| Rozi John olimo rafiki wa elimu na mwanakikundi wa SAUTI ZETU CLUB |
harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania
Jumatano, 10 Aprili 2013
Jumatatu, 8 Aprili 2013
MARAFIKI WA ELIMU WAKIFANYA UTAMBULISHO KWENYE MKUTANO WA WANANCHI WA KATA YA KIGERA
Juma Richard na bi. Perus masokomya walipokaribishwa na uongozi wa erikali ya mtaa wa kigera kwenda kutambulisha rasmi harakati za marafiki wa elimu
harakati za marafiki wa elimu ni harakati za mashirika, taasisi na watu wanaojali wenye nia ya kuboresha elimu na demokrasia nchini Tanzania, kubadilishana mawazo na maoni yao katika masuala ya elimu na kuchukua hatua kwa ajili ya kuleta mabadiliko. harakati zitachangia kubadili mifumo ya shule ziweze kutoa elimu bora kwa kuzingatia misingi bora ya utawala na haki za binadamu
njoo tupaze sauti zetu pamoja
Ijumaa, 5 Aprili 2013
AZIMIO LA MUSOMA NA WAJIBU WA WALIMU
Tukiziendeleza hizo gharama tutapata taabu sana. watoto hawatasoma . itachukua muda mrefu sana kabla watoto hawajasoma.....ukimaliza elimu yako ya sekondari umemaliza elimu yako
Unakwenda ama kufanya kazi au unakwenda katika chuo kinachofundisha kazi .......kuna kipindi katika maisha yako cha kusoma halafu baadaye kuna kipindi cha kazi Haya mawazo si mazuri........''
mwl jk nyerere tarehe 8 februari 1975
Jumatano, 3 Aprili 2013
MWL J.K NYERERE TUJISAHIHISHE
makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi chama kinachopenda ukweli na haki hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo.kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa na kupoteza nafasi zao,wanafanya kosa kubwa la unafsi,ambalo ni adui wa haki na ukweli
jk nyerere. - tujisahihishe
may,1962.
Ijumaa, 22 Machi 2013
Mara nyingi tumeliona suala la upatikanaji wa elimu bora kama ni suala la serikali peke yake na kusahau kuwa jamii nzima inajukumu la kusimamia elimu
tunajiuliza maswali mengi sana juu ya kuzidi kudolola kwa elimu nchini mara nyingi tumemtafuta mchawi bila kumpata na hata tunasahau kuwa wachawi wa tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu ni sisi wenyewe
hapo ulipo kama wewe ni mzazi ,mlezi ,au mwanajamii jiulize umewahi kufanya nini kusaidia sekta ya elimu umewahi kufuatilia na kutaka kujua juu ya elimu inayotolewa shuleni?
Juma richard ni mjumbe wakamati ya shule ya msingi hapa musoma anasema tangu amekuwa mjumbe wa kamati ya shule hajawahi kukutana na mzazi au mwanajamii aliyewahi kumuuliza juu ya mapato na matumizi ya shule pia hajawahi kuulizwa juu ya ruzuku za wanafunzi na hata ruzuku za maendeleo.
halii hii inamaanisha kwamba wengi wa wanajamii hawana muda wa kukaa na kutafakari juu ya elimu na mwisho wa siku huachia serikali peke yao na walimu ndiyo watoe elimu bora lakini pale tunapogundua kwamba tumefanya vibaya katika mitihani hapo utawasikia wazazi wengi wakilalamika kutaka kujua ni kwa nini.
wazazi wengi hawana muda wa kukagua madaftari ya watoto wao hawana muda wa kuzungumza na familia zao. walimu pia wanakatishwa tamaa na mazingira magumu ya kufundishia hivyo upelekea kutoa elimu isiyo bora na kuwaaminisha watoto kuwa elimu bora upatikana kwa masomo ya ziada yaani tution.
Kwa upande wake serikali inachukulia kushuka kwa elimu kama kitu cha kawaida na kusahau kuwa kuna wakati ruzuku za wanafunzi ucheleweshwa shule makusudi pia upelekwa zikiwa pungufu serikali usahau kwamba walimu wanaishi katika mazingira magumu sana ,shule hazina nyezo za kujifunzia na kufundishia
bajeti ya wizara ya elimu pia ni ndogo haikizi mahitaji bajeti kubwa uelekezwa kwenye utawala yaani posho za semina na kukarimu wageni.
lakini suala la kubadilika kwa mitaala limekuwa sugu na upelekea walimu kutokuielewa vizuri kwani hawana mafunzo juu ya mibadiliko hiyo.
kila mmoja ubaki akivutia kamba upande wake tujiulize ni wapi tumekosea tujisahihishe tufanye vema .
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)




