Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumanne, 21 Mei 2013

James Mwita Mboyi katibu wa marafiki wa elimu musoma

James Mwita Mboyi katibu wa marafiki wa elimu musoma
James Mwita Mboyi ni katibu wa marafiki wa elimu wanakikundi wa sauti zetu club, ni mmoja wa wapigania haki za wanafunzi wa sekondari amekuwa akitetea wanafunzi kupata haki ya elimu bora bila ubaguzi tangu akiwa shuleni na hii ndiyo sababu kubwa iliyopelekea yeye kujiunga na harakati za marafiki wa elimu na kuwa mmoja wa wanakikundi wa SAUTI ZETU CLUB  mpaka sasa amekuwa mhamasishaji wa uundwaji wa CLUB za wanafunzi wa sekondari japo kuwa yuko nje ya shule.