Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumanne, 29 Desemba 2015

MATUKIO PICHA WAKATI SHULE YA MSINGI MWISENGE IKIPOKEA ZAWADI YA COMPUTER 5

wanafunzi wakisubiri kupokea computer toka shirika la EXPO

afisa elimu aliyekaa akijaribu computer hizo afisa huyu ni mtaalam wa tehama aliyesimama ni mkurugenzi wa shirika la EXPO TECNOLOGY bw.John

huyu ni kati ya mwanafunzi aliyefanya vizuri kwenye masomo ya tehema na kupelekea shule yake kushinda computer 5

afisa elimu akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa Haki Elimu na walimu wa Mwisenge

picha ya pamoja walimu pamoja na wanafunzi waliofaulu masomo ya tehama

Jumatatu, 28 Desemba 2015

Shule ya kidato I - IV ina wanafunzi 45 tu

 Shule ya Sekondari Panzua iliyoko kata ya Panzua Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ina jumla ya wanafunzi 45 wa kidato cha kwanza hadi cha nne.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka wilayani humo, Ofisa Kilimo wa kata hiyo, Muharami Makulika, alisema wanafunzi hao wanatoka katika vijiji saba vinavyoizunguka kata hiyo. Alivitaja vijiji hivyo kuwa ni Kibuyuni, Mkuruwili, Masanganya, Bupu kwa Wilaya ya Mkuranga na Kisarawe kijiji cha Malegele na Bwama.
 
Alisema takwimu za mwaka jana zinaonyesha shule hiyo ilikuwa na idadi ya wanafunzi 50 tu katika kidato cha kwanza hadi cha nne, jambo linalosababisha kufa kwa elimu katika kata hiyo, huku wengi wao ambao ni wa kike wakidaiwa kuolewa katika umri mdogo kutokana na wazazi na walezi kushindwa kuwasomesha.
 
Kwa mujibu wa Makulika, wazazi na walezi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wamechangia kuhalalisha ndoa za wanafunzi hao kwa kisingizio cha kipato kidogo kila mwaka, wakati baadhi yao kutokuwa na mwamko kuhusu elimu kwa mtoto wa kike itakayomkomboa katika mnyororo wa umaskini kwa siku za baadaye.
 
Alisema wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, wamegeuka washawishi wakubwa kwa wanafunzi hao kufanya vibaya katika masomo yao ya kuhitimu darasa la saba kwa dhamira ya kufeli ili  wawaozeshe.
“Ni vigumu kutatua changamoto hii, labda ziingilie sekta binafsi kama taasisi inayopambana na masuala ya ndoa za utotoni kama Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania (Tamwa).
 
Ofisa kijiji wa kitongoji cha Kibuyuni katika kata hiyo, Idd Ummagala, alisema takwimu za mwaka jana zinaonyesha idadi ya  wanafunzi katika shule hiyo walikuwa 54 na wengi wao hawakuhitimu masomo yao kutokana na ndoa za utotoni.
 
Alisema takwimu hizo katika kipindi cha masomo cha mwaka huu, ni chini ya mwaka jana kutokana na sababu mbalimbali zikiwamo za ndoa za utotoni, hali duni ya wazazi na walezi. Kwa mujibu wa Ummagala, mkakati wa serikali kwa 2016, ni kuiboresha shule hiyo ili iwe ya bweni kwa lengo la kudhibiti wimbi la wanafunzi hao hususan wa kike wanaoangukia ndoa za utotoni.
 
 Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Sharifa Abdallah, alisema idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo, wanatoka katika familia duni ambapo wazazi ama walezi wanaishi kwa kutegemea kilimo ambacho hawawezi kukihudumia. Alisema wanakijiji wengi wa kata hiyo, wanategemea fedha za kujikimu kupitia kilimo cha matunda, maharage na mahindi, wakati wanakabiliwa na idadi kubwa ya watoto katika familia, jambo linalochangia wengi wao kukatishwa masomo kutokana na rasilimali fedha.
 
“Pamoja na changamoto hiyo, lakini bado wanaume wengi hawana mwamko kuhusu elimu ya mtoto wa kike, badala yake wanaendekeza mila potofu za ndoa za utotoni huku wengine wakiona ufahari kuozesha mtoto katika umri chini ya miaka 18.
 
Takwimu hizo ni miongoni mwa shule chache za kata zilizoko vijijini zinazokabiliwa na idadi hiyo ndogo ya wanafunzi, lakini bado serikali imeshindwa kutoa adhabu au kuweka sheria inayosimamia haki zao  kuhakikisha watoto wanapata elimu bora kwa maisha yao ya sasa na baadaye.
 
chanzo. ippmedia.com
 

Alhamisi, 17 Desemba 2015

ELIMU BURE INAWEZEKANA


Rais John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa Elimu bure kwa wanafunzi wa chekechea hadi kidato cha nne Inawezekana na hakuna ubabaishaji katika hilo.
Rais amesema hakuna tatizo la fedha kwa ajili ya Elimu bure kutokana na serikali kuvuna kiasi kikubwa cha fedha kupitia TRA ambapo amempongeza kaimu Mkurugenzi wa TRA Bw. Philip Mpango kwa kukusanya zaidi ya sh. 1.3 trillion.
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Magufuli amesema fedha hizo zitapelekwa moja kwa moja kwenye account za shule husika na Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri watapelekewa taarifa tu.
Aidha Mh. Rais ameonya wakuu wa shule na walimu wakuu watakaotumia vibaya fedha hizo watakiona. Katika hili tunapongeza Rais na kuwataka wananchi watoe ushirikiano kwa wakuu wa shule na walimu wakuu katika kuhakikisha Elimu inayotolewa itakuwa na tija kwa vijana wetu.
Ni ukweli usiopingika kuwa nia ya Serikali ni kuleta mabadiliko chanya kwa watanzania lakini bila ushirikiano wa watanzania wote nia hii ya Serikali haitafanikiwa.

imeandikwa na Davis Makundi rafiki wa elimu toka Dodoma

Jumatatu, 14 Desemba 2015

Jumatatu, 17 Agosti 2015

RAFIKI WA ELIMU OMARI MUSA MAKANYA AINGIA KWENYE ULINGO WA SIASA

rafiki wa elimu Omari Makanya mgombea udiwani kupitia ACT
Wakati taifa likiwa kwenye matatizo na changamoto kubwa katika sekta ya elimu, na tukiwa tuko kwenye wakati wa uchaguzi mkuu na kupokea ahadi nyingi kutoka kwa watangaza nia mbalimbali lakini asilimia kubwa ya watia nia awaonyeshi moja kwa moja kutatua changamoto za elimu nchini.

leo tunakutana na mtangaza nia nafasi ya udiwani Kata ya Mugango wilaya ya Musoma vijijini rafiki wa elimu bwana Omary Mussa Makanya. huyu ni mdau wa elimu anaechukizwa na changamoto zinazokabiri elimu nchini kutokana na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuboresha elimu ameamua kujitosa rasmi kwenye ulingo wa siasa kwa lengo la kuwasaidia wakazi wa eneo la mugango

mdau huyu wa elimu amekuwa msitari mbele kutatua changamoto za wanafunzi na walimu hasa kuhakikisha tunaondoa dhana ya viongozi kutowajibika kwa wananchi wao.
pia amekuwa mhamasishaji wa michango mbalimbali kwa kushirikiana na wazazi kutatua changamoto za shule ,

Marafiki wa elimu Musoma tunamuombea rafiki mwenzetu bw. Omari Mussa Makanya aweze kufanikiwa kutimiza ndoto yake ya kukomboa watoto wa kitanzania kupata elimu bora

Jumanne, 12 Mei 2015

Geita walimu hawana meza wala viti

Geita. Walimu wa Shule ya Msingi Mwatulole mkoani Geita, hawana meza wala viti hali inayowalazimu kukalia madaftari ya wanafunzi kwa kuyatandika kwenye magogo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi baada ya kukutwa wamekalia madaftari, walimu hao walisema ukosefu wa samani shuleni hapo unawaathiri katika ufundishaji.
“Wakati mwingine tunasahihisha madaftari, huku tumesimama,” alisema Mwalimu Mathias Matiginya na kuongeza:
“Unakuta mwalimu ana vipindi vinne kwa siku, lakini anaishia kufundisha viwili kutokana na kusimama muda mrefu, anachoka haraka.”
Pia, alisema shule hiyo ina walimu wengi na haina ofisi, viti wala meza, hivyo walimu wanatumia darasa kama ofisi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Catherine Mgisu alisema suala hilo limefikishwa kwa uongozi wa halmashauri na kamati ya shule.
Alisema kamati hiyo inafanya jitihada za kuhamasisha wazazi kusaidia maendeleo ya shule ikiwamo upatikanaji wa viti na meza za walimu.
“Hii shule ina changamoto nyingi siyo ukosefu wa vitu hivyo tu, bali ina wanafunzi wengi, uhaba wa madarasa na madawati pamoja na utoro wa wanafunzi,” alisema Mwalimu Mgisu.
Katika hatua nyingine; Mwalimu wa Taaluma, Salma Rajab alisema anakerwa na wingi wa wanafunzi.
Alisema kutokana na hali hiyo  kipindi cha mitihani mbanano huwa mkubwa hali inayowanyima fursa ya kusimamia vizuri.
“Walimu tunapata shida hasa wanafunzi wanapofanya mitihani, tunashindwa kupata uhalisia wa matokeo yao. Huwa hatulitawali darasa kutokana na msongamano, hivyo tunakaa nje,” alisema Mwalimu Rajab. Mwalimu Debora Lucas alisema darasa moja linachukua zaidi ya wanafunzi 3,000.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Geita, Magarita Nakainga alisema alipokea taarifa ya changamoto hizo na kwamba suala hilo linashughulikiwa ili kuhakikisha shule inakuwa na hali nzuri.


“Ni aibu kwa shule za mjini kuwa hivyo, hivi sasa tunaweka mikakati ya kukarabati na kuboresha miundombinu tunakusanya mapato ili tuanze kazi hiyo,”

chanzo mwananchi

alisema.

matukio ya picha mkutano wa mtandao wa marafiki wa elimu Musoma







Ijumaa, 1 Mei 2015

Marafiki wa elimu Kahama wajengewa uwezo

Marafiki wa elimu Kahama ni moja kati ya wilaya zilizoanza  kuinua upya ari ya marafiki wawilaya hiyo kujali elimu ,hivi karinubuni shirika la HAKI ELIMU liliandaa mpango maalumwa kuhamasisha harakati katika wilaya hiyo jambo lililoonyesha kupokelewa vyema na marafiki wa elimu wa wilaya hiyo na kupelekea ongezeko la marafiki wapya wa elimu.   picha zinaonyesha baadhi ya  matukio katika kongamano hilo

Joyce Mkina akizungumza na marafiki wa elimu Kahama


M

Jumamosi, 28 Machi 2015

WAZAZI WAGOMA KUCHANGIA CHAKULA CHA WANAFUNZI

Kutoka kijiji cha Bisumwa wilaya mpya ya Butiama  wazazi wamegomea uongozi wa shule yao pamoja na kamati juu ya suala la kuchangia chakula kwa wanafunzi shuleni kama agizo la serikali linavyosema wanafunzi wanapaswa kula shuleni ili kuongeza ari ya kujifunza na kupunguza utoro.

shule iliwaomba wazazi hao kichangia kiasi cha debe  moja la mahindi na maharage kilo4 kila mwezi kwa ajili ya chakula cha wanafunzi awali katikabkikao hicho cha kamati ya shule na wazazi kamati iliwaambia wazazi kuwa kila mzazi atatakiwa kuchangia mchango huo kwa kila mtoto iwapo mzazi una watoto 4 basi utatakiwa  kuchangia mahindi debe 4 na maharage  kilo 16

baada ya wananchi kusikiliza maelezo hayo toka kwa uongozi wa shule walitoa kauli ya pamoja kwamba hawako tayari kuchangia kiasi hicho kutokana na hali ya maisha ya sasa na pia hawako tayari kuchangia hata debe moja kwa watoto 4 hivyo shule iendelee na utaratibu wa kutawanyisha watoto mapema ili waende  majumbani mwao kula kisha warudi shule  kama ilivyokuwa ikifanyika awali


suala la wazazi kuchangia chakula kwa  ajili ya wanafunzi limeonekana kuwa tatizo sana hasa katika mikoa ya kanda ya ziwa na huenda likashindikana kabisa serikali inapaswa kuangalia njia mbadala ya kutekeleza mpango huu

Jumanne, 24 Februari 2015

mbunge Nyerere agawa computer na projector kwa awamu ya pili kwa shule za sec musoma mjiji

kwa awamu ya pili sasa mbunge wa musoma mjini mh. Vincent Nyerere anakusudia kugawa computer kumi na tano  baada ya awamu ya kwanza kugawa computer kumi na tano

akizungumza na wakazi wa musoma mjini katika viwanja vya shule ya msingi mkendo mbunge huyo alielezea mafanikio mbalimbali aliyoyafikia katika sekta ya elimu. mpaka sasa ni

kujenga maabara ya kisasa katika shule ya sekondari bweri maarufu kwa jina la bweri makatani lengo likiwa ni kuwaanda wanafunzi kupenda sayansi
na kuwaahidi wananchi wa musoma mjini kuwa azma yake ya kuibadili shule ya msingi mkendo kuwa high school iko pale pale japo ni mchakato unaochukua muda mrefu kidogo.

mbunge nyerere aliefika uwanjani hapo na baadhi ya computer hizo pamoja na projector amesema kitu kikubwa anachoweza kuwalipa watoto wa
maskini wapiga kura wake ni elimu bora pekee hivyo atajitahidi kuhakikisha anakuza kiwango na ubora wa elimu musoma mjini

mbunge nyerere aliahidi kuzifikishia shule zote umeme ili iwe rahisi watoto kujifunza ambapo mpaka sasa kuna miradi kadhaa ya kupeleka umeme mashuleni imefikia  hatua za mwisho mwandishi wa blog hii alifanikiwa kuitembelea shule ya sekondari nyasho iliyokuwa mbali sana na miundombinu ya umeme na kukuta nguzo zikiwa tayari zimesimamishwa na nyaya zikigoja kuwashwa umeme tu.


mauaji ya albino

makamu meya wa manspaa ya musoma pia alizungumzia  juu ya mafanikio waliyoyafikia mpaka saa juu ya  kuzuia na kulinda watoto albino ni pamoja na kuhakikisha shule ya msingi mwisenge mpaka sasa imepata uzio kwa ajili ya kulinda watoto hao.
na pia licha ya shule ya mwisenge kupata uzio maabara ya kisasa imejengwa na inasubiri kuzinduliwa tu.

mbunge nyerere ni moja ya wabunge wanaoonyesha nia na uchungu wa kujuza kiwango cha elimu nchini.
Ongeza kich




Jumatatu, 2 Februari 2015

kamati ya shule ya nyang'omboli yajipanga kunusuru wanafunzi kukaa sakafuni

kamati mpya ya shule ya msingi nyang'omboli musoma mjini kwa kushirikiana  na wazazi wameazimia kwa pamoja kutengeneza madawati mapya kwa ajiri ya kuwasaidia wanafunzi kuindokana na adha ya kuketi sakafuni kama wanavyoonekana pichani