Rafiki wa elimu Juma Richard akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Mwisenge |
Tanzania ni moja ya nchi zenye watoto wenye mazingira magumu wenye ulemavu nk.
mara nyingi watoto wenye mahitaji maalum hawapewi kipaumbele cha kwanza mfano mzuri ni shule ya msingi Mwisenge.
Shule hii ni shule yenye watoto wenye mahitaji maalum hivi karibuni wana blog hii walipokuwa wanahojiana na watoto hawa wanakiri wazi kuwa vifaa vya kujifunzia ni changamoto kubwa sana kwao.
shule hii ina watoto wenye mahitaji maalum kama wenye albinism na mara nyingi watoto wa jinsi hii wanahitaji mazingira ya kuwafanya waone kwa ukaribu hasa pale mwalimu anapoandika ubaoni
Lakini pia shule hii ina watoto wenye ulemavu wa macho nk.
wanafunzi wote hawa wanabainisha upungufu wa vifaa vya kujifunzia pia wanaomba mwenye mapenzi na shule hii achangie upatikanaji wa vifaa.
marafiki wa elimu musoma tunatoa wito kwa wote wenye mapenzi ya dhati na shule hii ya Mwisenge aliposoma Mwalimu Nyerere wachangie kwa hali na mali kuhakikisha wanafunzi hawa wanapata mahitaji haya
kila mtoto ana haki ya kupata elimu awe na mahitaji maalum au asiwe na mahitaji maalum na jamii pia tunayo nafasi ya kuwasaidia watoto wetu kuhakikisha wanapata elimu bora.
Marafiki wa elimu Tunawasihii sana wana Musoma na Tanzania nzima kusaidia shule ya Mwisenge .
Shirika la HAKI ELIMU limejitolea na kujenga maktaba ya kisasa kabisa shuleni hapo sasa ni jukumu letu na sisi wana Musoma kuiboresha shule yetu ya Mwisenge.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni