Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Ijumaa, 14 Juni 2013

Wananchi tuna wajibu wa kusimamia maendeleo ya ujenzi wa shule zetu


Leo harakati za marafiki wa elimu zinatufikisha katika shule ya msingi Kigera hapa tunafanikiwa kupata picha moja ya jengo la darasa lililojengwa muda mrefu na kuharibika.
kwa sasa linafanyiwa ukarabati ambao wazi unaonyesha ni ukarabati usiyofaa, jengo hili mwanzoni lilijengwa kwa matofari ya kuchoma baada ya kuanguka maeneo ya madirishani na milangoni, sasa pamejengwa na matofari ya cement tena kwa kiwango kidogo zaidi ya mwanzoni.

marafiki wa elimu tunawasihi wananchi kuuliza juu ya ujenzi wa madarasa na kusimamia viwango vya ujenzi kwani shule ni mali zao na zinajengwa kwa kodi zao