mkuu wa wilaya ya Arusha |
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongella, amesema mabadiliko ya haraka
katika elimu yanaweza kutokea iwapo walimu watawezeshwa kitaaluma na
kuwahimiza maafisa elimu kutoa motisha na kutambua mchango wa anayefanya
vizuri ili kuwajengea zaidi morali.
Mongella aliyasema hayo katika hafla maalum ya kutoa zawadi na vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha tatu waliofanya vizuri mitihani ya majaribio kwa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro katika masomo ya Hisabati, Elimu viumbe, Kemia, Fizikia na Kiingereza iliyoandaliwa na asasi ya Asante Africa Foundation , Africaid na Chuo Kikuu cha Elimu cha Mwenge kilichopo mjini Moshi.
“Kuendelea kwa nchi yoyote ile ni pale inapokuwa na wana sayansi wengi zaidi…mwanasiasa gani utaendesha nchi ambayo haina wanasayansi?” alihoji.
Alisema maofisa elimu wanaweza kuanzisha mradi kama huo wa kufanya majaribio ya mitihani kwa wanafunzi wa sekondari zilizopo kwenye mikoa yao au kwa kushirikiana na mikoa mingine.
“Hii ni changamoto kwa maofisa elimu, wanaweza kutenga hata Sh. milioni 10 kwa ajili ya walimu wa masomo hayo na kama wanafunzi watakuwa wamefanya vizuri wanaweza kuzawadiwa,” alisema.
Mongella alisema hata katika programu ya ‘Matokeo makubwa sasa’ inahitaji walimu waongezewe uwezo ili wanafunzi waweze kufanya vizuri zaidi na inawezekana kuwa hivyo kwa kuwashindanisha.
Kwa upande wake, meneja wa mradi huo wa uwezeshaji walimu wa shule za sekondari, Sokoro Munubi, alisema malengo yao yanaendana na mpango wa serikali unaosisitiza 'matokeo makubwa sasa' katika sekta ya elimu.
“Kwanza tunawajengea uwezo walimu kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara pamoja na kufanya ufuatiliaji wa mafunzo yanayotokana na walimu wao wenyewe katika maeneo ya shuleni.
Akizungumzia mafanikio ya mradi huo tangu kuanzishwa kwake, alisema umekwisha kufundisha walimu 80 wa sekondari 40 zilipo wilaya tisa za mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.
Alisema walimu 560 kutoka shule hizo nao wamekwisha kufundishwa na walimu wenzao katika maeneo ya shule zao na pia mradi umefadhili mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wa kidato cha tatu na kwamba wanafunzi 4,500 walishiriki kufanya mtihani huo.
Alisema kuanzia mwakani mradi huo unatarajia kuongeza mikoa miwili lengo likiwa kufikia mikoa sita kwa baadaye.
chanzo. ippmedia.com & nipashe