Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Alhamisi, 19 Desemba 2013

Waziri wa elimu adai yeye si waziri mzigo




Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, ameamua kuvunja ukimya na kueleza kuwa yeye si waziri mzigo na wala hashtushwi na jina hilo kwani hawezi kuzuia maamuzi ya watu kumuita hivyo.

Dk. Kawambwa amesema yeye ni mchapakazi na tayari juhudi za kiutendaji katika wizara anayoiongoza zimeanza kuonekana.

Amesema kuwa suala la kuitwa waziri mzigo linatokana na yeye kuwa kioo na dira ya wenzake  katika wizara hiyo na hivyo majina kama hayo hayawezi kukwepeka na wala kuathiri utendaji wake na kujivunia kuwa yeye ni mmoja wa wasimamizi wa upatikanaji bora wa elimu hapa nchini.

 Waziri Kawamba aliamua kuvunja ukimya huo wakati akifungua kikao cha kazi cha maofisa elimu wa mikoa na halmashauri kinachojadili maendeleo ya elimu ya msingi hapa nchini pamoja na kufanya udahili wa pamoja katika matokeo ya darasa la saba.

"Kuna mtikisiko mkubwa katika wizara yetu na mengi yanasemwa wote mnasikia na Watanzania wanafahamu. Tupo katika safari nzito lakini ili gari liondoke, lazima kwanza litikisike, hivyo msiwe na wasiwasi tutafika salama tu," alisema Dk. Kawambwa.

Alisema anashangazwa kuitwa mzigo kwani kutokana na uwajibikaji wake katika wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa elimu, wamepata mafanikio makubwa hususani katika kuinua kiwango cha ufaulu wa wanafunzi mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2013.

 Alisema kutokana na jitihada zake na kushirikiana na watendaji na wadau mbalimbali, kiwango cha ufaulu mwaka 2013 kwa wahitimu wa elimu hiyo ya msingi

kimeongezeka kutoka asilimia 31 mwaka uliopita hadi kufikia asilimia 50.61 mwaka 2013 ambao ufaulu huo ni ongezeko la asilimia 19.89 ukilinganishwa na mwaka jana.

Waziri Kawambwa alisema jumla ya watahiniwa 844,938 walifanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi na kati yao 427,606 sawa na asilimia 50.61, wamefaulu kwa zaidi ya alama 100 kati ya 250 matokeo ambayo aliyaita ni mazuri.

Alisema kuwa kati ya watahiniwa hao waliofaulu, wasichana ni 208,227 sawa na asilimia 46.68 na wavulana ni 219,379 sawa na asilimia 55.01kitu ambacho kimeinua kiwango cha ufaulu.

Hata hivyo, alisema ufaulu huo bado haujafikiwa lengo la mpango wa Matokeo Makubwa Sasa la kufikia asilimia 60, lakini kutokana na jitihada na kipindi kifupi tangu mpango huo utangazwe, ni wazi kuwa kazi imefanyika na kustahili kupongezwa.

Jumatano, 18 Desemba 2013

Serikali yagomea CWT kuhusu kima cha chini cha mishahara


 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa


Serikali  imesema haiwezi kuongeza vianzio vya mishahara kwa asilimia 53 kama Chama cha Walimu Nchini (CWT) kinavyotaka kwa kuwa fedha hizo ni zaidi ya asilimia 50 ya mapato ya nchi.

Kauli hiyo ilitolewa jana Bungeni na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alipokuwa akijibu maswali ya nyongeza ya Mbunge wa Viti Maalum, Cecilia Pareso (Chadema).

Pareso alitaka kujua ni lini serikali italipa malimbikizo ya walimu yakiwamo yanayotokana na kupandishwa madaraja.

Pia alihoji serikali inapata kigugumizi gani kulipa nyongeza ya asilimia 50 ya mishahara kwa kadiri walivyokubaliana na CWT.

Katika swali la msingi, Mbunge huyo alitaka kufahamu mpaka sasa serikali imeshughulikiaje madai ya stahili za walimu hapa nchini.

Akijibu maswali hayo,  Dk. Kawambwa alisema serikali imejipanga kuondokana na madeni ya walimu.

Alisema zoezi linaloendelea hivi sasa ni uhakiki wa madeni ya serikali kwa ushiriki kikamilifu na CWT.

Hata hivyo, alisema madai ambayo CWT yaliyotaka nyongeza ya asilimia 53 kwa vianzia vya mishahara yanazidi bajeti ya mishahara yote ya watumishi wa serikali nchin.Kwa msingi huo alisema hakukuwa na namna ambayo serikali ingelipa.

Hata hivyo, alisema serikali imekuwa ikiongeza mishahara kwa walimu ambapo mpaka sasa imeshaongeza asilimia 30.9.

Aidha, alisema serikali na CWT wanaendelea na majadiliano kuhusiana na madai hayo ya walimu na tayari vikao vinane vimefanyika.

“Katika vikao hivyo, serikali iliahidi kutoa nyongeza ya wastani wa asilimia 14.62 ya vianzia vya mishahara ya walimu wakati CWT walishuka kutoka asilimia 100 hadi asilimia 53 ya nyongeza waliyokuwa wanadai,” alisema.

Chanzo Ippmedia.com

Alhamisi, 12 Desemba 2013

Wananchi wadai uwajibikaji mkubwa wa wabunge Wananchi wengi Tanzania Bara waunga mkono madai hayo na vifungu vingine muhimu katika rasimu ya katiba






Tarehe 4 Desemba 2013, Dar es Salaam: Zaidi ya theluthi moja (36%) ya Watanzania Bara wameshiriki
katika marekebisho ya katiba kupitia mikutano ya jamii, SMS, mahojiano, barua na barua pepe. Idadi
kubwa walishiriki kupitia mikutano ya jamii iliyoandaliwa na Tume ya Kurekebisha Katiba (CRC). Pia,
karibu nusu ya Watanzania Bara wanaweza kuelezea Katiba ni nini.
Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika utafiti uitwao: Kurasimu Sheria Mama ya Nchi: Tafakari ya
Wananchi wa Tanzania Bara kuhusu Rasimu ya Katiba. Msingi wa utafiti huu mfupi ni taarifa kutoka
Sauti za Wananchi, utafiti wenye uwakilishi kitaifa, uliotumia simu ya mkononi, ngazi ya kaya katika
Tanzania Bara.
Taarifa zinaonyesha viwango vya juu vya ufahamu wa Katiba na ushiriki katika mchakato wa mapitio. Pia,
karibu watu saba kati ya kumi (67%) ya Watanzania Bara wanafahamu kuwa rasimu ya Katiba
ilizinduliwa, ingawa chini ya robo (23%) walijua jinsi ya kupata nakala ya Rasimu ya Katiba.
Moja ya maeneo makuu ya mjadala ni hali Muungano kati ya Bara na Zanzibar. Juu ya mada hii, utafiti
umegundua kuwa maoni yamegawanyika, nusu (51%) wakikubali na nusu (48%) wakikataa kuanzishwa
kwa Serikali tatu. Hata hivyo, walipoulizwa zaidi, idadi ya waliounga mkono Serikali tatu kwa Watanzania
wa Bara, ililingana na waliounga mkono Serikali moja, wote ni 19%. Sauti za Wananchi pia iliweza
kulinganisha matokeo haya na ya utafiti uliofanywa na Afrobarometer katika nchi nzima (pamoja na
Zanzibar) mwaka 2012. Mwaka 2012 karibu nusu (47%) ya Watanzania Bara walikataa mabadiliko yo
yote katika masuala ya Muungano, hata hivyo katika mwezi wa Julai mwaka 2013, robo (26%) ya
Watanzania Bara walikataa mabadiliko. Kinyume chake, moja kati ya kumi (8%) waliunga mkono
kuongezeka kwa uhuru wa Zanzibar mwaka 2012 wakati theluthi mmoja ya watu waliunga mkono jambo
hili mwaka 2013. Utafiti wa Sauti za Wananchi unafanyika Tanzania Bara tu, kwa hiyo uchambuzi huu
hauhusishi tawimu toka Zanzibar.
Kumekuwa na vifungu kadhaa katika rasimu ya katiba ambavyo vimekuwa vikijadiliwa kwa mapana
katika vyombo vya habari. Wananchi kwa kiasi kikubwa walikubaliana na rasimu katika yote haya. Karibu
wote (91%) ya Watanzania Bara wanataka kuwa na uwezo wa kumwondoa Mbunge wao kwa kushindwa
utendaji, hiki ni kielelezo cha wazi cha kutaka uwajibikaji; na ni hali iliyofanya kifungu hiki kupendwa
zaidi katika rasimu. Maeneo mengine ndani ya rasimu yaliyopata uungwaji mkono mkubwa toka kwa
wananchi ni:
Mgombea urais lazima awe na umri zaidi ya miaka 40 (84% wanakubaliana)
Mawaziri na Manaibu wao wachaguliwe na Rais na kupitishwa na Bunge (77% wanakubaliana)
Bunge lazima liundwe na wajumbe 75, wawili kutoka kila mkoa wa Tanzania Bara, wawili kila
mkoa wa Zanzibari (76% wanakubaliana)
Spika na Naibu Spika, wanapaswa wasiwe viongozi wa vyama vya siasa kwa miaka mitano kabla
ya kugombea nafasi hii (72% wanakubaliana)
Mawaziri na Manaibu wao wanapaswa wasiwe madiwani, wabunge au wajumbe wa Baraza la
Wawakilishi (70% wanakubaliana)
Wabunge wanapaswa kuwa katika ofisi kwa miaka isiyozidi 15 (70% wanakubaliana)
Wagombea huru waweze kuwania nafasi ya Urais na Ubunge (67% wanakubaliana)
Kuwe na tume Huru ya Uchaguzi, iliyoteuliwa na Rais (65% wanakubaliana)
Sauti za Wananchi pia iliwauliza Watanzania Bara kama waliunga mkono rasimu ya katiba. Pamoja na
kuwepo makubaliano ya jumla katika masuala muhimu, wengi wao wangepigia kura rasimu ya sasa.
Pamoja na hayo, theluthi mbili (65%) wanaamini kwamba Uchaguzi Mkuu ujao utafanywa kwa kutumia
Katiba mpya.
Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema “Kimsingi, katiba inapaswa kuandikwa kutokana na maoni
na amali za wananchi. Utafiti wa Sauti za Wananchi ni moja ya nyenzo muhimu inayotumika kupata
maoni ya wananchi kwa njia madhubuti na ya kisayansi. Ni matumaini yetu wale waliopewa jukumu la
kuandaa rasimu ya katiba watayasikiliza kwa makini.”
---- Mwisho ----
Kwa maelezo zaidi:
Risha Chande
Meneja Mawasiliano, Twaweza
e: rchande@twaweza.org | t: (255) (0) 656 657 559
Maelezo kwa Wahariri
Taarifa hii na data zilizomo zinaweza kupatikana www.twaweza.org, au www.twaweza.org/sauti
Twaweza ni jitihada ya miaka kumi zinazowalenga wananchi juu ya mabadiliko mapana katika
Afrika Mashariki. Twaweza anaamini kwamba mabadiliko ya kudumu yanahitaji kuanzia ngazi za
chini kwenda juu, na inataka kujenga mazingira na kupanua fursa za njia ambazo mamilioni ya
watu wanaweza kupata taarifa na kufanya mabadiliko kutokea katika jamii zao moja kwa moja
na kwa kuiwajibisha Serikali.
Unaweza kufuatilia kazi za Twaweza kupitia:
Mtandao: www.twaweza.org Facebook: Twaweza Tanzania Twitter: @Twaweza_NiSisi

Jumatatu, 9 Desemba 2013

wahitimu mzumbe wahimizwa kutumia elimu walioipata tulitumikia taifa vema

Wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe mkoani Morogoro, wamehimizwa kutumia maarifa, elimu na stadi walizozipata chuoni hapo kuwa kichocheo cha maendeleo katika jamii inayowazunguka na ukuaji wa uchumi wa taifa kwa ujumla.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Profesa Joseph Kuzilwa, amesema kwa kuhitimu kwao, kunawaweka katika nafasi nzuri zaidi ya kutumikia taifa lao na jamii inayowazunguka.

Aliyasema hayo wakati wa mahafali ya 12 ya chuo hicho mjini hapa mwishoni mwa wiki.

Profesa Kuzilwa alisema wasomi hao sasa ni rasilimali watu inayotegemewa kuleta maendeleo ya nchi, hivyo akawaomba wakawe mfano bora kwa jamii inayowazunguka na kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanatimiza wajibu kwa taifa lao.

Jumla ya wahitimu 1,803 walitunukiwa vyeti mbalimbali, kati yao asilimia 46 ni wanawake na 54 wanaume.

Wahitimu 215 walitunukiwa astashahada, 1,153 Shahada ya Kwanza, 433 shahada ya uzamili na wawili shahada ya uzamivu.

Jumla ya wahitimu katika kampasi kuu ya Morogoro, Dar es Salaam na Mbeya ni 3,554, ukilinganisha na wahitimu 3,049 mwaka 2011/12, sawa na ongezeko la wahitimu 504 walihitimu katika mahafali hayo.

Alisema ongezeko hilo ni sawa na asilimia 16 ambapo wahitimu 24 wamepata daraja la kwanza ikilinganishwa na 17 mahafali yaliyopita.

Pia alisema kutokana upungufu wa wanasayansi nchini, chuo kimeandaa program za shahada ya sayansi asili na tumizi kukabili hali hiyo na kuunga mkono Mpango wa Elimu ya Juu 2010-2020 wa vyuo vikuu kuongeza fursa za sayansi.

Mikakati ya kuanzisha program hizo inafanywa kwa  kushirikiana na vyuo vingine vikuu nchini na nje kama ilivyoainishwa katika mkakati wa tatu wa chuo wa 2012/13-2016/17 wa kuwa na mtizamo anuwai katika program zake.

Pia Chuo kwa kushirikiana na vyuo vikuu vya Korea kinatarajia kuanzisha kijiji cha sayansi ambapo program mbalimbali zikiwamo za kompyuta zitaanzishwa chini ya kitivo cha sayansi na teknolojia.

Alisema pamoja na mafanikio na mipango iliyopo, Chuo kinakabiliwa na ufinyu wa bajeti ambayo haikidhi mahitaji halisi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Profesa Daniel Mkude, alisema mhitimu kumaliza masomo siyo mwisho wa kujifunza, bali wazidi kujenga tabia ya kujisomea na kuchota maarifa.

“Taifa linawahitaji...mzidi kujisomea na kuendelea na hatua nyingine ya masomo,” alisema.

Alishauri wahitimu hao kujiepusha na tabia zisizofaa kwa vile taifa linapoteza rasilimali watu kutokana na baadhi hujiingiza katika matendo ya ulevi na kupoteza maisha wakiwa na umri mdogo.

Pia alisema wahitimu hao wanatakiwa kuwa mfano kwa jamii kwa kupiga vita ufisadi, wizi, mauaji ya vikongwe, imani za kishirikina, ukahaba, ubakaji, mauaji ya albino na utupaji wa watoto.

