Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatatu, 29 Aprili 2013

Kongamano la kujadili hali ya elimu musoma mjini

rafiki wa elimu Juma richard okumu akiongoza kongamano la kujadili hali ya elimu wilaya ya musoma mjini





kongamano la kujadili hali ya elimu wilaya ya musoma mjini lililofanyika shule ya msingi Mwisenge limeibua changamoto nyingi zinazochangia kushuka kwa kiwango cha elimu katika wilaya ya musoma mjini.

akibainisha changamoto hizo mwakilishi wa afisa elimu msingi ndg. Mroba  anasema siasa zinachangia kwa kiwango kikubwa kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani lakini pia anabainisha kuwa nidhamu, na wazazi kutokufuatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni pia inachangia,
lakini bado anakubaliana na hoja za washiriki kwamba serikali haiko makini katika kukabiliana na mabadiliko ya mitaala, na ucheleweshaji wa ruzuku za wanafunzi .

katika harakati za kupambana na changamoto ndugu Mroba kasema kuwa kwa sasa serikali imeongeza kasi ya ukaguzi katika shule nyingi za manispaa ambapo sasa zinafanyiwa ukaguzi mara mbili kwa mwezi,

licha ya baadhi ya washiriki kutofautiana na kauli ya ukaguzi wa shule mara mbili kwa mwezi afisa elimu huyo kasema kama bado ukaguzi haujafanyika katika shule zinazolalamikiwa basi atalifanyia kazi na nguvu ya ukaguzi itaonekana baada ya muda mfupi ujao.

Marafiki wa elimu musoma mjini ambao ndiyo waandaaji wa kongamano hili wameahidi kufanya kazi na viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa kiserikali kuhakikisha elimu inainuka na kufikia kiwango bora.