Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Ijumaa, 22 Machi 2013



Mara nyingi tumeliona suala la upatikanaji wa elimu bora kama ni suala la serikali peke yake na kusahau kuwa jamii nzima inajukumu la kusimamia elimu

tunajiuliza maswali mengi sana juu ya kuzidi kudolola kwa elimu nchini mara nyingi tumemtafuta mchawi bila kumpata na hata tunasahau kuwa wachawi wa tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu ni sisi wenyewe

hapo ulipo kama wewe ni mzazi ,mlezi ,au mwanajamii jiulize umewahi kufanya nini kusaidia sekta ya elimu umewahi kufuatilia na kutaka kujua juu ya elimu inayotolewa shuleni?

Juma richard ni mjumbe wakamati ya shule ya msingi hapa musoma anasema tangu amekuwa mjumbe wa kamati ya shule hajawahi kukutana na mzazi au mwanajamii aliyewahi kumuuliza juu ya mapato na matumizi ya shule pia hajawahi kuulizwa juu ya ruzuku za wanafunzi na hata ruzuku za maendeleo.

halii hii  inamaanisha kwamba wengi wa wanajamii hawana muda wa kukaa na kutafakari juu ya elimu na mwisho wa siku huachia serikali peke yao na walimu ndiyo watoe elimu bora lakini pale tunapogundua kwamba tumefanya vibaya katika mitihani hapo utawasikia wazazi wengi wakilalamika kutaka kujua ni kwa nini.

wazazi wengi hawana muda wa kukagua madaftari ya watoto wao hawana muda wa kuzungumza na familia zao.  walimu pia wanakatishwa tamaa na mazingira magumu ya kufundishia hivyo upelekea kutoa elimu isiyo bora na kuwaaminisha watoto kuwa elimu bora upatikana kwa masomo ya ziada yaani tution.

Kwa upande wake serikali inachukulia kushuka kwa elimu kama kitu cha kawaida na kusahau kuwa kuna wakati ruzuku za wanafunzi ucheleweshwa shule makusudi pia upelekwa zikiwa pungufu serikali usahau kwamba walimu wanaishi katika mazingira magumu sana ,shule hazina nyezo za kujifunzia na kufundishia

bajeti ya wizara ya elimu pia ni ndogo haikizi mahitaji bajeti kubwa uelekezwa kwenye utawala yaani posho za semina na kukarimu wageni.

lakini suala la kubadilika kwa mitaala limekuwa sugu na upelekea walimu kutokuielewa vizuri kwani hawana mafunzo juu ya mibadiliko hiyo.

kila mmoja ubaki akivutia kamba upande wake tujiulize ni wapi tumekosea tujisahihishe tufanye vema .