TAFAKARI
YA WIKI HII : Gazeti la RaiaTanzania limeripoti habari inayohusu shule
ya msingi katika mkoa wa Iringa yenye wanafunzi 600 ikiwa na mwalimu
mmoja tu (1), wakati huo huo Radio Uhuru imeripoti Shule moja mkoani
Shinyanga yenye wanafunzi takribani 500
wana matundu mawili (2) pekee ya vyoo .Gazeti la Mtanzania pia
limeripoti shule yenye wanafunzi 480 katika wilaya ya Serengeti ina
madawati matano tu (5).Muasisi wa Taifa letu , Mwalimu Nyerere alituasa
ili nchi iendelee tunahitaji mambo manne SIASA SAFI, ARDHI, UONGOZI
BORA NA WATU . Hakuna ubishi kwamba bado hatuna uongozi bora kwani
imepita miaka 50 tangu Uhuru kukiwa na awamu nne za uongozi lakini
changamoto kama hizi si ngeni miongoni mwa watanzania, Siasa yetu nayo
bado ina madhaifu hilo halina ubishi. Leo tuachane na UONGOZI MBOVU NA
SIASA MBOVU kabisa, tujiangalie SISI (WATANZANIA) kama wananchi
tujiulize tumefanya nini kuhakikisha tunaondokana na changamoto hizi? Je
ni kwa kiwango kipi tumefanikiwa katika yale tuliyofanya katika kuleta
mabadiliko ? Nini wajibu wetu watanzania katika kutatua changamoto
hizi?. Hii ni aibu kwetu sote, kwangu mimi, yule na wewe. Tafakari na
tujadili hatua zipi zichukuliwe kuhakikisha changamoto hizi
zinatatuliwa.
souce Haki Elimu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni