Tangu mwaka 2010, taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya Twaweza
kupitia mradi wake wa Uwezo, imekuwa ikifanya tafiti katika nchi za
Afrika Mashariki zinazolenga kubaini uwezo wa watoto wa shule za msingi
katika stadi za kusoma na kuhesabu.
Majaribio haya, yamekuwa yakihusisha masomo ya
Hesabu na lugha za Kiswahili na Kiingereza kwa ngazi ya darasa la pili.
Sampuli hujumuisha wanafunzi wa darasa la tatu na darasa la saba.
Sampuli ya washiriki
Takwimu zinaonyesha kuwa, mwaka 2010 watoto
walioshirikishwa kwenye utafii huo walikuwa 37,683 mwaka 2011 wanafunzi
114,761 na mwaka 2012 wanafunzi walioshiriki ni 104,568.
Kwa upande wa kaya, mwaka 2010 zilishiriki kaya
18,952 mwaka 2011 zilikuwa kaya 59,992 na mwaka 2012 kaya. 55,191. Kwa
wilaya, mwaka 2010 zilishiriki Wilaya 38, mwaka 2011 zilikuwa wilaya 119
na mwaka 2012 wilaya 126.
Shule zilizoshiriki kwenye utafiti uliofanyika
mwaka 2010 zilikuwa ni 1,010 mwaka 2011 zilikuwa 3,709 na mwaka jana
zikawa 3,624.
Mratibu wa Uwezo upande wa Tanzania, Zaida Mgalla
anasema aghlabu majaribio hayo hutayarishwa kwa pamoja na wataalamu wa
masomo kutoka vyuo vikuu, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na walimu wa
masomo husika wa darasa la pili.
Matokeo 2010
Utafiti huu ulipofanywa mwaka 2010 ulionyesha
kuwa, japo Kiswahili ni lugha inayozungumzwa kwa upana zaidi nchini,
idadi kubwa ya watoto hawawezi kusoma kupitia lugha hiyo.
“Kwenye sampuli zetu, chini ya nusu (42.2
asilimia) ya watoto waliofanyiwa uchunguzi waliweza kusoma kwa hatua ya
hadithi. Wakati watoto wote katika darasa la tatu wanapaswa kuweza
kusoma hadithi ya ngazi ya darasa la pili, watoto chini ya mmoja kati ya
watatu (32.7 asilimia) ndio wanaweza.
‘’Hata hivyo, hadi wanamaliza shule ya msingi,
mtoto mmoja kati ya 5 hawezi kusoma hadithi ya ngazi ya darasa la pili,
licha ya kumaliza miaka saba ya elimu ya msingi,”inasema sehemu ya
utafiti huo.
Kwa upande wa Kiingereza, ripoti hiyo ya mwaka
2010 inaonyesha kuwa chini ya mwanafunzi mmoja kati ya 10 (7.7 asilimia)
ndio anayeweza kusoma hadhithi ya Kiingereza ya ngazi ya darasa la pili

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni