Ikiwa
yamebaki majuma machache wanafunzi wa kidato cha nne waanze mtihani wa
wa taifa, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iko kwenye mchakato wa
kubadilisha mfumo wa upangaji za mitihani ya sekondari na matumizi wa
alama za maendeleo ya mwanafunzi (Continuous Assessment (CA).
Mfumo huo ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwenye Mtihani wa taifa
wa kidato cha nne mwaka huu, unakuja ikiwa ni miezi michache tangu Tume
ya Waziri Mkuu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kufeli kwa maelfu ya
wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012.
Akizungumzia mchakato huo, Kamishna wa Elimu Profesa Eustella
Bhalalusesa alisema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya
kuboresha elimu na kuwa haina uhusiano na taarifa ya tume iliyoundwa na
Waziri Mkuu ambayo mpaka sasa haijawekwa hadharani.
“Mambo yanakwenda yanabadilika hata binadamu yeyote anabadilika kila
siku, mfumo unaotumika sasa hivi ni wa siku nyingi,” alisema.Alisema kuwa, ili kuweza kuboresha vyema mfumo huo wameshirikisha wadau mbalimbali zikiwamo shule za sekondari.
“Kama unataka kuboresha lazima upate maoni, lengo letu ni
kushirikisha shule zote za sekondari za Tanzania, ila siwezi
kukuhakikishia kama zote zitashiriki kwa kuwa tunawatumia zaidi maofisa
elimu mkoa na wilaya. Tumeweka pia dodoso kwenye mdandao ili watu zaidi
washiriki.
Kuhusu tume ya Pinda hapa haihusiki kabisa, ile ilikuwa na mambo
yake, hata bila ile tume sisi hii tungefanya tu,” alisema Profesa
Bhalalusesa. Alisema kuwa, mpaka sasa wameshapokea zaidi ya asilimia 60 ya maoni hayo kutokana na lengo walilo jiwekea.
Dodoso hilo ambalo pia Mwananchi imefanikiwa kuliona, linasema kuwa
serikali inakusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu Upangaji wa Viwango
vya Alama (Grade Ranges) katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na
cha sita pamoja na matumizi ya ‘Alama Endelevu ya Mwanafunzi [Continuous
Assessment (CA)].
“Serikali imeamua kukusanya maoni haya kwa sababu kwa muda mrefu sasa
upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika katika mitihani ya kuhitimu
kidato cha nne na kidato cha sita havifanani pamoja na kwamba mitihani
hiyo yote ni ya elimu ya sekondari.Pia
mfumo wa elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule
unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),”
sehemu ya dodoso inasema.
Dodoso hilo linafafanua kuwa, muundo wa kwanza ni ule wa shule ambao
alama mgando (Fixed Grade Ranges) ambao alama zinazotumika kupanga
madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 –
20. Muundo wa pili ulioidhinishwa kutumiwa na Necta kuanzia mwaka 2012 ni Upangaji wa Alama Mgando usiobadilika (Fixed Grade Range).Kwa kidato cha nne alama zilizotumika ni A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49 na F = 0 – 34.
Kwa upande wa kidato cha sita alama zilizotumika ni A = 80 – 100; B =
75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 –
39. Kwa mujibu wa dodoso hilo, alama zinazopendekezwa ni A = 81 – 100, B = 61 – 80, C = 41 – 60, D = 21 – 40 naF = 0 - 20.
Utaratibu mwingine ambao washiriki wanapaswa kuchagua ni A = 80 –
100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49 na F = 0 – 34 huku utaratibu
wa tatu ukiwa A+ = 91 – 100, A = 81 – 90, B+ = 71 - 80, B = 61 - 70, C+ =
51 – 60, C = 41 – 50, D+= 31 – 40, D = 21 – 30, E = 11 – 20 na U = 0 –
10.
Akisoma Kauli ya Serikali Bungeni kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya
Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka
2012, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wiliam Lukuvi alisema kuwa
matokeo yaliyotangazwa awali na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
yafutwe na yapangwe tena kwa kutumia mfumo uliobadilika mwaka 2011 kama
ilivyopendekeza tume ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Hata hivyo, baada ya kufutwa kwa matokeo hayo na kupangwa upya,
Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa utaratibu uliotumika
kupanga matokeo hayo mapya ni uleule uliotumika kuandaa matokeo
yaliyofutwa wa Fixed Grade Ranges.
“Kuanzia sasa matokeo ya mtihani ya kidato cha nne na sita
yatachakatwa kwa kutumia Fixed Grade Ranges na Standardization (alama
zisizobadilika na kuuwisha alama za mitihani),” alisema Kawambwa.
chanzo.Mwananchi.co.tz
harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni