waziri wa elimu dk. shukuru kawambwa |
CWT imesema kauli hiyo ya serikali ni kutafuta visingizio baada ya kushindwa kutekeleza ahadi yake kuwa ifikapo Februari, mwaka huu deni la walimu litakuwa limelipwa.
Rais wa CWT, Gration Mkoba, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Alisema majadiliano ya mishahara ya walimu yalitokana na mgomo wa 2012 baada ya kukaa kwenye meza ya majadiliano na serikali ilikubali kulipa deni na kuandaa utaratibu wa kupandisha walimu madaraja.
“Inasikitisha kuona majadiliano yanahusisha waandishi wa habari bila ya kujua kuwa kwa kauli yake waziri tayari walimu wameingia kwenye mgogoro na serikali, lakini nawasihi walimu wasubiri tamko rasmi la mgogoro,” alisema.
Mkoba alisema tangu serikali ilipoahidi kutekeleza madai yao, hakuna hata dai moja lililotekelezwa lakini imewashangaza kuona ikijinadi kuwa inaendelea na majadiliano ya kulipa deni hilo wakati majadiliano hayana tija kwa mwalimu.
Alisema Novemba, mwaka jana mkutano mkuu wa CWT ulitoa siku 60 kwa serikali kukamilisha taratibu zote la kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu nchini.
Pia Januari mwaka huu kwenye kikao cha Baraza la Taifa la CWT kiliazimia kuwa ifikapo mwishoni mwa Februari, mwaka huu, ikiwa serikali itashindwa kulipa malimbikizo hayo litakuwa tayari kuongoza mgomo.
CHANZO:
NIPASHE
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni