Geita. Walimu wa Shule ya Msingi Mwatulole mkoani Geita, hawana meza wala viti hali inayowalazimu kukalia madaftari ya wanafunzi kwa kuyatandika kwenye magogo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi baada ya kukutwa wamekalia madaftari, walimu hao walisema ukosefu wa samani shuleni hapo unawaathiri katika ufundishaji.
“Wakati mwingine tunasahihisha madaftari, huku tumesimama,” alisema Mwalimu Mathias Matiginya na kuongeza:
“Unakuta mwalimu ana vipindi vinne kwa siku, lakini anaishia kufundisha viwili kutokana na kusimama muda mrefu, anachoka haraka.”
Pia, alisema shule hiyo ina walimu wengi na haina ofisi, viti wala meza, hivyo walimu wanatumia darasa kama ofisi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Catherine Mgisu alisema suala hilo limefikishwa kwa uongozi wa halmashauri na kamati ya shule.
Alisema kamati hiyo inafanya jitihada za kuhamasisha wazazi kusaidia maendeleo ya shule ikiwamo upatikanaji wa viti na meza za walimu.
“Hii shule ina changamoto nyingi siyo ukosefu wa vitu hivyo tu, bali ina wanafunzi wengi, uhaba wa madarasa na madawati pamoja na utoro wa wanafunzi,” alisema Mwalimu Mgisu.
Katika hatua nyingine; Mwalimu wa Taaluma, Salma Rajab alisema anakerwa na wingi wa wanafunzi.
Alisema kutokana na hali hiyo kipindi cha mitihani mbanano huwa mkubwa hali inayowanyima fursa ya kusimamia vizuri.
“Walimu tunapata shida hasa wanafunzi wanapofanya mitihani, tunashindwa kupata uhalisia wa matokeo yao. Huwa hatulitawali darasa kutokana na msongamano, hivyo tunakaa nje,” alisema Mwalimu Rajab. Mwalimu Debora Lucas alisema darasa moja linachukua zaidi ya wanafunzi 3,000.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita, Magarita Nakainga alisema alipokea taarifa ya changamoto hizo na kwamba suala hilo linashughulikiwa ili kuhakikisha shule inakuwa na hali nzuri.
“Ni aibu kwa shule za mjini kuwa hivyo, hivi sasa tunaweka mikakati ya kukarabati na kuboresha miundombinu tunakusanya mapato ili tuanze kazi hiyo,”
chanzo mwananchi
alisema.
harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania
Jumanne, 12 Mei 2015
Ijumaa, 1 Mei 2015
Marafiki wa elimu Kahama wajengewa uwezo
Marafiki wa elimu Kahama ni moja kati ya wilaya zilizoanza kuinua upya ari ya marafiki wawilaya hiyo kujali elimu ,hivi karinubuni shirika la HAKI ELIMU liliandaa mpango maalumwa kuhamasisha harakati katika wilaya hiyo jambo lililoonyesha kupokelewa vyema na marafiki wa elimu wa wilaya hiyo na kupelekea ongezeko la marafiki wapya wa elimu. picha zinaonyesha baadhi ya matukio katika kongamano hilo
![]() |
| Joyce Mkina akizungumza na marafiki wa elimu Kahama |
M
Jumamosi, 28 Machi 2015
WAZAZI WAGOMA KUCHANGIA CHAKULA CHA WANAFUNZI
Kutoka kijiji cha Bisumwa wilaya mpya ya Butiama wazazi wamegomea uongozi wa shule yao pamoja na kamati juu ya suala la kuchangia chakula kwa wanafunzi shuleni kama agizo la serikali linavyosema wanafunzi wanapaswa kula shuleni ili kuongeza ari ya kujifunza na kupunguza utoro.
shule iliwaomba wazazi hao kichangia kiasi cha debe moja la mahindi na maharage kilo4 kila mwezi kwa ajili ya chakula cha wanafunzi awali katikabkikao hicho cha kamati ya shule na wazazi kamati iliwaambia wazazi kuwa kila mzazi atatakiwa kuchangia mchango huo kwa kila mtoto iwapo mzazi una watoto 4 basi utatakiwa kuchangia mahindi debe 4 na maharage kilo 16
baada ya wananchi kusikiliza maelezo hayo toka kwa uongozi wa shule walitoa kauli ya pamoja kwamba hawako tayari kuchangia kiasi hicho kutokana na hali ya maisha ya sasa na pia hawako tayari kuchangia hata debe moja kwa watoto 4 hivyo shule iendelee na utaratibu wa kutawanyisha watoto mapema ili waende majumbani mwao kula kisha warudi shule kama ilivyokuwa ikifanyika awali
suala la wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya wanafunzi limeonekana kuwa tatizo sana hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa na huenda likashindikana kabisa serikali inapaswa kuangalia njia mbadala ya kutekeleza mpango huu

Jumanne, 24 Februari 2015
mbunge Nyerere agawa computer na projector kwa awamu ya pili kwa shule za sec musoma mjiji
kwa awamu ya pili sasa mbunge wa musoma mjini mh. Vincent Nyerere anakusudia kugawa computer kumi na tano baada ya awamu ya kwanza kugawa computer kumi na tano
akizungumza na wakazi wa musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi mkendo mbunge huyo alielezea mafanikio mbalimbali aliyoyafikia katika sekta ya elimu. mpaka sasa ni
kujenga maabara ya kisasa katika shule ya sekondari bweri maarufu kwa jina la bweri makatani lengo likiwa ni kuwaanda wanafunzi kupenda sayansi
na kuwaahidi wananchi wa musoma mjini kuwa azma yake ya kuibadili shule ya msingi mkendo kuwa high school iko pale pale japo ni mchakato unaochukua muda mrefu kidogo.
mbunge nyerere aliefika uwanjani hapo na baadhi ya computer hizo pamoja na projector amesema kitu kikubwa anachoweza kuwalipa watoto wa
maskini wapiga kura wake ni elimu bora pekee hivyo atajitahidi kuhakikisha anakuza kiwango na ubora wa elimu musoma mjini
mbunge nyerere aliahidi kuzifikishia shule zote umeme ili iwe rahisi watoto kujifunza ambapo mpaka sasa kuna miradi kadhaa ya kupeleka umeme mashuleni imefikia hatua za mwisho mwandishi wa blog hii alifanikiwa kuitembelea shule ya sekondari nyasho iliyokuwa mbali sana na miundombinu ya umeme na kukuta nguzo zikiwa tayari zimesimamishwa na nyaya zikigoja kuwashwa umeme tu.
mauaji ya albino
makamu meya wa manspaa ya musoma pia alizungumzia juu ya mafanikio waliyoyafikia mpaka saa juu ya kuzuia na kulinda watoto albino ni pamoja na kuhakikisha shule ya msingi mwisenge mpaka sasa imepata uzio kwa ajili ya kulinda watoto hao.
na pia licha ya shule ya mwisenge kupata uzio maabara ya kisasa imejengwa na inasubiri kuzinduliwa tu.
mbunge nyerere ni moja ya wabunge wanaoonyesha nia na uchungu wa kujuza kiwango cha elimu nchini.

| Ongeza kich |
Jumatatu, 2 Februari 2015
kamati ya shule ya nyang'omboli yajipanga kunusuru wanafunzi kukaa sakafuni
Jumamosi, 13 Desemba 2014
serikali za mitaa muongozo sahihi wa serikali kuu fanya maamuzi sahihi
huu ni wakati sahihi wa kufanya maamuzi sahihi kwa miaka mitano ijayo ili iwe sahihi kwa jamii yako kura yako haki yako maendeleo yako marafiki wa elimu musoma tunawatakia watanzania wote uchaguzi mwema wa serikali za mitaa
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)