|
Mbunge wa Musoma Mjini Vincent Nyerere akiwa na rafiki wa elimu Juma Richard Radio Victoria Fm |
Mapema hii leo katika kipindi cha radio kinachorushwa na
marafiki wa elimu musoma Radio victoria fm ya mjini musoma, Mbunge wa jimbo la musoma mjini Mheshimiwa Vincent Nyerere ameeleza yale anayoyafanya kama kiongozi wa wananchi kuhakikisha anaboresha elimu katika jimbo lake.
katika mada iliyokuwa inasema VIONGOZI TUNAOWACHAGUA WANAJITOLEA KUBORESHA ELIMU?
Mbunge Nyerere anasema katika kipindi chake cha uongozi amefanikiwa kujenga maabara ya kisasa kwa pesa kidogo ya mfuko wa jimbo anayopata,amesema kwa mwaka anapokea kiasi cha milioni 17 mara 2 na amefanikiwa kujenga maabara yenye thamani ya shilingi milioni 68 amefanikiwa kupata kontena la vitabu lenye urefu wa futi 20 na kuvigawa mashuleni.
pia mbunge huyo anasema kwa jitihada zake pamoja na chama chake wamefanikiwa kutoa madawati kwa shule za chekechea na wametangaza tenda ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi jimbo la musoma mjini.
katika shukurani zake mbunge Nyerere kalipongeza shirika la
Haki Elimu kwa kufanikisha ujenzi wa maktaba ya kisasa katika shule ya msingi mwisenge na kuahidi kuendeleza ushirikiano na
marafiki wa elimu kuhakikisha kiwango cha elimu kinaimarika jimbo la musoma mjini.
Vincent Nyerere ni moja ya viongozi wanaoonesha nia ya kuboresha elimu! je kiongozi wako anawajibika kuboresha elimu?