Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatatu, 29 Aprili 2013

Kongamano la kujadili hali ya elimu musoma mjini

rafiki wa elimu Juma richard okumu akiongoza kongamano la kujadili hali ya elimu wilaya ya musoma mjini





kongamano la kujadili hali ya elimu wilaya ya musoma mjini lililofanyika shule ya msingi Mwisenge limeibua changamoto nyingi zinazochangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya ya musoma mjini.

akibainisha changamoto hizo mwakilishi wa afisa elimu msingi ndg. Mroba  anasema siasa zinachangia kwa kiwango kikubwa kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani lakini pia anabainisha kuwa nidhamu, na wazazi kutokufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni pia inachangia,
lakini bado anakubaliana na hoja za washiriki kwamba serikali haiko makini katika kukabiliana na mabadiliko ya mitaala, na ucheleweshaji wa ruzuku za wanafunzi .

katika harakati za kupambana na changamoto ndugu Mroba kasema kuwa kwa sasa serikali imeongeza kasi ya ukaguzi katika shule nyingi za manispaa ambapo sasa zinafanyiwa ukaguzi mara mbili kwa mwezi,

licha ya baadhi ya washiriki kutofautiana na kauli ya ukaguzi wa shule mara mbili kwa mwezi afisa elimu huyo kasema kama bado ukaguzi haujafanyika katika shule zinazolalamikiwa basi atalifanyia kazi na nguvu ya ukaguzi itaonekana baada ya muda mfupi ujao.

Marafiki wa elimu musoma mjini ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hili wameahidi kufanya kazi na viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa kiserikali kuhakikisha elimu inainuka na kufikia kiwango bora.

Jumatano, 24 Aprili 2013

SERIKALI INAWEKEZA KWA ELIMU YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM ?

Rafiki wa elimu Juma Richard akiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Mwisenge

Tanzania ni moja ya nchi zenye watoto wenye mazingira magumu wenye ulemavu nk.
mara nyingi watoto wenye mahitaji maalum hawapewi kipaumbele cha kwanza mfano mzuri ni shule ya msingi Mwisenge.
 Shule hii ni shule yenye watoto wenye mahitaji maalum hivi karibuni wana blog hii walipokuwa wanahojiana na watoto hawa wanakiri wazi kuwa vifaa vya kujifunzia ni changamoto kubwa sana kwao.
shule hii ina watoto wenye mahitaji maalum kama wenye albinism na mara nyingi watoto wa jinsi hii wanahitaji mazingira ya kuwafanya waone kwa ukaribu hasa pale mwalimu anapoandika ubaoni

Lakini pia shule hii ina watoto wenye ulemavu wa macho nk.
wanafunzi wote hawa wanabainisha upungufu wa vifaa vya kujifunzia pia wanaomba mwenye mapenzi na shule hii achangie upatikanaji wa vifaa.

marafiki wa elimu musoma tunatoa wito kwa wote wenye mapenzi ya dhati na shule hii ya Mwisenge aliposoma Mwalimu Nyerere  wachangie  kwa hali na mali kuhakikisha wanafunzi hawa wanapata mahitaji haya

kila mtoto ana haki ya kupata elimu awe na mahitaji maalum au asiwe na mahitaji maalum na jamii pia tunayo nafasi ya kuwasaidia watoto wetu kuhakikisha wanapata elimu bora.
Marafiki wa elimu Tunawasihii sana wana Musoma na Tanzania nzima kusaidia shule ya Mwisenge .

Shirika la HAKI ELIMU limejitolea na kujenga maktaba ya kisasa  kabisa shuleni hapo sasa ni jukumu letu na sisi wana Musoma kuiboresha shule yetu ya Mwisenge.


NYUMBA YA MWALIMU SHULE YA MSINGI MWISENGE HAPA NDIPO ALIPOSOMA MWALIMU NYERERE


Picha inayoonekana hapo juu ni moja ya nyumba za walimu wa shule ya msingi mwisenge, hapa ndipo aliposoma Mwalimu Nyerere na hii ndiyo hali halisi ya nyumba za walimu zilivyo kwa sasa.

Lazima tutafakari na kujiuliza kwa pamoja kama tutaendelea kuisubiri serikali izikarabati au tutachukua jukumu sie wenyewe.
kwa namna moja au nyingine serikali imejitahidi sana kwa upande wa madarasa kwani kidogo madarasa ya shule hii ni ya kisasa na yanaridhisha .
lakini tunapozitazama nyumba za walimu wa shule hii inatia huruma sana kwanza ni nyumba za tope pili ni nyumba za muda mrefu sana na zimechakaa.

Hapa hakuna sababu tena ya  kuisubiri serikali ni lazima kamati ya shule ibuni mbinu mbadala ya kuisaidia shule yao.
lakini pia kuna viongozi wengi sana nchi hii  wamesoma shule ya msingi mwisenge na wana nyadhifa mbalimbali serikalini je wanaifikiriaje shule hii?

ni jukumu letu marafiki wa elimu wanajamii wazazi kamati za shule kuhakikisha tunafanikisha ujenzi wa nyumba za walimu wa shule ya msingi mwisenge na si mwisenge tu bali shule zote za wilaya ya musoma mjini
Marafiki wa elimu tunaanza kampeni sasa tutafahamishana muda si mrefu juu ya kampani yenyewe
kama umeguswa na taarifa hii tafadhali wasiliana na marafiki wa elimu musoma kwa e-mail jmrchrd@yahoo.com  tutakuunganisha na kamati ya shule ya msingi mwisenge tujitolee kusaidia shule hii kwani ni mfano wa taifa.

Alhamisi, 18 Aprili 2013

Je viboko vinaashiria upatikanaji wa elimu bora?

picha kwa hisani ya islam mposso
 leo tuvizungumzie viboko na nafasi yake katika kuinua kiwango cha nidhamu ya wanafunzi na elimu mara nyingi tumekuwa tukiwasikia wazazi wakilaumu juu ya adhabu ya viboko kufutwa mashuleni. Tumewasikia pia walimu wakilalama sana na kudai kurejeshwa kwa viboko kwa upande wa wanafunzi wanafurahi na kusema viboko havina nafasi  kwao.

Je viboko ni sawa

katika maandiko matakatifu viboko vinaruhusiwa kama njia ya kuleta maadili kwa  mtoto.
Lakini pia ni muhimu kuangalia na kutambua jinsi ya kukitumia kiboko kumfunza mlengwa, Tanzania tuliendelea kuamini na mpaka sasa tunaamini kuwa kiboko ni njia ya kumfunza mtoto hii ni sawa kabisa.

picha kwa hisani ya Islam Mposso
Je kiboko kinasaidia

tukirudi nyuma miaka ya 2000 kurudi nyuma viboko mashuleni vilikuwa ni sehemu ya maisha ya shule.
lakini pia ukiangalia mazingira ya shule ya kipindi kile na sasa kulikuwa na tofauti kubwa sana, zamani suala la utoro kwa wanafunzi kilikuwa ni kitu cha kawaida sana na hii ilisababishwa na viboko. Lakini kwa wale waliyovumilia viboko walipata faida ya kupata elimu bora.

Hivi karibuni serikali imesema inatarajia kurejesha  adhabu ya viboko mashuleni
hapa napata mushkeli kidogo na sababu kubwa ni hali halisi jinsi ilivyo baada ya kupunguzwa kwa adhabu ya viboko mashuleni suala la utoro lilipungua kwa kiwango kikubwa sana na baadhi ya wanafunzi wakaanza kuyaona mazingira ya shule kuwa ni rafiki kwao.
Binafsi tunaamini suala si viboko suala la msingi ni kuboresha mitaala ya shule zetu. walimu kupewa mafunzo ya mara kwa mara kwa sababu mafunzo ya walimu ni wajibu wao na ni lazima wayapate ili kuendana na mabadiliko ya mitaala.
lakini pia tunapozungumzia kuongeza adhabu ya viboko mashuleni ni lazima tuwe tayali kukabiliana na ongezeko la utoro, kwa maana kwamba shule hakutakuwa mahali rafiki tena kwa wanafunzi. Lakini twapaswa pia kukubali kuwa nidhamu za wanafunzi wetu zimeshuka sana lakini hii si kutokana na viboko hii inatokana na wana jamii wenyewe kuamua kuwalea watoto wao pekee yao tofauti na malezi ya zamani ambayo mtoto alikuwa ni mali ya jamii na kila mwana jamii alikuwa na jukumu la kumsimamia mtoto wa mwenzake.
Lakini suala la viboko moja kwa moja linaingia kiafya tunapaswa kukubali kwamba watoto wa zamani walikuwa tofauti na watoto wa sasa , mtoto wa zamani aliweza kumudu fimbo zaidi ya kumi na kuendelea na masomo darasani lakini mtoto wa sasa akichapwa fimbo tano tu basi utaanza kuona mabadiliko katika mwili wake hili la kiafya halina uchunguzi zaidi lakini tunaweza kuamini kwamba miili yetu ya sasa si kama ya zamani huenda ni kutokana na vyakula tulavyo au mabadiliko ya kimazingira
marafiki wa elimu tunaamini kiboko kina nafasi ila nafasi ya mwisho kabisa kwani adhabu mbadala zipo za kutosha tunahitaji mitaala bora elimu itakuwa bora na si viboko

Jumanne, 16 Aprili 2013

Boresha chekechea ni jukumu la kila mmoja wetu

wanafunzi wakiwa wamekaa chini

Suala la elimu ya awali ni suala nyeti linalotakiwa kutazamwa kwa macho mawili na jamii nzima Serikali na kila mdau wa elimu elimu. Elimu ya awali (chekechea) umsababisha mwanafunzi kuanza darasa la kwanza akiwa anazijua stadi za awali.
Mwanafunzi hawezi kuwa mzigo tena kwa mwalimu wa darasa la kwanza ikiwa atapitia elimu ya awali ( chekechea)
ni jukumu letu sote kuhakikisha elimu ya chekechea inakuwa bora  kwa watoto wote kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama uji, madawati, walimu bora pamoja na miundo mbinu rafiki ya kuwafanya wapende mazingira ya shule.

Kwa pamoja tuinue sauti za wanyonge

Jumatatu, 15 Aprili 2013

Dennis Ngadaya rafiki wa elimu mwanasiasa toka Nyampulukano Sengerema

Dennis Ngadaya rafiki wa elimu toka Sengerema
Huyu ni mmoja wa marafiki wa elimu wa siku nyingi alojikita katika siasa ni miongoni mwa wagombea udiwani kata ya NYAMPULUKANO  huko SENGEREMA  mara nyingi anaamini kuwa anauwezo wa kuitumikia jamii kwa upande wa siasa

harakati za marafiki wa elimu ni harakati za watu wote viongozi wa siasa wasio wanasiasa wanaojua kusoma na wasiojua kusoma walio ndani ya shule na wasio ndani ya shule kwa pamoja TUNAINUA SAUTI ZA WANYONGE

Jumamosi, 13 Aprili 2013

walimu na ualimu

tatizo la ualimu linachangiwa na walimu walioshidwa masomo yao elimu ya sekondari serikali lazima ilitizame na kuongeza thamani ya ualimu kuwa bora zaidi

Jumatatu, 8 Aprili 2013

Bi Neema Mafuru mratibu wa marafiki wa elimu musoma mjini


Neema Mafuru rafiki wa elimu musoma na mratibu wa shughuri za marafiki wa elimu

MARAFIKI WA ELIMU WAKIFANYA UTAMBULISHO KWENYE MKUTANO WA WANANCHI WA KATA YA KIGERA


Juma Richard na bi. Perus masokomya walipokaribishwa na uongozi wa erikali ya mtaa wa kigera kwenda kutambulisha rasmi harakati za marafiki wa elimu

harakati za marafiki wa elimu ni harakati za mashirika, taasisi na watu wanaojali wenye nia ya kuboresha elimu na demokrasia nchini Tanzania, kubadilishana mawazo na maoni yao katika masuala ya elimu na kuchukua hatua kwa ajili ya kuleta mabadiliko. harakati zitachangia kubadili mifumo ya shule ziweze kutoa elimu bora kwa kuzingatia misingi bora ya utawala na haki za binadamu

njoo tupaze sauti zetu pamoja

Ijumaa, 5 Aprili 2013

AZIMIO LA MUSOMA NA WAJIBU WA WALIMU



Tukiziendeleza hizo gharama tutapata taabu sana. watoto hawatasoma . itachukua muda mrefu sana  kabla watoto hawajasoma.....ukimaliza elimu yako ya sekondari  umemaliza elimu yako

Unakwenda ama kufanya kazi  au unakwenda katika chuo kinachofundisha kazi .......kuna kipindi katika  maisha yako cha kusoma halafu baadaye kuna kipindi cha kazi Haya mawazo si mazuri........''

mwl jk nyerere tarehe 8 februari 1975

Jumatano, 3 Aprili 2013

MWL J.K NYERERE TUJISAHIHISHE



makosa ni makosa na dhuluma ni dhuluma japo watendao makosa hayo au dhuluma ile ni wakubwa au ni wengi chama kinachopenda ukweli na haki  hakina budi kiwape wanachama wake uhuru na nafasi ya kusahihisha makosa  na kuondoa dhuluma. Wanachama hawana budi waone kuwa ni wajibu wao kuutumia uhuru huo, na nafasi hiyo.kwa sababu ya kuogopa kuchukiwa na kupoteza nafasi zao,wanafanya kosa kubwa la unafsi,ambalo ni adui wa haki  na ukweli


jk nyerere. -  tujisahihishe

may,1962.