rafiki wa elimu Juma richard okumu akiongoza kongamano la kujadili hali ya elimu wilaya ya musoma mjini |
kongamano la kujadili hali ya elimu wilaya ya musoma mjini lililofanyika shule ya msingi Mwisenge limeibua changamoto nyingi zinazochangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya ya musoma mjini.
akibainisha changamoto hizo mwakilishi wa afisa elimu msingi ndg. Mroba anasema siasa zinachangia kwa kiwango kikubwa kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani lakini pia anabainisha kuwa nidhamu, na wazazi kutokufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni pia inachangia,
lakini bado anakubaliana na hoja za washiriki kwamba serikali haiko makini katika kukabiliana na mabadiliko ya mitaala, na ucheleweshaji wa ruzuku za wanafunzi .
katika harakati za kupambana na changamoto ndugu Mroba kasema kuwa kwa sasa serikali imeongeza kasi ya ukaguzi katika shule nyingi za manispaa ambapo sasa zinafanyiwa ukaguzi mara mbili kwa mwezi,
licha ya baadhi ya washiriki kutofautiana na kauli ya ukaguzi wa shule mara mbili kwa mwezi afisa elimu huyo kasema kama bado ukaguzi haujafanyika katika shule zinazolalamikiwa basi atalifanyia kazi na nguvu ya ukaguzi itaonekana baada ya muda mfupi ujao.
Marafiki wa elimu musoma mjini ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hili wameahidi kufanya kazi na viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa kiserikali kuhakikisha elimu inainuka na kufikia kiwango bora.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni