Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumanne, 4 Juni 2013

Marafiki wa elimu na changamoto

marafiki wa elimu wawezeshaji wakimsikiliza dada Lilyan Omary toka shirika la Haki elimu

Mara kwa mara tumezungumza tumeandika pia kuhusu shughuli za marafiki wa elimu Musoma mjini na Tanzania kwa ujumla marafiki wa elimu ni wanajamii wa kawaida kabisa wanaojitolea kuleta mabadiliko na kuhakikisha kunakuwepo na elimu bora nchini.
harakati za marafiki wa elimu musoma wanaunda kikundi chao kinachofahamika kwa jina la (SAUTI ZETU CLUB) kikundi hiki mpaka sana kinao wanakikundi zaidi ya 39 kiko imara na kimekuwa kikiendesha mijadala ya wazi kimeshirikishwa mara kadhaa katika mikutano ya ngazi za kata kuelezea juu ya elimu, na mbinu za kufanikisha elimu bora.
marafiki wa elimu musoma sasa wanajipanga kuanza kuhamasisha jamii za vijijini  kujitolea kuboresha elimu na kuelezea juu ya umuhimu wa elimu bora kwa wakazi wa vijijini tumeanza na tunaamini tutafanikiwa kama kuna ushauri au maoni tafadhari wasiliana nasi kwa nambari 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75  au e-mail     jmrchrd@yahoo.com