Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Ijumaa, 24 Mei 2013

ELIMU KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM MUSOMA JUHUDI ZA ZIADA ZINATAKIWA

rafiki wa elimu Juma Richard akicheza bao na wanafunzi wenye mahitaji maalum wa shule ya msingi Mwisenge

Elimu ya wanafunzi wenye mahitaji maalum Manispaa ya Musoma bado ni changamoto kubwa sana. kutokana na matatizo mengi ambayo yanawakabili watoto wenye mahitaji maalum katika wilaya ya Musoma Mjini.
hali halisi inaonyesha wanafunzi wenye mahitaji maalum bado hawalidhiki na upatikanaji wa elimu yao.
katika wilaya ya Musoma Mjini zipo shule 3 zinazopokea watoto wenye mahitaji maalum ambazo ni Mwisenge, Nyarigamba na Mwembeni B

shule ya msingi Mwisenge upokea watoto wenye mahitaji maalum na wasio na mahitaji maalum,lakini wenye mahitaji maalum wapo wasioona, wenye albiniziam ambao nao uoni wao ni mdogo pia kuna wasiosikia na wenye ulemavu wa viungo kidogo sana.
wakati tukifanya mazungumzo na watoto hao hasa wasioona wamedai kutokuwepo kwa vitabu vya kutosha kwa ajili yao japo kuna mazingira rafiki kwa ajili yao lakini pia changamoto nyingine inayowakabili kwa ujumla ni kutokuwepo walimu wa kutosha wa kufundisha masomo ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

shule ya msingi Mwembeni B pia inapokea wanafunzi wenye mtindio wa ubongo wasiosikia na wenye ulemavu wa viungo tatizo kubwa linaloikabili shule hii iliyoko katikati ya mji ni kuwa na miundombinu mibovu hakuna choo za kisasa kama ilivyo kwa shule ya msingi Mwisenge  lakini pia kuna tatizo la walimu wa kutosha kufundisha wanafunzi wenye mtindio wa ubongo na kupelekea baadhi yao kukaa shule kwa muda mrefu bila  kuelewa wanayojifunza.

Shule ya Nyarigamba iko nje ya mji lakini pia inazo changamoto zilezile ambazo zinakabili shule ya Mwisenge na Mwembeni ,
marafiki wa elimu wamekuwa wakifuatilia mara nyingi kutaka kujua ni hatua zipi zinachukuliwa kuboresha shule hizi bila kupata majibu ya kuridhisha.
lakini pia marafiki walitaka kujua kutoka ofisi ya afisa elimu sekondari kuwa kuna shule ngapi za sekondari kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum na kubaini kwamba katika manispaa nzima kulikuwa na shule moja tu iliyokuwa imetengwa kupokea wanafunzi wa aina hiyo lakini hakuna hata mwanafunzi mmoja mwenye mahitaji maalum anaesoma katika shule hiyo ya Musoma Tech.
na badala yake matumizi ya shule hiyo yamekuwa ya kawaida kwa wanafunzi wa kawaida kabisa licha ya kwamba hawa wanafunzi wenye mahitaji maalum wanapomaliza masomo yao na kuchaguliwa hawana shule yao maalum wanayopelekwa hivyo huishia kusoma shule mchanganyiko na wanafunzi wa kawaida