MARAFIKI WA ELIMU MUSOMA
harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Jumanne, 29 Mei 2018
Mkutano wa marafiki wa elimu Musoma
Marafiki wa elimu musoma mapema siku ya jumamosi walikutana na kujadili changamoto zinazokabili elimu katika manispaa ya Musoma Mjini,
katika mkutano huo wa marafiki wa elimu, waliweza kubaini uwepo wa mimba nyingi kwa wanafunzi hasa wa sekondari ambazo haziripotiwi kwenye vyombo vya dora.
aidha marafiki hao wa elimu kwa pamoja waliaziamia kuanzisha mpango mahususi wa kutoa elimu kwa wanajamii, kwani imegundulika wazazi wengi wamekuwa chanzo cha mimba hizo kwa kuficha ukweli pindi watoto wao wapatapo ujauzito wakiwa shule.
.
picha matukio na, CIV Juma Okumu
Ijumaa, 20 Januari 2017
Pakua mpango mkakati wa haki elimu 2017/2021
Nadharia ya mabadiliko katika mpango Mkakati wa HakiElimu wa miaka mitano (2017- 2021). Nadharia hii inaonesha Dira tuliyonayo, matarajio tunayotegemea na jinsi ya kufika huko. Jipatie nakala ya mpango huu kwa lugha ya Kiswahili kwa kupakua kutoka katika link ifuatayo http://bit.ly/2iIzT2P
Jumanne, 17 Mei 2016
walimu 35,411 kuajiliwa mwaka wa fedha 2016/2017
Walimu 35,411 nchini wataajiriwa katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Watakaokaidi kwenda kuripoti katika mikoa ya pembezoni, hawataajiriwa na serikali.
Hatua hiyo imeelezwa kwamba imetokana na serikali kupokea maombi
mengi ya kazi kwa walimu, ambao mwaka jana hawakuripoti katika vituo
walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea kuajiriwa na shule
binafsi, lakini hawakufanikiwa.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Selemani Jaffo alisema hayo alipokuwa akijibu swali la nyongeza la
Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu serikali
inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni, ikiwemo
Lindi na kwingineko, lakini hawakuripoti.
Jaffo alisema ni kweli kuna walimu wengi ambao hawakuripoti katika
mikoa ya pembezoni. Alisema si Lindi peke yake, bali na mikoa mingine,
ikiwemo Katavi na Kigoma.
Alisema kwa mwaka huu, wataajiri walimu 35,411, lakini ambaye
hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini tu, hawataajiriwa tena
serikalini, kama wanavyoomba tena baada ya kukosa katika shule binafsi
Ijumaa, 15 Aprili 2016
marafiki wa elimu musoma wasaidia jamii
kutokana na uhitaji wa jamii marafiki wa elimu musoma tumeona ni nafasi nzuri kujichangisha na kuweza kusaidia wanafunzi vifaa vya shule tazama picha za matukio pale marafiki tulipojumuika na jamii kuchangia tulichokuwa nacho
rafiki wa elimu Juma okumu akielezea dhana ya marafiki wa elimu |
mwenyekiti wa mtandao wa marafiki wa elimu musoma Bi perus Masokomya akikabidhi vifaa hivyo |
picha ya pamoja marafiki wazazi na wanafunzi |
Alhamisi, 31 Machi 2016
marafiki wa elimu musoma kutoa msaada kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu
kutokana na dhana ya marafiki wa elimu ya kuhakikisha elimu bora kwa wanafunzi wote wa kitanzania, hivi karibuni mtandao wa marafiki wa elimu wameamua kujichangisha ili kuweza kukusanya vifaa vya shule kwa ajili ya kuweza kusaidia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu.
mpango huo wa marafiki wa elimu umelenga kusaidia wanafunzi 25 vifaa vya shule kama madaftari,kalamu mabegi na sare za shule.
mpango huo utatekelezwa tarehe 15/04/2016
kwa mdau atakaeguswa na mpango huu anaweza kuwasiliana na marafiki wa elimu musoma kwa nambari 0755 650 075
mpango huo wa marafiki wa elimu umelenga kusaidia wanafunzi 25 vifaa vya shule kama madaftari,kalamu mabegi na sare za shule.
mpango huo utatekelezwa tarehe 15/04/2016
kwa mdau atakaeguswa na mpango huu anaweza kuwasiliana na marafiki wa elimu musoma kwa nambari 0755 650 075
katibu msaidizi wa marafiki wa elimu Kaseja january akisoma machapisho |
rafiki wa elimu Juma okumu pamoja na Godfrey Mjaya wakisoma machapisho kabla ya kikao kuanza |
mwenyekiti mpya wa mtandao wa marafiki wa elimu musoma Bi Perus masokomya |
rafiki elimu Daniel Richard akipokea michango ya marafiki |
Kaseja January akihakiki vifaa vilivyopatikana |
katibu wa marafiki wa elimu musoma Bi Rose Olimo |
mlezi wa mtandao wa marafiki wa elimu musoma thomas bega aliyesimama |
marafiki wakimsikiliza mwenyekiti wa mtandao |
mwenyekiti wa mtandao akizungumza na marafiki |
Jumatatu, 1 Februari 2016
Haki elimu yakusanya maoni kuhusu lugha ya kufundishia
shirika la Haki elimu linakusanya maoni ya wananchi kupitia mtandao wake wa twitter juu ya mapendekezo ya lugha ya kufundishia kama iwe KISWAHILI au KIINGEREZA unaweza kushiriki kwa kuwafuata kwenye ukurasa wao wa twitter kwa anwani ya @hakielimu
shiriki kwa kupiga kura yako je lugha ipi ungependa itumike kufundishia?
shiriki kwa kupiga kura yako je lugha ipi ungependa itumike kufundishia?
Jumatatu, 25 Januari 2016
shule ya msingi Mwisenge B yafanikiwa kupata darasa la tehama
darasa la tehama shule ya msingi Mwisenge B |
baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye chuma cha tehama |
awali shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu liliweza kuichukua shule ya Mwisenge A na B na kuiingiza katika mipango yake na kuifanya shule ya mfano na kuweza kujenga Maktaba ya kisasa kabisa shuleni hapo pamoja na kukarabati madarasa ya awali (chekechea ( kwa kutoa vifaa vya kufundishia na kujifunzia pamoja na kuwapeleka walimu wa madarasa ya awali mafunzo.
mwalimu wa tehama shule ya msingi Mwisenge B |
licha ya hayo shirika hilo pia limekuwa likitoa motisha kwa baadhi ya wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni hapo hasa katika mpango uliouanzisha shuleni hapo wa vilabu vya masomo,ambapo vilabu hivyo vya masomo vimekuwa vikisaidia sana kuhakikisha vinamaliza kabisa tatizo la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika shuleni hapo.
baada ya jitihada kubwa za shirika la Haki Elimu hivi karibuni wadau wengine wa elimu wamejitokeza na kuweza kuisaidia shule hiyo kwa kuipatia computer 17 pamoja na projector 3 na kuifungia shule hiyo huduma ya internet ya uhakika jambo linaloonyesha nia ya kuitoa shule hiyo ilipokuwepo na kuipaisha zaidi kitaaluma .hivi karibuni kumekuwepo na mipango mbalimbali ya kuifanya shule hiyo kuwa kituo cha tehama kwa shule za msingi musoma mjini ,jambo litakalo kuwa zuri ikizingatiwa kuwa shule ya msingi Mwisenge ndipo aliposoma baba wa taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere.pamoja na iongozi wengine wakubwa kama kina jaji Sinde Joseph Warioba.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)