harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ijumaa, 28 Machi 2014
mwanafunzi bingwa wa hisabati na ndoto za udaktari
Unapomuona kabla ya kuzungumza naye, ni rahisi kuamini
kwamba Sunday Mrutu (18) ana hulka ya usikivu, upole na
kutafakari kabla ya kutamka ama kuchukua hatua yoyote.
Ndivyo ilikuwa wakati nikijiandaa kumhoji, muda mfupi baada
ya uongozi wa Shule za St. Anne Marie za jijini Dar es Salaam,
kumtunukia Sh milioni tatu, kutokana na mafanikio yake
katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne mwaka jana.
Mkurugenzi wa Shule za St. Anne Marie, Jasson Rweikiza,
Uanamtaja Mrutu kuwa kati ya wanafunzi wawili wa shule hiyo
waliopata kati ya pointi saba na tisa za daraja la kwanza, yeye
(Mrutu) akiwa na pointi saba.
Kwa upande mwingine, Rwekiza akasema Mrutu alikuwa
miongoni mwa wanafunzi 10 bora nchi nzima, akishika nafasi
ya sita, wakati aliongoza katika utahiniwa uliofanywa na
Baraza la Mitihani, kama ilivyo kwa hisabati aliyopata alama 98
kati ya 100.
Rwekiza anasema matokeo hayo na mengine hususani
yaliyowahusisha wanafunzi 32 wa St. Anne na shule dada ya
Brilliant, waliopata daraja la kwanza, yanajenga heshima kwa
vijana hao na uongozi wa shule hizo.
Tayari uongozi wa St. Anne Marie, Brilliant Sunshine, zote
zikimiliwa na Rwekiza, zimetoa jumla ya Shilingi milioni 13.2
kwa wanafunzi waliopata daraja la kwanza.
Zawadi hizo ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa na Mkurugenzi
wa shule hizo, Rwekiza, kwa wanafunzi waliohitimu kidato cha
nne mwaka jana.
Wanafunzi hao walipata kiasi tofauti cha fedha ambapo
waliofaulu kwa kati ya pointi 15-17 walikuwa 14 na
walizawadiwa Shilingi 200,000 kila mmoja.
Wengine na kiasi cha fedha alizopata kila mmoja ni 13
waliofaulu kwa kati ya pointi 13-14 (300,000), wanafunzi
watano waliofaulu kwa kati ya pointi 10-12 (500,000) na wawili
waliopata kati ya pointi 7-9 (1,000,000).
Hata hivyo, mwanafunzi aliyekuwa miongoni mwa wawili hao,
SundayMrutu alipewa zawadi tofauti kutokana na mafanikio
makubwa aliyoyapata katika mitihani hiyo.
Mwanafunzi huyo alizawadiwa Shilingi 1,000,000 kwa miongoni
mwa wanafunzi 10 bora nchini ambapo alishika nafasi ya sita
huku akiwa wa kwanza kwa upande wa wavulana.
Pia Mrutu alizawadiwa Shilingi 500,000 kwa kuwa wa kwanza
kwenye utahiniwa uliofanywa na Baraza la Mitihani la Taifa na
kiasi kama hicho kwa kuongoza katika somo la hisabati nchi
nzima, ambapo alipata alama 98.
Rwekiza, akasema ingawa fedha hizo zinaweza kuonekana kuwa
nyingi, lakini zitasaidia kuibua na kuhamasisha ari ya usomaji
kwa wanafunzi wa shule hizo na nyingine nchini.
“Tunalolifanya hapa kwa kutoa zawadi hizi za hamasa ni jambo
la kawaida kwa kila mwaka, lengo kubwa hapa ni kuhakikisha
watoto wetu wanaamini kwamba ahadi tunayowapa kuhusu
kusoma kwa bidii zinatekelezwa,” anasema.
Mrutu anathibitisha kwamba hisabati ni moja ya masomo
anayoyamudu darasani, hali hiyo ikichochewa na umakini,
usikivu na uelewa pindi mwalimu anapofundisha darasani.
“Hisabati inaaminika kuwa somo gumu sana, lakini ninaamini
kwamba kama mwanafunzi atakuwa msikivu, atatulia na
kufuata mafundisho ya mwalimu, itakuwa kinyume
chake….hisabati ni somo zuri na linaloeleweka kwa urahisi,”
anasema.
Mrutu anakumbuka namna alivyowafuatilia na kuwatii walimu
wake waliowahi kumfundisha hisabati, akiwataja kwa jina moja
moja kuwa Tarimo, Tino na Samuel.
Wakati Mrutu akisema hivyo, wanafunzi wa shule kadhaa za
sekondari wamekuwa wakilielezea somo hilo kama moja ya
masomo yanayowashinda katika kusoma na kufaulu.
KUHUSU UFAULU WAKE
Mrutu anasema hadi matokeo ya kidato cha nne yalipotoka na
kutaarifiwa kuhusu ufaulu wake, hakuamini kwa urahisi.
“Nilifuatwa nyumbani (bila kumtaja mtu aliyemfuata) na
kuambiwa kwamba nimefanikiwa vizuri sana kwenye mitihani
yangu,” anasema.
ANAPENDELEA UDAKTARI
Mrutu anasema pamoja na kuwa na uwezo unaomfanya
alimudu vyema somo la hisabati, kusudio lake ni kutaka
kusomea Udaktari.
“Ninajua hisabati ni somo muhimu lisilopewa kipaumbele sana
kwa madaktari, ila mimi nafsi yangu ni kuona ninasoma kufikia
kuwa Daktari wa binadamu,” anasema.
CHANGAMOTO KWA WANAFUNZI SHULENI
Mrutu, anasema ni jambo lililo wazi kwamba katika maisha ya
takribani miaka minne ya kusoma sekondari ya awali,
wanafunzi wanajenga urafiki na uhusiano wa karibu.
Hata hivyo, anasema kinachotakiwa kwa mwanafunzi ni kuweka
mipaka ya urafiki na uhusiano, kisha kusimamia dhamira, nia na
utashi vinavyomuongoza.
Anasema kukosekana kwa mipaka katika urafiki na uhusiano, ni
miongoni mwa vyanzo vya kuibuka tabia zisizofaa, nyingi kati ya
hizo zikitokana na kujifunza kunasababishwa na muingiliano wa
kirafiki ama kimahusiano.
“Sasa inapokuwa kwamba mpo marafiki wengi shuleni na
huwezi kuwakimbia, ni vizuri mwanafunzi ukajiepusha na kuiga
mambo, vinginevyo utajikuta unaachwa na wale uliokuwa
unawaiga, kwa maana kila mtu ana mbinu zake,” anasema.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Jumatano, 19 Machi 2014
madarasa walimu na vitabu bado changamoto
Shule ya sekondari Tongoni mkoani Tanga ina majengo
mazuri, walimu 12, maabara, vitabu lakini kitaifa inashika
nafasi ya tatu kutoka mwisho katika matokeo ya kidato cha
nne mwaka jana.
Shule hiyo, ina walimu 12 wengi wao wakiwa na elimu ya
kiwango cha shahada ya elimu. Ina madarasa manane,
madawati kwa kila mwanafunzi, maabara na vitabu vya
kutosha.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007 haijafaulisha
mwanafunzi hata mmoja kwa kiwango cha daraja la kwanza, la
pili wala la tatu. Daraja la kujivunia kwa shule hiyo kwenye
mitihani ya kidato cha nne ni la nne na sifuri kwa watahiniwa
wake.
Sasa shule hiyo ina wanafunzi wapatao 123 kati yao wasichana
ni 52 na wavulana 71.
“Ni wanafunzi watatu tu kati ya 47 walioweza kufaulu mtihani
wa kidato cha pili mwaka juzi … shule ikalazimika kuwatafutia
wanafunzi hao shule nyingine ili waendelee na masomo.
Waliobaki wakalazimika kurudia kidato cha pili,” alisema
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Mfaume Juma.
Mwalimu Juma anasema mwaka jana, watahiniwa wa kidato
cha nne walikuwa 37 wanafunzi saba kati yao hawakupata
matokeo yao kwa kushindwa kukamilisha ada ya mtihani na 28
wakaambulia daraja sifuri. Ni wawili tu walipata daraja la nne.
“Mwaka jana wanafunzi 28 walipata daraja sifuri katika mtihani
wa kidato cha nne, saba matokeo yao yalizuiwa na Baraza la
Mitihani la Taifa kwa kushindwa kulipa ada ya mtihani,”
anasema Mwalimu Mkuu huyo.
Miongoni mwa changamoto zinazoikabili shule hiyo, Mwalimu
Mkuu anazitaja kuwa ni mwamko mdogo wa baadhi ya wazazi
kuhusu umuhimu wa elimu hasa ulipaji wa ada na michango ya
shule bado ni tatizo kubwa.
Hatua hiyo, anasema inasababisha shule hiyo kushindwa
kujiendesha kikamilifu asilimia 75 ya wanafunzi wanadaiwa ada.
Changamoto nyingine ni ukosefu wa nyumba za walimu na
mabweni kwa wanafunzi. Asilimia 70 ya wanafunzi wa shule
hiyo huishi nje ya eneo hilo.
“Kutokana na ukosefu wa nyumba za walimu na mabweni kwa
wanafunzi baadhi ya wanafunzi wanachelewa kufika shule…
kuna wanafunzi wanaoishi katika kisiwa cha Mwarongo
ambacho ili kufika ng’ambo ya pili lazima wavuke kwa
mashua.Wakati mwingine hutegemea hali ya upepo wa bahari
siku ukivuma vibaya watoto wanashindwa kufika shuleni,”
anafafanua Mwalimu Juma.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wanasema, wamekuwa
wakishindwa kuhudhuria masomo kwa wakati au kuchelewa
hasa siku ambazo hali ya upepo wa bahari ukiwa mbaya.
“Mimi huwa naamka nyumbani saa 11 alfajiri, kuosha vyombo
na kuchota maji baada ya hapo najiandaa kwenda shule, lakini
ukifika Kivukoni ni lazima usubiri maji yajae ndiyo chombo
kiweze kuvuka.
Siku ambazo upepo ni mbaya mara kadhaa tulishawahi kuzama,
hali iliyotulazimu baada ya kunusurika turudi nyumbani badala
ya kwenda shule. Hii inatuumiza na kutuathiri sana
kimasomo,” anasema Mariam Hassan mwanafunzi wa kidato
cha kwanza shuleni hapo.
Naye Zuberi Hamid, mwanafunzi wa kidato cha tatu shuleni
hapo anasema, imekuwa ni kama kawaida kwao kutohudhuria
vipindi viwili vya kwa asubuhi kutokana na hali ya usafiri kuwa
ya mashaka na kimsingi hali hiyo imekuwa ni njia mojawapo
inayochangia kufeli masomo yao.
“Muda tunaoingia shuleni ni saa nne asubuhi unakuta vipindi
viwili vya mwanzo vimekamilika. Pia muda tunaotoka shule nao
hadi kuvuka na kufika nyumbani tunachelewa.Tukifika
nyumbani muda unakuwa umekwenda sana hata fursa ya
kujisomea inakuwa finyu sana, “ anasema Hamid.
Baadhi ya walimu wanasema , shule hiyo yenye walimu 12 kati
yao hakuna waliobobea katika masomo ya Biolojia, Fizikia na
Hisabati hali inayowalazimu wanafunzi kufanya mitihani ya
masomo hayo bila kufundishwa.
“Kwa sababu ya kutokuwa na walimu wa Physics,Hesabu na
Biology wanafunzi wanalazimika kufanya mitihani bila
kufundishwa masomo hayo hili nalo ni tatizo sana,” anasema
Thomas Simengwa, Mwalimu wa somo la Historia na Kiswahili
katika shule hiyo.
Omary Bushiri ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Tongoni
anakiri kuwepo mwamko mdogo wa wazazi katika uchangiaji wa
sekta ya elimu kijijini hapo sambamba na mmomonyoko wa
maadili kwa baadhi ya wanafunzi wa shuleni hiyo.
Bushiri ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya shule
hiyo, anasema changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo
pamoja na mambo mengine ni mawasiliano duni kati ya
uongozi wa shule, wazazi na wanafunzi.
“Ni ukweli kabisa kwamba maendeleo ya shule ya sekondari
Tongoni yamekuwa yakididimia siku hadi siku lakini tatizo lipo
kwa pande zote tatu kwa maana ya uongozi wa shule,
wanafunzi, walimu na bodi ilishaomba uongozi wa shule
kuandalia mkutano na wanafunzi lakini hadi leo jambo hilo
halijafanyika ,“ anasema Bushiri.
Anasema lengo la Bodi ya shule kutaka kukutana na wanafunzi
wa shule hiyo ni baada ya kufahamishwa kuwa walimu
wamekuwa na tabia ya kutoingia darasani kwa wakati na
wengine kuishia njiani bila kufika shule na tabia nyingine
ambazo ni kinyume cha maadili ya wanafunzi.
“Wanafunzi walishalalamika kwamba walimu hawaingii darasani
kwa wakati….lakini si hilo tu, pia wanafunzi wenyewe wana
matatizo yao mengi tu ujana umewazidi na ndio maana tulitaka
kuzungumza nao,” anasema.
Anasema anashangaa wanafunzi kuchelewa shule kwa
kisingizio cha usafiri wa mashua wakati kuna boti
inayowasafirisha bila kikwazo chochote na kwamba hilo ni
tatizo na uzembe wa ufuatiliaji wa wanafunzi kati ya uongozi
wa shule na wazazi.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tongoni, Luis Makame anasema
wakazi wa kata hiyo hawana mwamko katika uchangiaji wa
masuala ya elimu wakiamini kuwa elimu ya msingi inatosheleza
kuendesha maisha ya watoto wao.
“Kusema kweli, changamoto kubwa hapa ni uelewa wa wazazi
katika kuchangia sekta ya elimu.Wengi wanaamini kuwa, kila
mtoto ana riziki yake na kwamba elimu ya msingi inatosha
kabisa kuendesha maisha ya watoto wao ya kila siku, “ anasema
Makame.
Kwa upande wao, baadhi ya wazazi wa Kata ya Tongoni
wakizungumzia hali hiyo wanatupia lawama uongozi wa shule
na kusema kuwa umeshindwa kuwafuatilia wanafunzi wao na
baadhi wamekuwa na mienendo isiyofaa.
Selemani Sharif ni mmoja wa wazazi, ambaye anasema kuwa,
licha ya walimu kutoa malalamiko ya wazazi kutochangia ada
kikamilifu, lakini nao wameshindwa kusimamia uendeshaji wa
shule kwani hata wanafunzi nao wanalalamikia walimu
kutoingia madarasani kwa wakati.
“Sisi wazazi tunalaumiwa hatutaki kuchangia maendeleo ya
shule, lakini walimu nao wanalalamikiwa na wanafunzi
kutoingia madarasani na si hilo tu, uongozi wa shule
umeshindwa kusimamia tabia za wanafunzi wao ambao
tunawakuta vichochoroni wakati wa masomo na hiki kichaka
ndiyo gesti yao, walimu wanakuwa wapi wakati huo hata
wanafunzi wazurure ovyo,” anahoji Sharif.
Naye Mwajuma Mwanajumaa anaiomba serikali kufanya
mabadiliko ya uongozi wa shule hiyo kwa sababu wazazi
hawaridhishwi na matokeo ya shule hiyo.
“Shule hii wakati ikijengwa wananchi tuliichangia…kuitokana
na umuhimu wake kama kweli hatupendi elimu ilikuwaje
tulitoa nguvu zetu hadi ikajengwa…walimu na uongozi wa
shule umetukatisha tamaa sana… sasa ili twende vizuri
tunaiomba serikali iingilie kati suala hili,” anasisitiza
Mwanajumaa.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ambaye pia
ni Ofisa elimu Sekondari wa Jiji hilo , Bashiri Shelimo anasema
hatua ya kwanza itakayochukuliwa ni kuuondoa uongozi mzima
wa shule hiyo.
Shelimo anasema, hatua ya pili ni kuhamisha walimu wa shule
hiyo na kuwapeleka walimu wapya sambamba na kuunda upya
bodi ya shule hiyo.
Anasema changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo hadi
kufikia katika hali hiyo mbaya ni uongozi mbovu uliodumu kwa
muda mrefu unaofanya kazi kwa mazoea.
“Nina miezi kadhaa tangu nilipohamia hapa lakini kwa
uchunguzi wangu wa awali nimeona kuna haja ya kuupangua
uongozi wa shule hiyo.
Bahati nzuri Mwalimu mkuu mwenyewe aliomba yeye na
makamu wake wapumzishwe na tukaona ni sababu za msingi ili
kuleta mabadiliko chanya kwenye shule ile,” anafafanua Ofisa
elimu huyo.
CHANZO: NIPASHE
Jumapili, 16 Machi 2014
Baadhi ya wanafunzi wa kiume katika shule za msingi wilayani Kibaha, Pwani, wamejiingiza katika vitendo vya kujaamiana wenyewe kwa wenyewe na watu wengine kutoka nje ya shule na kufikia hatua ya kupasua kaptula zao makusudi ili kurahisisha vitendo hivyo.
Shule hizo zipo katika mji wa Mlandizi mkoani humo na vimesababisha wanafunzi hao kuporomoka kimasomo kwa kuwa wanatumia muda mwingi kukaa machimbo ya mchanga na vichakani kwa ajili ya kufanya vitendo hivyo.
Katika uchunguzi uliofanywa na NIPASHE imebainika vitendo hivyo hufanywa nyakati za asubuhi wakati vipindi vya masomo vinaendelea na jioni mara wanapotoka shuleni.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo, mahudhurio ya wanafunzi kwenye shule hizo yamekuwa ya kusuasua na kusababisha walimu kuwa na kazi ya ziada ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.
Uchunguzi huo umefanywa katika shule za msingi za Mtongani, Azimio na Jamhuri zote zipo ndani ya mji huo wa Mlandizi.
HALI HALISI
Katika hali inayoonyesha kuwa ni mbaya kwenye shule hizo, baadhi ya wanafunzi wameonekana kuathirika kisaokolojia na kupungukiwa na uwezo wa kimasomo darasani.
Hata hivyo, afya za wanafunzi hao zipo hatarini kutokana na hofu ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa ukiwamo Ukimwi baada ya watu wazima kuhusishwa kuwaingilia.
Baadhi ya walimu wa shule hizo walipozungumza na gazeti hili walikiri kuwapo kwa vitendo hivyo na kwamba vimeongezeka kwa kasi ya kutisha na kuwapa hofu.
Walisema walengwa wa vitendo hivyo ni wanafunzi kuanzia darasa la tatu hadi la nne ambao mara nyingi wanalazimishwa kulawitiwa na wanafunzi wenzao wa madarasa ya juu.
Aidha imedaiwa wanafunzi wengine wanafanyiwa vitendo hivyo na watu wazima wakiwa nyumbani kwao na kwenye mabanda ya kuonyesha picha za video nyakati za usiku.
"Tatizo hili limekuwa kubwa, walimu tumejitahidi kupambana nalo kwa kiasi kikubwa lakini inaonyesha hatujafanikiwa," alisema Mwalimu Jamila Kipengele wa Shule ya Msingi Mtongani.
Mwalimu Kipengele ambaye anaongoza kitengo cha taaluma, alisema vitendo hivyo vinafanyika katika maeneo hayo ambapo huko wanafunzi wanakutana mara wanapofanikiwa kutoroka wakati wa vipindi vya masomo.
"Tunavyosikia huko machimbo wanakuwa watoto kutoka shule tofauti na kutendeana matendo hayo machafu, baada ya kugundua jambo hilo tuliamua kufanya msako mkali wa kuwakamata wote wanaohusika na kuwarudisha shuleni," alisema Kipengule.
Kwa shule ya Azimio, Mwalimu Emmanuel Mwambeja ambaye anafundisha darasa la tatu, alieleza nusu ya wanafunzi 98 wa darasa lake hawaingii darasani katika vipindi vya jioni na badala yake wanaishia kwenye machimbo.
Mwalimu Tetula Kessy wa Shule ya Msingi Azimio, ambaye yupo kwenye kamati ya kuzuia unyanyasaji wa watoto chini ya Plan Tanzania, alisema wanafunzi wengi wanajikuta wakiingia katika vitendo hivyo kutokana na kushawishiwa na watu wazima na kuangalia picha za ngono kwenye mabanda yaliyozunguka kila eneo kwenye shule hizo.
"Tunapokaa na kuwauliza kwa nini wanafanya hivyo, wanajibu kwamba walikuwa wakifanyiwa nyumbani au wanaona kwenye vibanda vya video na wao wanajaribu kwa wenzao," alisema Mwalimu Kessy.
WATOTO WAPASUA KAPTULA ZAO
Katika Shule ya Msingi Jamhuri baadhi wanafunzi wameeleza upo wakati wanafunzi walifikia hatua ya kupasua kaptula zao upande wa nyuma ili kurahisisha kuingiliwa na wenzao.
Baadhi ya wanafunzi ambao majina yao yanahifadhiwa, walisema wanafunzi hao walikuwa na kawaida kwenda kwenye korongo lililo jirani na shule hiyo na kisha kulawitiana.
"Wanachana kaptula sehemu ya nyuma kwa kutumia wembe, tulikuja kugundua wanaporudi darasani wanakuwa katika hali tofauti ndipo tukaamua kuripoti kwa walimu," alisema mwanafunzi mmoja.
Kauli za wanafunzi hao ziliungwa mkono na Mratibu wa Elimu Kata ya Kilangalanga, Thomas Tito, ambaye alisema amefanya juhudi kubwa kupambana nalo wakati alipokuwa Mwalimu Mkuu katika shule hiyo.
"Nakumbuka nilipokuwa naongoza shule hiyo niliwakuta wanafunzi wamepasua kaptula zao kwa nyuma na wembe, nilipodadisi niligundua wanafanya mchezo huo hatari kwa sababu wanapotoka huko vichakani wanakuwa wamechafuka sana," alisema.
Kufuatia hali hiyo aliamua kuripoti katika vyombo vya sheria kwa ajili ya kuchukuliwa hatua lakini ilishindikana baada ya kuonekana watoto hao walikuwa wakilawitiana wenyewe kwa wenyewe.
"Polisi walishindwa kuendelea kufuatilia na kuachia jukumu hilo uongozi wa shule, nilichofanya niliwaita wazazi kuwaeleza jambo hilo pamoja na kuwachukulia hatua ya kinidhmu wahusika," alisema mwalimu Tito.
MABANDA YA VIDEO
Hata hivyo, taarifa za uhakika zinaeleza kwamba kinachoendelea ndani ya mabanda ya video yaliyotapakaa kila kona ya mji wa Mlandizi, ni mambo ya kutisha.
Imeelezwa kwamba ndani ya mabanda hayo, wamiliki wanaweka picha za ngono bila kujali muda wala umri wa wateja wao, kinachotokea wanaume watu wazima wanawachukua watoto waliokuwamo ndani na kuwaingilia kinyume na maumbile.
Baadhi ya wanafunzi waliotoa ushuhuda huo (majina yamehifadhiwa) walisema mara picha hizo zinapoonyeshwa, wanaume hao wanawadanganya watoto kwa kuwapa pesa kidogo na kisha wanawapakata na kuwaingilia.
"Kule watu wakubwa wanapakata watoto halafu wanawavua nguo kuwafanyia mambo mabaya," alisema mwanafuzi mmoja.
Wanafunzi wengine mara baada ya kuangalia picha hizo, wakienda shuleni wanawachukua wanafunzi wenzao na kwenda kuwafanyia jambo hilo.
"Tuna mwanafunzi mwezetu hapa shuleni (jina analitaja) amekuwa na tabia ya kuwaingilia wenzake kinyume na maumbile," alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Akizungumzia suala hilo, Mwalimu Kipengele alisema kinachozungumzwa na wanafunzi hao ni jambo la kweli, tayari wamembaini mtoto huyo na kumchukulia hatua ikiwamo kuwaita wazazi wake.
"Mwanafunzi huyu mahudhurio yake ni mabaya sana, tulipomfuatilia na kumbana sana alikiri kuhusika, na watoto waliofanyiwa vitendo hivyo walijitokeza tunaendelea kuwapatia ushauri nasaha,"alisema Mwalimu Kipengele.
Aliomba serikali kuangalia upya utoaji vibali vya kuendesha biashara hiyo, kwani kuna hatari wanafunzi wengi wakaathirika na vitendo hivyo na kuambukizwa Ukimwi pamoja na kushuka kiwango cha elimu kwa ujumla.
Hata hivyo wamiliki wa mabanda hayo wanapinga kauli hizo kwa kusema vibali vyao vimewapa masharti ya kutoonyesha picha za aina hiyo, endapo kuna watu wanafanya hivyo basi hawaendeshi biashara zao kihalali.
Twaha Linde ambaye alikutwa akionyesha video katika banda lililojengwa jirani na shule ya Msingi Mtongani, alisema kwa upande wake hajawahi kuonyesha picha hizo.
Pamoja na utetezi huo, ndani ya banda hilo walikuwapo wanafunzi zaidi ya 10 wa shule tofauti wakifuatilia picha, licha ya muda huo wa saa 6:00 mchana walitakiwa kuwapo darasani.
WAZAZI LAWAMANI
Walimu wamelaumu wazazi kwa kutokuwa na utaratibu mzuri wa kufuatilia maendeleo ya watoto wao kila siku.
Walisema hata wanapopewa taarifa ya watoto wao kutofika shule au kuhusishwa na tabia hizo wanawakingia kifua na kuwa wakali.
"Inakuwa tabu pale tunapowapa taarifa wazazi juu ya tabia za watoto wao, mara nyingi wanakuja wakiwa wakali na kusema tunawaongopea, mara nyingi inabidi kutumia mbinu za kuwahoji mbele yao na wanapobaini kuna ukweli wanabaki wakilia," alisema Mwalimu Tito.
Aliomba wazazi kuwa na taratibu ya kuchunguza tabia za watoto wao na kufuatilia maendeleo yao ya kielimu kwa ajili ya kuwajengea maadili mema.
"Sisi tunasaidia kurekebisha pale wanapokuja shuleni, lakini wakiwa nyumbani hawana udhibiti na ndiyo maana hali hii inazidi kuongezeka huku wazazi hawana habari," aliongeza kusema.
Hata hivyo Zuhura Yusufu (30) mkazi wa Mlandizi, alisema kinachosemwa na walimu wa shule hizo kina ukweli kwani wazazi wengi hawawajibiki ipasavyo katika malezi ya watoto wao.
Alisema kuibuka kwa hali hiyo kutawazindua wazazi wenzake kwa kuanza kuwafuatilia watoto mara kwa mara
OFISA ELIMU ANENA
Ofisa Elimu wa shule za Msingi wa Wilaya ya Kibaha, Winfrida Mbuya, alipozungumza na NIPASHE Jumapili, alisema suala hilo limeenea katika shule nyingi na kuwa la kijamii kutokana na wanaohusika hutoka ndani ya familia.
Alisema ofisi yake inaandaa tathmini ya jumla kujua ukubwa wake ili kuandaa mkakati wa ufuatiliaji kwa kuchukua hatua mbalimbali ikiwamo kutoa elimu ya ushauri kwa watoto walioathirika.
"Ni vizuri tukashirikiana pamoja kuwatambua watoto walioathirika ili waweze kupewa ushauri na wale waliohusika na unyama huo kuchukuliwa hatua za kisheria," alisema.
RC: IMENISHTUA SANA
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwamtumu Mahiza, amesema ameshtushwa na jambo hilo, na kwamba atakahakikisha anakutana haraka na viongozi wenzake kulifuatilia.
Alisema yeye kama kiongozi wa juu katika eneo hilo hataweza kuzungumza chochote kabla ya kukutana na wenzake.
"Mimi nimeshtuka sana lakini sitaweza kusema kitu kwa sababu bado viongozi wenzangu ngazi ya Wilaya na Halmashauri sijakutana nao, nipe muda nitatoa tamko langu," aliongeza kusema.
Alhamisi, 13 Machi 2014
siri ya kufanya vibaya matokeo ya kidato cha 4 kwa shule za serikali
Miongoni mwa habari zilizoripotiwa katika gazeti hili jana ni
pamoja na ripoti maalum iliyofichua baadhi ya sababu za
kufanya vibaya kwa wanafunzi wa moja kati ya shule 10 za
sekondari zilizoburuta mkia katika mtihani wa taifa wa kidato
cha nne uliofanyika mwaka mwishoni mwa 2013.
Katika shule hiyo iitwayo Mvuti, iliyopo kwenye Kata ya
Msongola, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam, ni mtahiniwa
mmoja tu aliambulia daraja la tatu. Wengine watatu walipata
daraja la nne huku 40 waliobaki wakipata daraja sifuri na
mwishowe shule hiyo ikashika nafasi ya 3,251 kati ya 3,256
zilizokuwa kwenye kundi la sekondari zenye watahiniwa 40 au
zaidi.
Ripoti hiyo inaonyesha kuwa shule ya Mvuti ina changamoto
nyingi zinazokwaza maendeleo yao kitaaluma. Uwezo mdogo
wa wanafunzi wanaoripoti katika shule hiyo, ukosefu wa vitabu
vya ziada na kiada, tatizo la usafiri, njaa kwa wanafunzi na pia
kukosekana kwa mkuu wa shule ni baadhi ya matatizo
yanayoikwamisha shule hiyo.
Sisi tunaona kuwa matatizo haya lukuki yanayoikabili Mvuti
yanapaswa kutafutiwa ufumbuzi haraka. Ni wazi kuwa hatua
sahihi zisipochukuliwa sasa, Mvuti na shule nyingine za umma
zenye changamoto zinazofanana nayo zitaendelea kupata
matokeo mabaya katika kila mwaka; jambo ambalo halipaswi
kuachwa hivi hivi.
NIPASHE tunajua kuwa nyingi kati ya changamoto zinazoikabili
Mvuti na shule nyingine za aina yake zinaweza pia
kushughulikiwa na uongozi wa shule husika.
Halmashauri za manispaa na wilaya ambazo ni miongoni mwa
wamiliki wa shule hizi, zinapaswa pia kutekeleza majukumu yao
kwa ukamilifu, sawa na serikali kuu na wadau wengine wa sekta
ya elimu nchini.
Jambo muhimu ni kuwa na dhamira ya dhati kwa kila upande,
kwa maana ya viongozi wa shule, wanafunzi, wazazi, serikali na
wadau wengine.
Kwa mfano, inaelezwa kuwa awali, Mvuti haikuwa na bodi kwa
miaka miwili. Hili ni tatizo linalochangia kuwapo kwa matokeo
mabaya kwani kupitia bodi, ndipo shule huwa na fursa nzuri ya
kujiwekea malengo na kuyasimamia.
Lipo pia tatizo la usafiri na njaa. Baadhi ya wanafunzi wa Mvuti
hulazimika kupanda mabasi sita hadi nane kwa safari ya kutoka
nyumbani kwenda shule na kurudi, achilia mbali safari nyingine
ya kutembea kwa miguu umbali wa takriban kilomita nane kwa
safari mbili kutoka katika kituo cha mabasi cha Mvuti hadi
shuleni kwao. Matatizo ya aina hii huwakabili pia wanafunzi wa
shule nyingine nyingi zilizo pembezoni mwa miji.
Shule hiyo pia hukabiliwa na tatizo la kupokea baadhi ya
wanafunzi wasio na uwezo darasani.
Ripoti inaonyesha kuwa asilimia 70 ya wanafunzi walioripoti
mwaka 2011 ili kuanza kidato cha kwanza walikuwa hawajui
kusoma wala kuandika.
Aidha, inaelezwa kuwa ni wanafunzi watatu tu ndiyo waliofaulu
kwenye mtihani wao wa kidato cha pili miongoni mwa wale
waliofeli sana mwaka huu na kuifanya shule ya Mvuti iingie
katika orodha ya shule 10 zilizofanya vibaya.
Ni wazi kuwa kama taratibu zingefuatwa, shule hiyo isingepata
matokeo hayo mabaya kwani wale waliofeli kidato cha pili
wangepata nafasi ya kukariri darasa na wala siyo kuvushwa
kirahisi na mwishowe kushusha ufaulu wa shule hiyo.
NIPASHE tunaamini kuwa bodi ya shule ya Mvuti, kwa
kushirikiana na wazazi wa wanafunzi na wadau wengine wa
elimu, wanaweza kubuni utaratibu mzuri wa kukabiliana na
tatizo la usafiri, maji na chakula kwa watoto wao.
Mipango ya kujenga mabweni zaidi kwenye shule za
pembezoni kama Mvuti ni muhimu. Aidha, Wizara ya Elimu
inapaswa kuangalia vyema mfumo wake wa kuwapima
watahiniwa wa darasa la saba ili wanafunzi wote
wanaochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wawe na sifa
sahihi kwani ni vigumu sekondari hizi za kata kupata matokeo
mazuri ikiwa zitaendelea kupokea wanafunzi wasiojua kusoma
wala kuandika.
Njia pekee ya kuzikomboa shule za kata kama Mvuti ni
kushughulikia kero zilizopo. Kwa kufanya hivyo, nazo
zitaimarika na kupandisha viwango vyao vya ufaulu.
Ijumaa, 7 Machi 2014
kauli ya Kawambwa yawachefua walimu
waziri wa elimu dk. shukuru kawambwa |
CWT imesema kauli hiyo ya serikali ni kutafuta visingizio baada ya kushindwa kutekeleza ahadi yake kuwa ifikapo Februari, mwaka huu deni la walimu litakuwa limelipwa.
Rais wa CWT, Gration Mkoba, alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Alisema majadiliano ya mishahara ya walimu yalitokana na mgomo wa 2012 baada ya kukaa kwenye meza ya majadiliano na serikali ilikubali kulipa deni na kuandaa utaratibu wa kupandisha walimu madaraja.
“Inasikitisha kuona majadiliano yanahusisha waandishi wa habari bila ya kujua kuwa kwa kauli yake waziri tayari walimu wameingia kwenye mgogoro na serikali, lakini nawasihi walimu wasubiri tamko rasmi la mgogoro,” alisema.
Mkoba alisema tangu serikali ilipoahidi kutekeleza madai yao, hakuna hata dai moja lililotekelezwa lakini imewashangaza kuona ikijinadi kuwa inaendelea na majadiliano ya kulipa deni hilo wakati majadiliano hayana tija kwa mwalimu.
Alisema Novemba, mwaka jana mkutano mkuu wa CWT ulitoa siku 60 kwa serikali kukamilisha taratibu zote la kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu nchini.
Pia Januari mwaka huu kwenye kikao cha Baraza la Taifa la CWT kiliazimia kuwa ifikapo mwishoni mwa Februari, mwaka huu, ikiwa serikali itashindwa kulipa malimbikizo hayo litakuwa tayari kuongoza mgomo.
CHANZO:
NIPASHE
bunge la katiba lakiuka katiba ya tanzania ibara ya 18
Bunge
la Katiba limeamua kuweka kitanzi kwa uhuru wa wananchi kupata habari
za mchakato wa Katiba Mpya, kwa kuwazuia waandishi wa habari kuingia
kwenye Kamati 12 za wajumbe wa Bunge hilo zitakazojadili Rasimu ya
Katiba.
Mjadala mkali ulizuka kwa juzi na jana kwenye Bunge hilo, huku baadhi ya wajumbe wakitaka uhuru wa wananchi kupata habari uwapo kwa waandishi kuruhusiwa kuingia kwenye kamati na wengine wakiwamo wajumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti wakipinga vikali kwa kutaka waandishi wapewe taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kamati husika.
Kifungu cha 57 fasili ya kwanza ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, kinaeleza kuwa vikao vyote vya kamati vitakuwa vya faragha na hakuna mtu yeyote asiyekuwa mjumbe wa kamati, mtumishi wa Bunge au mtaalam aliyeitwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakayeruhusiwa kukaa katika sehemu yoyote ya ukumbi wa mikutano ya kamati wakati kikao cha faragha kinaendelea.
Fasili ya tatu, inaeleza kuwa bila kuathiri masharti ya kanuni hii Mwenyekiti wa Kamati ya mjumbe yeyote kwa idhini ya Mwenyekiti anaweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mambo yaliyojitokeza kwenye kikao cha kamati.
Baadhi ya wajumbe waliiomba kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kifungu hicho, walitaka waandishi wa habari kuruhusiwa kwani kwa kuwazuia ni kwenda kinyume cha ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotaka kuwapo kwa uhuru wa kupata taarifa.
OLUOCH
Ezekiel Oluoch alisema anashauri vikao viwe wazi kwani hakuna jambo la siri la kujifungia kwani wananchi wana haki ya kujua kinachojadiliwa kwenye kamati na kwamba ni vyema kamati zikawa huru.
HALIMA MDEE
Halima Mdee alisema wenye jukumu la kuzitengeneza kanuni ni wajumbe na kwamba awali kamati ya kanuni na kumshauri mwenyekiti baada ya majadala mkubwa kamati ilipendekeza waandishi waruhusiwe kuingia kwenye vikao, na ikakubaliwa kwenye vikao vya kamati ambavyo vitakuwa na mijadala mikubwa na watakapokuja kwenye Bunge watafanya majumuisho kwenye manbo yaliyojadiliwa.
“Tulikubalina watu watakaokatazwa ni wananchi wa kawaida kutokana na
udogo wa kumbi, ila waandishi wa habari wakubaliwe, sisi ndiyo tunaopitisha kanuni na sisi tuliridhia ilikuwa ni matarajio yetu,”
alisema.
Alisema waliotajwa kwenye kanuni waruhusiwe kuingia na utaratibu utakaotumika uamuliwe na mwenyektii wa kamati kushauriana na makamu mwenyekiti.
“Waandishi wa habari waingie mnaogopa nini, mnaficha nini?...hii Katiba ni ya wananchi wana haki ya kujua kila kinachoendelea ndani ya kamati na nje ya kamati na kwenye ukumbi wa Bunge,” alisema Mdee.
MOSES MACHALI
Moses Machali alipendekeza fasili ya tatu ya kifungu hicho, ifutwe kwa kuwa inaweka kitanzi kwa uhuru wa wananchi kupata habari na hakimlazimishi mwenyekiti au makamu kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.
Alisema vikao vyote vifanyike kwa uwazi bila kuzuia mtu ingawa hawataruhusiwa kushiriki kwenye mjadala wa kamati.
“Hao wanaosisitiza kura ya wazi halafu mnaogopa na kuwakataa waandishi wa habari mnaficha nini, sioni sababu ya msingi,” alisema Machali.
MARIA SARUNGI
Maria Sarungi alisema vikao vya kamati viwe wazi kwa waandishi wa habari kwa kuwa Rasimu ya Katiba itakwenda kwao kwa ajili ya kuipigia kura.
“Mwanzo wa Rasimu ya Katiba unasema kwakuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua...Katiba hii si ya kwetu tuliokaa humu ndani bali ya wananchi wa Tanzania, mchakato ulivyoanza ilianza kwa wananchi hadi tulipofika,” alisema.
FREEMAN MBOWE
Freeman Mbowe alisema Katiba inayotungwa ni ya wananchi na wanaowakilishwa ndani ya Bunge hilo wanataka kujua kila kinachoendelea ndani ya Bunge hilo.
“Tusifikiri tunahitaji kuridhiana sisi wenyewe tulioko ndani ya Bunge hili kuna Watanzania kwa mamilioni wa vyama na taasisi mbalimbali wanatisikiliza,” alisema.
Wakati wajumbe huyo anazungumza, baadhi ya wajumbe walipiga kelele na kuzomea hali iliyomlazimu kuacha kuzungumza na mwenyekiti kumsihi kuendelea, lakini Mbowe alisema: “Siwezi kuendelea wakati wajumbe wanapiga kelele.”
MAHALU
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekti wa Muda,Prof. Costa Mahalu, alisema kamati yake inapeleka mapendekezo kwa wajumbe na wenye maamuzi ni wajumbe na baadaye wanaagizwa kurekebisha mwafaka uliofikiwa na kuonyesha msimamo wao kwa pamoja.
Mjumbe wa Kamati, Bakari Khamis Bakari, alisema hakuna uhuru usiokuwa na kinga kulingana na maelezo ya maeneo husika na kwamba kamati italichukua suala hilo na kujadailiana ili kupata namna bora ya kuruhusu waandishi wa habari kuchukua habari.
George Simbachawene, mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti, alisema maoni ya kamati ni kuwa hisia na sababu wanazotoa wajumbe hao zilikuwapo kwenye kamati yao na walipenda waandishi waruhusiwe ili mchakato huo uonekane kwa umma wote.
“Kilichotushinda na kufikia uamuzi wa maoni hayo ni utekelezaji wake...kwa busara yetu tukaliwekea utaratibu kwenye fasili ya tatu, vyombo vyetu vya habari ni vingi, kamati iko ukumbi wa Msekwa asubuhi anakuja mwandishi anachukua anapeleka, habari zitakazokwenda juu ya hoja moja jambo moja zitakuwa hazijakamilika zitawachanganya wananchi na si kuwasaidia,” alisema.
Alisema waandishi watachukua habari kivyao na kuwachanganya wananchi na ndiyo maana wameamua mwenyekiti wa kamati atoe taarifa kwa waandishi.
DK. MWAKYEMBE
Dk. Harrison Mwakyembe alisema kitaaluma ni mwandishi wa habari na mwanasheria na kwamba anaona hakuna haja ya waandishi wa habari kuruhusiwa kuwepo kwenye kamati na badala yake wapewa taarifa na mwenyektii wa kamati husika.
Hata hivyo, baadhi ya watoa hoja, walipinga hatua hiyo huku wanaopinga waandishi kuingia kwenye ukumbi wakishangilia kwa kupiga meza kusisitiza waandishi kunyimwa kuingai kwenye kamati hizo, huku wachache wa vyama wa upinzani wakipinga uamuzi huo.
DK. TULIA ACKSON
Mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri mwenyekiti, Dk. Tulia Ackson, alisema hakuna uhuru usiokuwa na mipaka na kwamba kamati inapendekeza kifungu hicho kubaki jinsi kilivyo.
Hoja hiyo ilimalizika kwa wajumbe kupitisha kifungu jinsia kilivyo kuwa waandishi hawataruhusiwa kuingia kwenye kamati na badala yake watapewa taarifa na mwenyektii wa kamati.
Mjadala mkali ulizuka kwa juzi na jana kwenye Bunge hilo, huku baadhi ya wajumbe wakitaka uhuru wa wananchi kupata habari uwapo kwa waandishi kuruhusiwa kuingia kwenye kamati na wengine wakiwamo wajumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti wakipinga vikali kwa kutaka waandishi wapewe taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa kamati husika.
Kifungu cha 57 fasili ya kwanza ya Kanuni za Bunge Maalum la Katiba, kinaeleza kuwa vikao vyote vya kamati vitakuwa vya faragha na hakuna mtu yeyote asiyekuwa mjumbe wa kamati, mtumishi wa Bunge au mtaalam aliyeitwa na Mwenyekiti wa Bunge Maalum atakayeruhusiwa kukaa katika sehemu yoyote ya ukumbi wa mikutano ya kamati wakati kikao cha faragha kinaendelea.
Fasili ya tatu, inaeleza kuwa bila kuathiri masharti ya kanuni hii Mwenyekiti wa Kamati ya mjumbe yeyote kwa idhini ya Mwenyekiti anaweza kutoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu mambo yaliyojitokeza kwenye kikao cha kamati.
