Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumamosi, 2 Machi 2013

                          

        HABARI NJEMA KWA MARAFIKI WA ELIMU

marafiki wa elimu musoma kupitia blog hii tunapenda kuwakaribisha marafiki wa elimu wote wa musoma mjini pamoja na wakazi wote wa musoma mjini kuitembelea maktaba ya jamii iliyopo katika kata ya Kigera  musoma mjini maktaba ufunguliwa siku za jumamosi na jumapili kwanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni 

 

maktaba ipo jirani na shule ya msingi kigera  imetazamana na shule ya  msingi kigera ,kusoma  vitabu ni bure na kila mmoja anakaribishwa kuitembelea na kujionea baadhi ya vitabu vilivyopo pia kujifunza mbinu mbalimbali kutoka kwa marafiki wa elimu musoma 

kwa mnaotaka kututembelea wasiliana nasi kwa namba

0755 65 00 75   au  0786 65 00 75

marafiki wa elimu tunaamini kuwa kila mtanzania ana haki ya kupata na kupokea habari karibu tuhabarishane.