Mahafali ya Chuo Kikuu Mzumbe, pia yalihudhuriwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe, Tunu ambao walishiriki kama wazazi na kushuhudia mmoja wa watoto wao akipata shahada yake.
 
Chanzo.  Ippmedia.com

Jumatano, 4 Desemba 2013

Asakwa kwa kutorosha,kubaka mwanafunzi

Wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili na unyayasaji wa kijinsia, mtoto mwenye umri wa miaka 14 (jina linahifadhiwa) mkazi kijiji cha Chinangali mpakani mwa Kibaigwa, Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma, amebakwa na kulawitiwa kwa muda wa wiki mbili.

Akizungumza jana na NIPASHE, Mhudumu wa Shirika la lisilo la Kiserikali linalopinga ukatili wa kijinsia na watoto (Afnet) kwa kushirikiana na Tunajali, Mnemelwa Simba, alisema tukio hilo lilitokea katika kijiji hicho hivi karibuni.

Simba alisema wazazi wa mtoto huyo walifika kwa mhudumu huyo kuomba ushauri baada ya kuona mtuhumiwa wa ukatili huo akiwa hajachukuliwa hatua stahiki za kisheria na vyombo husika.

Alisema mtoto huyo, ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari iliyopo Kibaigwa, amelazimika kusitisha masomo ili kupata matibabu kutokana na kufanyiwa ukatili huo.

Alisema mtoto huyo alifungiwa ndani ya nyumba kwa muda huo na mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Hassan, ambaye ni mgeni katika kijiji hicho anayefanya vibarua vya ujenzi.

 “Mimi namjua huyu. Anatambulika kwa jina la Hassan. Na ni mgeni. Hata mwaka hajamaliza. Na mpaka sasa yupo, ni mtu na akili zake, aliyefanya kitendo hiki,” alisema Simba.

 Alisema wazazi wa mtoto huyo baada ya kumtafuta kwa muda mrefu, walitoa taarifa kwa ulinzi shirikishi ili kumtafuta.Simba alisema baadaye iligundulika kijana huyo akiwa na binti huyo, alimuhamishia katika Kijiji cha Ndurugumi.Alisema walipofika katika kijiji hicho walisikia amehama naye tena.

 Simba alisema mtoto huyo alikutwa katika Kijiji cha Ngomai kwa kaka yake na Hassan. Alisema Hassan alidai kuwa mtoto huyo alipelekwa na mdogo wake.

 Mama mzazi wa mtoto huyo, Suzan Fugusa, alisema ilikuwa siku ya Jumapili mtoto wake alimuaga anaenda kanisani kama ilivyo kawaida.
Alisema baada ya kuona muda umepita na mtoto huyo hajarudi kutoka kanisani walianza kumtafuta.

Fugusa alisema baada ya siku kadhaa kupita, walikwenda kutoa taarifa kwa ulinzi shirikishi na kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa.

“Baada ya kumtafuta katika hivi vijiji na kufanikiwa kumpata mkuu wa mtaa alisema suala hilo ni kubwa na kutuambia twende polisi ambako tulihojiwa na mtuhumiwa alikubali kuwa alimtorosha mtoto huyo,” alisema Fugusa.Alisema polisi waliwataka kwenda hospitali kufanyiwa vipimo.

Fugusa alisema walimpeleka, lakini kulingana na woga wa mtoto huyo, alishindwa kueleza ukweli kuhusu vitendo alivyokuwa akifanyiwa.

 “Baada ya kumpima ukimwi na mimba tukarudi nyumbani. Na mara baada ya kurudi akiwa na bibi yake, alienda kujisaidia.
Ndipo haja zote zikawa zinatoka kwa pamoja. Tukarudi hospitali tena. Tulipoona mambo tofauti, alipimwa akagundulika kweli aliingiliwa kinyume cha maumbile na kuanza matibabu ambayo anaendelea mpaka sasa,” alisema Suzan na kuongeza:

 “Tumetumia gharama nyingi kumtafuta mtoto wetu mpaka kumfuata. Na hii kesi ilishafika mahakamani isipokuwa hukumu imetolewa haraka kabla hatujapeleka ripoti ya pili ya daktari iliyogundua ameingiliwa na mtuhumiwa yupo nje hata hatuelewi tuanzie wapi. ”

Kwa upande wake, mtoto huyo alisema siku ya tukio alikuwa akitoka kanisani na kukutana na kijana huyo, ambaye alimwambia waende nyumbani.
Alisema baada ya kufika nyumbani kwa Hassan, alimzuia kurudi  nyumbani kwao na kumfungia ndani na kuanza kumuingilia kinyume cha maumbile kila kijiji walichokuwa wakienda.

“Kwa sasa naendelea na matibabu. Nimesitisha masomo mpaka nitakapopona. Maana niliumizwa. Bado nasikia maumivu makali,” alisema mtoto huyo.

Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE,  Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibaigwa, Inspekta Beda Msoma, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
 Msoma alisema jalada lilifunguliwa kituoni hapo kwa hati ya mashitaka ya kubaka KBG/247/2013.

Alisema kesi hiyo ilikuwa na ushahidi wa kutosha na haelewi kwa nini mtuhumiwa ameachiwa huru, hivyo ataifuatilia kwa mpelelezi wake kuona kwa nini iliamuliwa hivyo.
“Hii kesi naijua ilivyokuja kuripotiwa. Nilifanya jitihada zote. Nikafanikiwa kuifikisha mahakamani ikiwa na ushahidi wa kutosha. Sasa nashangaa kusikia eti yupo huru.

Iliamuliwa vipi wakati ilikuwa na vithibitisho… Huyu binti nilimpeleka akafanyiwa councelling (ushauri) kwa madaktari wakishirikiana na ustawi wa jamii,” alisema Inspekta Msoma.

Alisema mtoto huyo alipimwa na kugundulika kuwa alibakwa.

Msoma alisema baada ya siku mbili, bibi ya mtoto huyo alirudi polisi na kudai kuwa ameona hali tofauti ndipo akapimwa tena na kubainika aliingiliwa pia kinyume cha maumbile.
CHANZO: NIPASHE

Jumatatu, 2 Desemba 2013

picha 5 zinazoonyesha choo tegemezi cha shule ya msingi Kiara na Nyang'omboli

choo cha shule ya msingi Nyang'omboli na Kiara
korido ya choo ilivyo
mashimo ya choo hicho hayana mifuniko
mashimo ya choo yakiwa wazi



choo kinavyoonekana


Jumapili, 1 Desemba 2013

Serikali kusaidia mikakati ya taasisi zinazosaidia elimu

Naibu Katibu Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Zuberi  Samatama, amesema serikali itasaidia mikakati inayoibuliwa na taasisi mbalimbali za kiserikali katika kuboresha elimu ya msingi nchini.
 
Samatama alisema hayo, wakati akizindua kampeni ya uboreshaji wa elimu ya msingi Manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam, inayofahamika kama Mnazi mkinda.
 
Alisema kampeni hiyo ambayo lengo lake kubwa ni kuhakikisha wanafunzi wanakuzwa vipaji walivyozaliwa navyo, ni jambo la kuigwa kwani itawafanya watoto kuhudhuria masomo kwa muda wote.
 
Alisema serikali itahakikisha inaanzisha tuzo maalum kwa walimu wabunifu kwa ajili ya kuwapa moyo na kuwatambua.
 
"Kitu hiki mlichokibuni kitasaidia sana katika kuhakikisha wanafunzi wanapenda kusoma kwa sababu watatambua kile wanachokipenda kipo kwenye shule zao," alisema Samatama.
 
Alisema katika mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), umesababisha ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi wa darasa la saba kutoka kiwango cha asilimia 5.6 hadi silimia 75, mwaka jana.
 
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mwenda Hasara Maganga, alisema kampeni ya Mnazi mkinda, itawavutia watoto kwa kupenda shule na kuacha tabia ya ukwepaji.
"Kwa ujumla tatizo la machimbo halitakuwepo kwa sababu kila mtoto atapata kile anachopenda," alisema.
 
Baadhi ya vipaji vitakavyokuzwa katika kampeni hiyo ni pamoja na Hisabati, Sayansi, Teknohama, Dini na Sanaa ya maigizo, ngoma, muziki na sarakasi.
 
Afisa Elimu ya Msingi wa Manispaa hiyo, Elizabeth Thomas, alisema kampeni ya Mnazi mkinda imesambazwa kwenye shule zote pamoja na kuandaa kituo maalumu cha ukuzaji vipaji katika shule ya msingi Mnazimmoja.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

halmashauri Mbozi yashindwa kulipa pesa ilizowakopa walimu sh.milioni 200


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), Hawa Ghasia
 
Chama cha walimu wilaya ya Momba na Mbozi, kimemuomba Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, kuwasaidia walimu kulipwa fedha zao zaidi ya Sh. milioni 200 walizokopwa na halmashauri ya wilaya ya Mbozi.
 
Fedha hizo zilikopwa kwa walimu mapema mwaka huu, zilikuwa michango ya walimu waliyokuwa wakikatwa kutoka kwenye mishahara yao kwa ajili ya kuweka akiba kwenye Chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS).
 
Akiwasilisha malalamiko hayo kwa niaba ya walimu wote,  alisema walimu hao waliambiwa na halmashauri kuwa fedha hizo zimetumika kwa ajili ya shunguli zilizo nje ya shughuli za walimu.
 
Awali walimu hao wilaya ya Mbozi na Momba walikuwa wilaya moja kabla ya kugawanywa na kuwa mbili. Walipotaka kufahamu kuhusu fedha hizo waliambiwa zimetumika kuandaa sherehe za wafanyakazi (Mei Mosi) ambazo mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.
 
Wakionyesha kukata tamaa na madai ya malimbikizo ya madeni wanayoidai serikali zaidi ya shilingi bilioni moja kwa wilaya hiyo, pia walizidi kuvunjika moyo baada ya kutaka kuwasilisha kilio chao kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Tamisemi), Hawa Ghasia, na kukataa kuwasikiliza kwa madai kuwa serikali imeshamaliza matatizo yao.
 
Katika taarifa iliyosomwa na Nyanguye ilisema kuwa, Ghasia alimkataza Katibu wa Chama Cha Walimu, Emilia Mwakyoma aliyekuwa akisoma taarifa kwa kumtaka akae chini mara moja kwani hawezi kusikiliza madai ambayo yameshamalizwa.
 
Alisema hali hiyo ilisababisha walimu kushindwa kuwasilisha malalamiko yao siku hiyo, na hivyo kulazimika kuyawasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM, Kinana ili kuomba msaada kama wanaweza kusaidiwa.
 
“Tumekuja tu kujaribu kama tunaweza kusaidiwa kwani walimu tumeshasahaulika sana. Licha ya kusahaulika pia tunanyang’anywa haki zetu za msingi na Serikali na hatujui kama tutazipata na wala hatuoni wakumlalamikia tena zaidi ya kuishi kwa matumaini," alisema Nyanguye.
 
Akijibu malalamiko yao kwa mshangao, Katibu Mkuu CCM, Kinana alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi, Charles Mkombachepa kueleza matumizi ya fedha hizo za walimu, ambazo zinadaiwa kutumika kuandaa sherehe bila ya wakopwaji kutaarifiwa chochote.
 
“Unachotakiwa Mkurugenzi ni kuwaeleza walimu fedha zao umezitumia kufanyia nini, angalia bado wakiwa wana machungu ya madeni wanayoidai serikali, hivi serikali inatakiwa kukopa au kukopwa na tangia lini Mei Mosi zikaandaliwa na walimu? " alihoji Kinana.
 
Akijibu tuhuma hizo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbozi, Mkombachepa, alikiri kutumia fedha hizo lakini kwa ajili ya kulipia huduma zilizotolewa na taasisi mbalimbali wilayani hapo.
 
"Katibu Mkuu, kweli fedha hizo zilitumika, lakini si kwa ajili ya Mei Mosi bali zilitumika kuandaa usafiri, kurekebisha magari na shughuli nyingine ambazo hazihusiani na walimu moja kwa moja," alisema Mkombachepa.
 
Mkombachepa, aliomba kuzilipa fedha hizo ndani ya miezi miwili kuanzia Desemba na kumaliza mwezi Januari mwakani, taarifa ambayo ilizidi kumkasirisha Kinana.
 
Kwa fedheha kubwa Kinana, alimtaka Mkurugenzi huyo kuacha kuwafanyia walimu usanii kwenye fedha zao ambazo wamezipata kwa taabu na kuagiza walimu hao kulipwa fedha zao haraka iwezekanavyo.
 
Aidha Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Asha Rose Migiro, aliahidi kuyashughulikia matatizo ya walimu kwa kufikisha taarifa za matatizo yao, ikiwamo malimbikizo  ya madeni wanayoidai serikali kwa viongozi wanaohusika.

Ijumaa, 29 Novemba 2013

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa vita nchini Syria vimesababisha kuharibu watoto kimwili na kisaikolojia.


Wakimbizi watoto walio katika umri wa kwenda shule ambao wamekimbilia katika nchi jirani wameendelea kukosa elimu na wanalazimika kufanyakazi ili kujikimu.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi limesema watoto wapatao 300,000 wanaoishi nchini Lebanon na Jordan huenda wakakosa masomo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2013.
Wengi wa ambao hawaendi shuleni wanakwenda kufanyakazi kwa muda mrefu wakipata malipo kidogo, wakiwa na umri mdogo wa hata miaka saba.
Zaidi ya nusu ya wakimbizi wa Syria milioni 2.2 ni watoto, wengi wakikabiliwa na hatari kubwa na hata nje ya eneo la vita.
Hatari hizo ni pamoja na athari za kimwili na kisaikolojia.
Akizindua ripoti hiyo, Kamishina wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Antonio Guterres alisema: "Kama hatutachukua hatua haraka, kizazi cha watu wasio na hatia kitaishia kufa kutokana na vita."
Utafiti huu ni mpya kabisa na unajaribu kuonyesha madhara makubwa kwa watoto kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vilivyodumu kwa miaka mitatu. Madhara hayo ni kwa watoto walio ndani na nje ya mipaka ya Syria.

chanzo bbc.com

Jumapili, 10 Novemba 2013

chama cha walimu kuidai tena serikali

Chama  Cha Walimu Tanzania (CWT) kimeipa serikali siku 60 za kukamilimisha madeni ya mishahara ya walimu ya Sh. bilioni 48 pamoja na kukamilisha majadiliano ya mishahara  ya walimu na chama hicho.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Rais wa CWT, Gratian Mukoba, wakati akizungumza na NIPASHE kuhusu maazimio ya mkutano mkuu wa Taifa wa walimu nchini uliofanyika mkoani Arusha  Oktoba 28-29, mwaka huu.
Mukoba alisema hatua hiyo ilifikiwa na chama hicho baada ya serikali kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutekeleza ahadi walizokiahidi chama hicho juu ya madai ya walimu ya muda mrefu.
Alisema chama hicho kinaidai serikali zaidi ya Sh. bilioni 48, ambazo serikali ili ahidi kuzilipa Septemba mwaka huu, lakini hawakufanya hivyo badala yake ikasema  inafanya uhakiki kwanza wa madai hayo ili kukamilisha malipo hayo ambayo mpaka sasa hayajafanyika.
“Tuliendelea kukaa kimya tukisubiri serikali ikamilishe uhakiki wake na kutoa taarifa ya madai ambayo walimu wanaidai, lakini bado haikufanya hivyo, kwa hiyo na sisi baada ya kukaa kikao chetu cha walimu Taifa tukaweka maazimio haya,” alisema Mukoba.
Alisema wanatarajia kukabidhi barua ya notisi kwa Katibu Mkuu Kiongozi leo na hatua za kisheria zitafuata endapo serikali haitatimiza hayo ambayo wameyaorodhesha baada ya siku 60 kumalizika.
Alisema, maazimio mengine waliyoyaandika  kwenye barua hiyo ya notisi ni serikali iwe imebadilisha muundo wa walimu na wakaguzi ndani ya siku hizo 60.Azimio lingine  waliitaka serikali kukamilisha majadiliano na chama cha walimu kuhusu mishahara ya walimu ya mwaka ujao kwa mwaka  wa fedha wa 2013/2014.
“Haya yote na mengine ambayo sijakuainishia tunayataka yatekelezwe na serikali ndani ya siku hizi 60 tulizotoa na endapo serikali itaendelea kukaidi basi hatua zaidi za kisheria zitafuata na tutatoa msimamo wa chama kuwa nini kitafanyika,” alisema Mukoba.
NIPASHE lilimtafuta Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, jana ili kuzungumzia suala hilo, lakini simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.Hata Naibu Waziri, Philip Mulugo, alipotafutwa simu yake ilikuwa ikiita bila majibu.
 ippmedia.com

Jumatatu, 4 Novemba 2013

TAMKO LA HAKIELIMU KUHUSU UPANGAJI WA VIWANGO VYA ALAMA, MATUMIZI YA ALAMA ENDELEVU YA MWANAFUNZI NA UFAULU 4 NOVEMBA 2013.


Hivi karibuni serikali imetoa tamko kuhusu mfumo mpya wa upangaji wa viwango vya alama, matumizi ya alama endelevu ya mwanafunzi na ufaulu. HakiElimu na wadau wake imetafakari tamko hilo na kutoa maoni ya yafuatayo:

1. Hatujatambua lengo la serikali kuleta mabadiliko haya; hasa ikikumbukwa kuwa Tume ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda haijawahi kuweka bayana taarifa yake kuhusu sababu za wanafunzi kutofaulu vizuri katika mitihani ya kumaliza kidato cha nne. Wajumbe wa Tume hiyo wamekuwa wakitoa dondoo fupi fupi za matokeo ya kazi yao-kama vile Bungeni na katika hadhira nyingine za kitaifa; bila kutoa ripoti yenyewe. Je, kwa mabadiliko haya,wizara inataka kuwaaminisha Watanzania kwamba alama zilivyokuwa zimepangiliwa hapo awali,ndiyo sababu kuu ya wanafunzi kutofaulu vizuri?

2. Wizara imeeleza kwenye tamko lake kwamba imeshirikisha wadau mbalimbali katika kufikia uamuzi huo. Hata hivyo, katika orodha ya wadau walioshirikishwa inaonekana bayana kuwa asasi za utetezi hazikupewa nafasi. Baada ya kufanya mawasiliano na baadhi ya wadau wanaodaiwa kushiriki,wenyewe wamekiri kuwa ingawa walishiriki mawazo yao hayakuzingatiwa na hawakukubaliana kuhusu kushusha alama za ufaulu kufikia 20 kati ya 100.

3. Mpangilio wa alama zitakazotumika kuanzia mwaka huu unaleta tafsiri ya ndani kuhusu nia ya wizara kubadilisha alama hizo. Tafsiri hiyo ni kulazimisha kuona kwamba wanafunzi wachache zaidi wanapata daraja la 5 (ambalo limeanzishwa badala ya daraja sifuri); kukiwa na uwezekano wa kupunguza wanafunzi wanaopata daraja hili kwa asilimia 2.2% ukilinganisha na utaratibu uliotumika kwa matokeo ya mwaka 2012. Mpangilio huo mpya una uwezekano wa kuongeza kundi la wanafunzi wanaopata daraja la tatu na la nne kwa asilimia 12.1% kuliko utaratibu uliotumika mwaka 2012. Hata hivyo, alama hizo mpya zinaweza kupunguza uwezekano wa kupata daraja la kwanza na la pili kwa asilimia 11.9%. Serikali na wadau wengine wa elimu wanatambua bayana kuwa njia kuu ya kuboresha elimu na matokeo katika mitihani ni kuboresha utaratibu wa utoaji wa elimu. Kwa nini serikali, hasa katika kipindi hiki inataka kuona matokeo mazuri bila kuwekeza kwenye mipango ya kuboresha mfumo na utaratibu wa utoaji wa elimu? HakiElimu inatafsiri uamuzi huo wa serikali kama ni kukwepa ukweli na utaalamu; na badala yake serikali inatafuta njia ya mkato ya kuwafurahisha wazazi na wananchi ili wapunguze kelele.

