Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatano, 28 Mei 2014

tukio la kuvamiwa na kukatwa vidole mwenyekiti wa mtandao wa marafiki wa elimu musoma

napenda kuwashukuru marafiki wa elimu wa musoma mjini kwa kuonyesha moyo wa kuguswa na tukio lililonipata la kuvamiwa na kukatwa vidole  viwili na kukatwa kichwa kwa panga nawashukuru marafiki kwa mchango wao wa hali na mali kwa kuwa pamoja nami katika kipindi kigumu nilichokuwa nacho pia nawaomba wanaoamini kuwa tukio hili linaweza kunipata kutokana na harakati tunazoziendesha kama inavyosemwa na wengi naomba wasiamini hivyo, bali ni tukio la kivamizi la kawaida kabisa linaloweza mpata mtu yeyote. pia napenda kushukuru kituo cha radio victoria fm kwa kuwa pamoja nami, naibu katibu mkuu wa DP ndugu Abdu Mluya kwa kuwa pamoja nami na asasi zingine za musoma mjini kwa kuwa pamoja nami hakika Mungu ni mwema sasa ninaendelea vizuri kabisa.

picha ya kidole kilichokatwa
moja ya kidole cha rafiki wa elimu kilichokatwa