madarasa yaliyobomolewa na kuwaacha wanafunzi bila kuwa na pahala pa kusomea |
Diwani huyo amekubwa na dhoruba hiyo baada ya kugundulika kubomoa madarasa hayo pasipo kufuata utaratibu. hivi karibuni ililipotiwa na kituo cha habari cha BBC katika kipindi cha haba na haba kuwa wanafunzi wa madarasa ya awali wa shule hiyo wamekuwa wakisomea katika moja ya jengo la ofisi kutokana na upungufu wa madarasa.
lakini suala hilo limechukua sura ya kisiasa zaidi baada ya MNEC Vedastus Manyinyi Mathayo kutoa ahadi hewa katika moja ya mikutano yake ya kisiasa kuwa atatoa mabati 100 kwa ajili ya ukarabati wa jengo hilo ambapo mpaka leo hajapeleka hata bati moja
hivi karibuni Mbunge wa Musoma Mjini Vincent Nyerere na Meya Alex Kisurula katika mikutano yao ya kuelezea mafanikio na changamoto wameahidi wananchi wa kata ya Kigera kuwa madarasa hayo yatakarabatiwa kabla ya mwezi disemba mwaka huu.
wito wetu marafiki wa elimu musoma kwa viongozi : ELIMU NI TAALUMA ISIYOHITAJI SIASA VIONGOZI WASILETE MCHEZO NA ELIMU YA WATOTO WA MASKINI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni