Ripoti ya Tume ya Kuchunguza
Matokeo ya Kidato cha Nne iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
mapema mwaka huu, iliibua madudu mengi ambayo hayajawekwa hadharani.
Wajumbe waliounda kamati hiyo kwa nyakati tofauti waliliambia gazeti
hili hivi karibuni kuwa waligundua mambo mengi yanayodhihirisha udhaifu
mkubwa katika uendeshaji wa sekta ya elimu nchini. Sehemu
kubwa ya matokeo ya uchunguzi huo inasemekana yamejikita zaidi katika
kuzitupia lawama taasisi za Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) na
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Udhaifu wa kiutendaji kati ya taasisi hizo mbili unadaiwa umechangia
kwa wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani ya Kidato cha Nne
mwaka jana kiasi cha kuilazimisha Serikali kuunda tume kuchunguza tatizo
kutokana na kilio kikubwa cha wadau wa elimu na wananchi.
Viongozi watatu waandamizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi hawakupatikana kuzungumzia uchunguzi huo jana. Simu ya Waziri wa wizara hiyo, Dk Shukuru Kawambwa haikupatikana kabisa pale ilipopigwa.
Naye Naibu wake, Philipo Mulugo alijitetea kwamba alikuwa na shughuli
nyingi na hivyo hakuwa na muda wa kuzungumzia suala hilo wakati Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome hakupokea kabisa simu yake.
Matokeo hayo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwaka jana
yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 walipata
sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo
waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakiwa wamepata
daraja la nne. Katika mtihani huo, watahiniwa 397,136 walikuwa wa shule
na 68,806 wa kujitegemea.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu Pinda aliamua kuunda tume iliyoanza kufanya kazi kuanzia Machi hadi Juni mwaka huu. Tume hiyo iliyokuwa inaongozwa na Profesa Mchome ilimkabidhi Waziri Mkuu ripoti Juni 15, mwaka huu.Hata hivyo, ripoti hiyo haijawahi kutolewa hadharani baada ya tume kumaliza kazi yake.
Badala yake imeshuhudiwa Profesa Mchome, ambaye alikuwa Katibu
Mtendaji wa Taasisi ya Vyuo Vikuu Tanzania akipandishwa kuwa Katibu Mkuu
wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Huku
kwa upande mwingine, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk
Joyce Ndalichako akichukua likizo ya muda mrefu ya mapumziko.
Madudu yaliyogunduliwa na tume
Wajumbe wa tume hiyo walisema kuwa matokeo ya uchunguzi wao yalibaini
kuwa, maswali na mitihani iliyotungwa ilikuwa ni ile yenye kuzingatia
maudhui badala ya kuzingatia kujenga maarifa na ujuzi.
“Tulitegemea kwa vile tangu mwaka 2006, mihutasari ya elimu ya
Tanzania ilibadilika kutoka ile inayozingatia maudhui, kwenda kwenye ile
inayozingatia kujenga maarifa na ujuzi basi na mtihani ungekuwa na
mwelekeo huo,” alisema mmoja wa wajumbe wa tume ile.
Pia uchambuzi wa kamati ile uligundua kuwa hakukuwapo mawasiliano
kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta).TET, ambao ndio wasimamizi wa
mitalaa ya elimu walitakiwa kuhakiki mitihani ile baada ya kutungwa na
Necta, lakini hilo halikufanyika.
Chanzo kingine kililiambia gazeti hili kuwa tume hiyo ilibaini katika
uchunguzi wake kuwa Necta ilitumia wataalamu wasio na juzi wa kutosha
kutunga na kuhakiki mitihani. Uchunguzi
huo ulibaini baadhi ya mitihani kama ya masomo ya Hisabati, Kemia na
Fizikia ilikuwa na maswali yaliyohitaji muda mwingi wa kuyajibu kuliko
uliopangwa.
“Hii ilifanya wanafunzi kushindwa kukamilisha kujibu maswali yote
yaliyotakiwa kujibiwa kwenye mitihani hiyo. Pia tulibaini kwamba baadhi
ya maswali katika mitihani ya masomo ya Fizikia na Kemia yalikuwa nje ya
mihutasari iliyotumika kuwaandaa wanafunzi,” aliongeza mjumbe mwingine.Mjumbe mmoja aliongeza pia kuwa mitihani ilikuwa na misamiati migumu na hata kuwasumbua walimu walioisahihisha.
Hali hii inaweza kuwa imechangia, kwa kiasi kikubwa, kuongeza ugumu
wa mitihani hiyo na hili linaweza kuchangia wanafunzi kushindwa kuelewa
vizuri maswali wanayoulizwa kwenye mitihani.
Wajumbe wa tume hiyo walieleza hali hiyo imefanya imani kujengeka kuwa mitihani ya Tanzania ni migumu kuliko ya nchi nyingine.Huku
kwa upande mwingine, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk
Joyce Ndalichako akichukua likizo ya muda mrefu ya mapumziko.
Madudu yaliyogunduliwa na tume
Wajumbe wa tume hiyo walisema kuwa matokeo ya uchunguzi wao yalibaini
kuwa, maswali na mitihani iliyotungwa ilikuwa ni ile yenye kuzingatia
maudhui badala ya kuzingatia kujenga maarifa na ujuzi.
“Tulitegemea kwa vile tangu mwaka 2006, mihutasari ya elimu ya
Tanzania ilibadilika kutoka ile inayozingatia maudhui, kwenda kwenye ile
inayozingatia kujenga maarifa na ujuzi basi na mtihani ungekuwa na
mwelekeo huo,” alisema mmoja wa wajumbe wa tume ile.
Pia uchambuzi wa kamati ile uligundua kuwa hakukuwapo mawasiliano
kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Baraza la Mitihani la Taifa
(Necta).TET, ambao ndio wasimamizi wa
mitalaa ya elimu walitakiwa kuhakiki mitihani ile baada ya kutungwa na
Necta, lakini hilo halikufanyika.
Chanzo kingine kililiambia gazeti hili kuwa tume hiyo ilibaini katika
uchunguzi wake kuwa Necta ilitumia wataalamu wasio na juzi wa kutosha
kutunga na kuhakiki mitihani.Uchunguzi
huo ulibaini baadhi ya mitihani kama ya masomo ya Hisabati, Kemia na
Fizikia ilikuwa na maswali yaliyohitaji muda mwingi wa kuyajibu kuliko
uliopangwa.
“Hii ilifanya wanafunzi kushindwa kukamilisha kujibu maswali yote
yaliyotakiwa kujibiwa kwenye mitihani hiyo. Pia tulibaini kwamba baadhi
ya maswali katika mitihani ya masomo ya Fizikia na Kemia yalikuwa nje ya
mihutasari iliyotumika kuwaandaa wanafunzi,” aliongeza mjumbe
mwingine. Mjumbe mmoja aliongeza pia kuwa mitihani ilikuwa na misamiati migumu na hata kuwasumbua walimu walioisahihisha.
Hali hii inaweza kuwa imechangia,
kwa kiasi kikubwa, kuongeza ugumu wa mitihani hiyo na hili linaweza
kuchangia wanafunzi kushindwa kuelewa vizuri maswali wanayoulizwa kwenye
mitihani. Wajumbe wa tume hiyo walieleza hali hiyo imefanya imani kujengeka kuwa mitihani ya Tanzania ni migumu kuliko ya nchi nyingine.
mwananchi.co.tz
harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni