Hatimaye
Baraza jipya la Mawaziri limetangazwa , tumeshuhudia mabadiliko katika
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambapo Naibu Waziri wa Elimu wa
sasa ni Mh. Jenista Mhagama amechukua nafasi ya Mh. Philipo Mulugo. Wako
watanzania wanayaona mabadiliko haya kutokuwa na tija huku wengine
wakiamini mabadiliko yanaweza kutokea, wote wana sababu za msingi kabisa
kuamini kile wanachoamini. Je mdau wa elimu ni mambo yapi Uongozi wa
sasa unatakiwa kuyazingatia/kuyafanya ili kuhakikisha kiwango cha elimu
nchini kinapanda na wanafunzi kote nchini wanapata elimu bora? Tafakari
na tushikirikishane
chanzo haki elimu facebook page
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni