Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatano, 17 Julai 2013

BAADHI YA SHULE MKOANI MARA ZAKOSA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO




Machungu ya matokeo mabovu ya kidato cha nne 2012 yanaanza kuonekana bayana. Kama ilivyotarajiwa, wanafunzi waliokuwa wamefaulu vizuri walikuwa wachache-kiasi kwamba wasingetosheleza mahitaji ya wanaotakiwa kujiunga na kidato cha 5. Mpaka sasa, shule binafsi saba za sekondari Mkoa wa Mara zimetangaza rasmi kuwa mwaka huu hazitaweza kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano. Shule hizo ni:

Makoko Semonary, Kowaki Girls, JK Bukanga, Isenye, Kibara, Ellys na Busegwe.

Hizi ni baadhi tu ya shule zilizotoa taarifa rasmi. Hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Baadhi ya shule zimefuta combination kadhaa-kutokana na kukosa wanafunzi. Hali hii iturejeshe kwenye hatua madhubuti za kuchukua ili wanafunzi walioko shuleni sasa wapate kilicho bora zaidi katika kujifunza na kujiandaa kwao. Wakiandaliwa vizuri, watafaulu vizuri-na miaka ijayo tukaondokana na tatizo hili la kukosa wanafunzi. Hata hivyo, ni heri kukosa wanafunzi wenye sifa kuliko kung'ang'ania kushusha alama za ufaulu ili tuwapate wengi wakajaze nafasi. Watanzania tuvumilie hali hii-ila tuendelee kushikamana kudai kilicho bora zaidi kwa watoto wetu na elimu yetu.