Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatano, 27 Februari 2013

mwalimu Byabato rafiki wa elumu toka Serengeti

Rafiki wa elimu mwalimu Byabato anapatikana wilaya ya Serengeti hapa anazungumza na marafiki wenzake wa elimu  akisisitiza juu ya mbinu za kuboresha elimu pamoja na kuelezea mafaniko ya marafiki wa elimu wa wilaya ya mugumu serengeti

marafiki hawa wa serengeti ni moja ya marafiki wa elimu waliyofanikiwa sana katika harakati za kuboresha elimu 

Jumanne, 26 Februari 2013

Choo cha shule ya msingi Kigera A na B

Hiki ndicho choo cha shule ya msingi kigera chenye jumla ya matundu 6 pamoja na choo cha walimu shule hii ina wanafunzi zaidi ya 500 ambaye imegawanywa kigera A na B kwa hali hii bado haiendani na sera ya elimu 

ni wakati wa wazazi na wanajamii kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanaendeleza miundo mbinu ya shule zao na si kuachia serikali pekee

Jumatatu, 25 Februari 2013

HAWA NDIYO WALIYOFELI MATOKEO YAO JE UNADHANI YUKO SAHIHI KWA HILI ALILOLIFANYA


Hii  ndiyo tanzania tuliyoambiwa yenye neema

Kutokana na wanafunzi wengi kutokufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha nne mwaka huu.

baadhi ya mambo yaliyochangia anguko la wanafunzi wengi katika baadhi za shule za msingi za musoma mjini zinachangiwa na wanafunzi wenyewe

baadhi ya wanafunzi wa shule za  Nyasho sekondary, Buhare sekondary,Kiara sekondary, Mwisenge sekondary pamoja na victoria sekondary 

wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu kwa walimu wao ,uvutaji bangi na kucheza kamari nyakati za masomo hali hii imeanza kujitokeza katika shule hizi tangu mwaka 2011

na kupelekea baadhi ya wanafunzi ufaulu wao kuanza kushuka jeshi la polisi lilijitahidi kadri ya uwezo wake kuzuia hali hii ambayo ilianza kukomaa na kupelekea wanafunzi wengi wa shule hizo kujiunga na makundi ya kiharifu yaliyokuwa yakijulikana kama mbio za vijiti. mdomo wa furu ,jamaika mocas pamoja na mengineo.

kutokana na jitihada za polisi zilifanikiwa kuzuia kwa kiwango walichoweza lakini kwa baadhi ya wananchi wameendelea kusema kwamba makundi hayo ya wanafunzi bado yamejikita mizizi katika uvutaji bangi na uporaji

kutokana na hali hii marafiki wa elimu musoma tunashauri serikali ya tanzania kusaidia shule za kata kujenga nidhamu ya wanafunzi pia serikali ijikite katika kuboresha changamoto za elimu zinazokabili taifa 

wapo walioshindwa kutokana na utovu wa nidhamu kama hawa tuliyowasemea lakini asilimia kubwa  walioshindwa mitihani ni kutokana na serikali kutoithamini sekta ya elimu


Juma Richard Okumu mmoja wa marafiki wa elimu wanaopatikana musoma mjini  no. 0755 650 075   au  0786 650 075

ELISANTE KITULO TOKA HAKI ELIMU AKIZUNGUMZA NA MARAFIKI WA ELIMU MUSOMA (hawaonekani pichani)

Marafiki wa elimu  musoma  wakitafakari  kwa pamoja mbinu  za  kuboresha  elimu

PIUS MAKOMELELO TOKA HAKI ELIMU AKITETA NA MARAFIKI WA ELIMU MUSOMA

BAADHI YA MARAFIKI WA ELIMU MUSOMA WAKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU MUSOMA NI HARAKATI HURU ZENYE LENGO LA KULETA USAWA , UBORA NA UPATIKANAJI WA ELIMU BORA KATIKA MKOA WA MARA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUNAENDELEZA HARAKATI ZETU KATIKA MAENEO MBALIMBALI HAPA MUSOMA MJINI

KILA MMOJA WETU ANAWEZA KUWA RAFIKI WA ELIMU NA KUJUMUIKA NA MARAFIKI WENGINE NCHINI POTE

TUTAENDELEA KUFAHAMISHANA JUU YA HARAKATI ZETU NA NAMNA YA KUTUPATA KARIBUNI SANA KATIKA BLOG HII MPYA KABISA

KARIBUNI SANA KWENYE BROG HII MPYA YA MARAFIKI WA ELIMU MUSOMA