Baadhi ya wajumbe waliiomba kuwasilisha mapendekezo yao kwenye kifungu hicho, walitaka waandishi wa habari kuruhusiwa kwani kwa kuwazuia ni kwenda kinyume cha ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayotaka kuwapo kwa uhuru wa kupata taarifa.
OLUOCH
Ezekiel Oluoch alisema anashauri vikao viwe wazi kwani hakuna jambo la siri la kujifungia kwani wananchi wana haki ya kujua kinachojadiliwa kwenye kamati na kwamba ni vyema kamati zikawa huru.
HALIMA MDEE
Halima Mdee alisema wenye jukumu la kuzitengeneza kanuni ni wajumbe na kwamba awali kamati ya kanuni na kumshauri mwenyekiti baada ya majadala mkubwa kamati ilipendekeza waandishi waruhusiwe kuingia kwenye vikao, na ikakubaliwa kwenye vikao vya kamati ambavyo vitakuwa na mijadala mikubwa na watakapokuja kwenye Bunge watafanya majumuisho kwenye manbo yaliyojadiliwa.
“Tulikubalina watu watakaokatazwa ni wananchi wa kawaida kutokana na
udogo wa kumbi, ila waandishi wa habari wakubaliwe, sisi ndiyo tunaopitisha kanuni na sisi tuliridhia ilikuwa ni matarajio yetu,”
alisema.
Alisema waliotajwa kwenye kanuni waruhusiwe kuingia na utaratibu utakaotumika uamuliwe na mwenyektii wa kamati kushauriana na makamu mwenyekiti.
“Waandishi wa habari waingie mnaogopa nini, mnaficha nini?...hii Katiba ni ya wananchi wana haki ya kujua kila kinachoendelea ndani ya kamati na nje ya kamati na kwenye ukumbi wa Bunge,” alisema Mdee.
MOSES MACHALI
Moses Machali alipendekeza fasili ya tatu ya kifungu hicho, ifutwe kwa kuwa inaweka kitanzi kwa uhuru wa wananchi kupata habari na hakimlazimishi mwenyekiti au makamu kutoa taarifa kwa waandishi wa habari.
Alisema vikao vyote vifanyike kwa uwazi bila kuzuia mtu ingawa hawataruhusiwa kushiriki kwenye mjadala wa kamati.
“Hao wanaosisitiza kura ya wazi halafu mnaogopa na kuwakataa waandishi wa habari mnaficha nini, sioni sababu ya msingi,” alisema Machali.
MARIA SARUNGI
Maria Sarungi alisema vikao vya kamati viwe wazi kwa waandishi wa habari kwa kuwa Rasimu ya Katiba itakwenda kwao kwa ajili ya kuipigia kura.
“Mwanzo wa Rasimu ya Katiba unasema kwakuwa sisi wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tumeamua...Katiba hii si ya kwetu tuliokaa humu ndani bali ya wananchi wa Tanzania, mchakato ulivyoanza ilianza kwa wananchi hadi tulipofika,” alisema.
FREEMAN MBOWE
Freeman Mbowe alisema Katiba inayotungwa ni ya wananchi na wanaowakilishwa ndani ya Bunge hilo wanataka kujua kila kinachoendelea ndani ya Bunge hilo.
“Tusifikiri tunahitaji kuridhiana sisi wenyewe tulioko ndani ya Bunge hili kuna Watanzania kwa mamilioni wa vyama na taasisi mbalimbali wanatisikiliza,” alisema.
Wakati wajumbe huyo anazungumza, baadhi ya wajumbe walipiga kelele na kuzomea hali iliyomlazimu kuacha kuzungumza na mwenyekiti kumsihi kuendelea, lakini Mbowe alisema: “Siwezi kuendelea wakati wajumbe wanapiga kelele.”
MAHALU
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekti wa Muda,Prof. Costa Mahalu, alisema kamati yake inapeleka mapendekezo kwa wajumbe na wenye maamuzi ni wajumbe na baadaye wanaagizwa kurekebisha mwafaka uliofikiwa na kuonyesha msimamo wao kwa pamoja.
Mjumbe wa Kamati, Bakari Khamis Bakari, alisema hakuna uhuru usiokuwa na kinga kulingana na maelezo ya maeneo husika na kwamba kamati italichukua suala hilo na kujadailiana ili kupata namna bora ya kuruhusu waandishi wa habari kuchukua habari.
George Simbachawene, mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti, alisema maoni ya kamati ni kuwa hisia na sababu wanazotoa wajumbe hao zilikuwapo kwenye kamati yao na walipenda waandishi waruhusiwe ili mchakato huo uonekane kwa umma wote.
“Kilichotushinda na kufikia uamuzi wa maoni hayo ni utekelezaji wake...kwa busara yetu tukaliwekea utaratibu kwenye fasili ya tatu, vyombo vyetu vya habari ni vingi, kamati iko ukumbi wa Msekwa asubuhi anakuja mwandishi anachukua anapeleka, habari zitakazokwenda juu ya hoja moja jambo moja zitakuwa hazijakamilika zitawachanganya wananchi na si kuwasaidia,” alisema.
Alisema waandishi watachukua habari kivyao na kuwachanganya wananchi na ndiyo maana wameamua mwenyekiti wa kamati atoe taarifa kwa waandishi.
DK. MWAKYEMBE
Dk. Harrison Mwakyembe alisema kitaaluma ni mwandishi wa habari na mwanasheria na kwamba anaona hakuna haja ya waandishi wa habari kuruhusiwa kuwepo kwenye kamati na badala yake wapewa taarifa na mwenyektii wa kamati husika.
Hata hivyo, baadhi ya watoa hoja, walipinga hatua hiyo huku wanaopinga waandishi kuingia kwenye ukumbi wakishangilia kwa kupiga meza kusisitiza waandishi kunyimwa kuingai kwenye kamati hizo, huku wachache wa vyama wa upinzani wakipinga uamuzi huo.
DK. TULIA ACKSON
Mjumbe wa Kamati ya Kanuni na Kumshauri mwenyekiti, Dk. Tulia Ackson, alisema hakuna uhuru usiokuwa na mipaka na kwamba kamati inapendekeza kifungu hicho kubaki jinsi kilivyo.
Hoja hiyo ilimalizika kwa wajumbe kupitisha kifungu jinsia kilivyo kuwa waandishi hawataruhusiwa kuingia kwenye kamati na badala yake watapewa taarifa na mwenyektii wa kamati.
CHANZO:
NIPASHE
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)