ni zipi ,baada ya juhudi hizi za viongozi tuliweza kuyaona mafanikio kwani hata wale waliyokuwa wanadharau elimu waliweza kuona umuhimu wake na kuanza kuijali elimu
huko ndipo tulipotoka.
Tulipo leo
ni pahali ambapo kuna matabaka ya elimu wanaotakiwa waonyeshe njia ya kuthamini elimu hawana moyo huo tena maskini wengi wanaojua umuhimu wa elimu wanashindwa kuwezesha watoto wao kusoma na kufikia malengo yao tofauti na zamani ambapo elimu ilitolewa bure na jamii zote zilipata elimu kwa usawa lakini sasa kutokana na matabaka tuliyonayo nchini mwenye pesa mwanae anapata elimu bora na maskini mwanae anategemea kupata matokeo bora ya mitihani tu.
ifike mahali tuseme kwa sauti ya pamoja kwamba sote ni watanzania sote tunaishi katika nchi moja sote tupate elimu sawa ,afya sawa na mahitaji sawasawa katika elimu
Tunapoelekea
kama hatutachukua hatua madhubuti tunalirudisha taifa mahali ambapo hakuna maskini atakaeijali elimu kama njia ya kumkwamua na mazingira magumu.
kwani gharama za elimu zinazidi kuongezeka , ubora wa elimu haupo tena kwa mtoto wa maskini tumeona na tunaendelea kuona watoto wengi wa maskini wanaishia kidato cha nne lakini elimu aliyoipata haikumpa stadi za kukabiliana na ugumu wa maisha
lakini watoto wa wenye pesa wamewezeshwa kupata elimu bora na mwisho wa siku watoto wa maskini uendelea kunyonywa na watoto waliyotoka kwenye familia zenye uwezo wa kifedha ,ajira hakuna kwa wanaoshidwa kidato cha nne wanaishia kuhangaika mabarabarani na bodaboda ,wanaishia kuwa vibaka kutokana na elimu duni waliyoipata
wazazi na walezi wa watoto maskini itafika pahali sasa hawatauona umuhimu wa elimu tena na tutaendelea kuzalisha taifa la watu wajinga wanaotawaliwa na wajanja wachache wenye pesa .
Hii ni Tanzania yetu sote lazima tuseme kwa pamoja
ELIMU SAWA KWA WOTE
Jumamosi, 2 Machi 2013
HABARI NJEMA KWA MARAFIKI WA ELIMU
marafiki wa elimu musoma kupitia blog hii tunapenda kuwakaribisha marafiki wa elimu wote wa musoma mjini pamoja na wakazi wote wa musoma mjini kuitembelea maktaba ya jamii iliyopo katika kata ya Kigera musoma mjini maktaba ufunguliwa siku za jumamosi na jumapili kwanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni
maktaba ipo jirani na shule ya msingi kigera imetazamana na shule ya msingi kigera ,kusoma vitabu ni bure na kila mmoja anakaribishwa kuitembelea na kujionea baadhi ya vitabu vilivyopo pia kujifunza mbinu mbalimbali kutoka kwa marafiki wa elimu musoma
kwa mnaotaka kututembelea wasiliana nasi kwa namba
0755 65 00 75 au 0786 65 00 75
marafiki wa elimu tunaamini kuwa kila mtanzania ana haki ya kupata na kupokea habari karibu tuhabarishane.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)