waziri mkuu Mizengo Pinda |
Msabaha aliuliza katika kipindi cha maswali na majibu ya papo hapo ambayo hujibiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kila Alhamisi.
Alisema nchi yoyote iliyoendelea duniani ilianza kuwekeza kwenye elimu na kutoa mfano wa nchi ya Malyasia, lakini hapa nchini watoto wanabeba madumu ya maji na fagio na kuketi sakafuni, wakati nchi jirani ya Kenya wanaenda na Laptop shuleni.
“Tuliambiwa chenji ya rada itapunguza tatizo mashuleni, lakini mpaka sasa watoto wanakaa chini na dawati moja wanakaa watoto mpaka watano,” alisema.
Akijibu, Waziri Mkuu Pinda alisema jitihada ambazo serikali inafanya kuhusu elimu ni kuchukua maamuzi makubwa ambayo yamefanya suala la elimu kuzaa changamato kubwa kutokana na uandikishaji wa darasa la kwanza hadi la saba kuongezeka na kusababisha mahitaji ya shule za sekondari, elimu ya juu ya vyuo vikuu kuongezeka.
Aliwataka Wabunge waendelee kusaidia serikali ili bajeti ya Wizara ya Elimu iendelee kukua siku hadi siku kwani kukua kwa bajeti hiyo kutaongeza mambo mengi.
Katika swali la nyongeza Msabaha alitaka kujua wakati huu wa utandawazi wa Sayansi na Teknolojia, serikali inachukua hatua gani kuona wanafunzi wa shule za msingi wanaanza kwenda shule na Laptop.
Hata hivyo, wakati akijibu, Waziri Mkuu Pinda alimhoji “unataka laptop kwa watoto wote wa shule inawezekana? Kwa sababu lazima uulize hilo swali.”
Alisema suala la wanafunzi wa darasa la kwanza mpaka la saba si kuwa na Laptop bali ni kuwa na mfumo wa digitali ambao utamwezesha vitabu vyake vyote kuwa ndani ya kompyuta kwa kutumia kifaa kinachoitwa tablets badala ya kubeba mzigo mkubwa wa vitabu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni