Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Alhamisi, 17 Desemba 2015

ELIMU BURE INAWEZEKANA


Rais John Pombe Magufuli amewahakikishia watanzania kuwa Elimu bure kwa wanafunzi wa chekechea hadi kidato cha nne Inawezekana na hakuna ubabaishaji katika hilo.
Rais amesema hakuna tatizo la fedha kwa ajili ya Elimu bure kutokana na serikali kuvuna kiasi kikubwa cha fedha kupitia TRA ambapo amempongeza kaimu Mkurugenzi wa TRA Bw. Philip Mpango kwa kukusanya zaidi ya sh. 1.3 trillion.
RAIS JOHN POMBE MAGUFULI
Magufuli amesema fedha hizo zitapelekwa moja kwa moja kwenye account za shule husika na Ofisi za Mkuu wa Mkoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri watapelekewa taarifa tu.
Aidha Mh. Rais ameonya wakuu wa shule na walimu wakuu watakaotumia vibaya fedha hizo watakiona. Katika hili tunapongeza Rais na kuwataka wananchi watoe ushirikiano kwa wakuu wa shule na walimu wakuu katika kuhakikisha Elimu inayotolewa itakuwa na tija kwa vijana wetu.
Ni ukweli usiopingika kuwa nia ya Serikali ni kuleta mabadiliko chanya kwa watanzania lakini bila ushirikiano wa watanzania wote nia hii ya Serikali haitafanikiwa.

imeandikwa na Davis Makundi rafiki wa elimu toka Dodoma