4. Serikali imekubali kutumia asilimia 40 kutoka kwenye Alama za Tathmini Endelevu ya Mwanafunzi (Continuous Assessment, CA), ili ziunganishwe na alama 60 za mtihani wa mwisho. Hata hivyo, uzoefu unaonesha kuwa alama hizo zilikuwa zinachakachuliwa huko shuleni, na hata Baraza la Mitihani Tanzania mwaka huu walikiri hilo kutokea. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itatumia njia gani kuhakikisha kuwa zinapatikana alama sahihi toka shuleni zinazoendana na uwezo wa mwanafunzi? Je, kwa kiasi gani walimu wameandaliwa na kujengewa mazingira mazuri ya kufanikisha zoezi hili? Hata hivyo, serikali inapaswa pia kuwaeleza watanzania uzoefu wa nchi nyingine za Afrika katika matumizi ya alama za CA; wengine wanatumia asilimia ngapi? Ni muhimu kuwa na ushahidi kuwa kiwango cha CA tutakachokitumia kitaboresha utaratibu wa kutathmini wanafunzi; na kuwatendea haki badala ya kuwaghiribu au kuwaumiza.

5. HakiElimu inasikitika kuona wizara inalazimisha kila mwanafunzi atakayefanya mtihani wa kidato cha nne au cha sita awe amefaulu. Hiyo inathibitishwa na tafsiri ya alama ambazo zitatumika zinazoonesha kwamba kuanzia atakayepata alama sifuri mpaka mia moja atakuwa amefaulu kwa namna fulani. Kwa mfano, hata atakayepata alama kuanzia 0 mpaka 19 katika somo fulani atahesabiwa kuwa amefaulu, japo katika kiwango kisichoridhisha. Kwa nini wizara inakosa ujasiri wa kukubali kuwa mwanafunzi atakayepata chini ya alama fulani ahesabiwe kuwa hakufaulu?

6. Kwa upangaji huo mpya wa alama za ufaulu, Tanzania itakuwa nchi ya kwanza katika bara la Afrika kwa kuwa na kiwango cha chini kabisa cha ufaulu katika elimu ya sekondari na kuna hatari kwamba kushushwa kwa alama za ufaulu kutapunguza ama kuondoa hamasa ya wanafunzi kusoma kwa bidii, kwa kuamini kuwa hawatafeli na cheti watapata tu. Kama wadau wote tunakubaliana kuwa nia ya kutoa elimu ni kuandaa Watanzania ambao watakuwa na maarifa na uwezo wa kushindana na wengine wanaosoma katika nchi nyingine Afrika.

7. HakiElimu pia inasikitika kuona kuwa wizara inapotosha malengo ya “Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now-BRN)” kwa kutafuta njia za mkato. BRN imeeleza bayana kuwa kati ya mikakati itakayotumika kupata Matokeo Makubwa katika elimu ni kuboresha mchakato wa kufundisha na kujifunza shuleni na kuboresha utaratibu wa utoaji wa elimu kwa kuweka bayana majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na ile ya TAMISEMI. Wizara iwaambie Watanzania kuwa kwa kiasi gani upangaji huu wa alama utasaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa maana ya kumjengengea mwalimu uwezo, mazingira mazuri na hamasa ya kufundisha na pia kutengeneza mazingira mazuri ya mwanafunzi kujifunza. Katika haya, je, ni kweli kwamba huu upangaji upya wa madaraja ni kipaumbele chetu namba moja? Si busara kushughulikia mpangilio wa alama na madaraja kwanza wakati mchakato wa kuboresha mfumo wa elimu ili kupata hayo matokeo mazuri bado uko chini. Kitendo hicho ni kukurupuka na kuruka hatua muhimu zinazoweza kuboresha elimu.

8. HakiElimu inawatahadharisha Watanzania, wakiwemo wazazi, wanafunzi na vijana wenye nia ya kurudia mitihani ili wapate vyeti; na serikali yenyewe kuzingatia ukweli kwamba: Elimu ni uwezo, SIYO cheti. Jitihada za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinaonesha wazi kuwa nia ni kuona matokeo mazuri hata kama matokeo hayo hayataendana na uwezo walio nao wanafunzi. Katika kutengeneza raslimali watu ya kutosha, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine haina namna ya kukwepa kuhakikisha kwamba mfumo wa elimu unaandaa vijana au wananchi wenye uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili wao wenyewe, jamii na Taifa kwa ujumla; pia kuwa na wananchi ambao watakuwa na ujasiri, tija na ubunifu, katika uzalishaji katika shughuli na fursa mbalimbali watakazozipata au kuzitafuta. Hali hii haipatikani kwa kuhangaika na alama za ufaulu kama kipaumbele. Tunahitaji kuhangaika na mfumo wa utoaji elimu utakaotusaidia kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

HakiElimu inaishauri Serikali kusitisha matumizi ya alama na madaraja haya mapya. Irudi kwa wadau na ushahidi kuhusu uamuzi huu; huku ikitoa nafasi ya kuchukua maoni ambayo yanaweza kuboresha mfumo wa upimaji wa wanafunzi. Wakati zoezi hilo linaendelea, HakiElimu inaisisitiza Serikali kutumia matokeo ya tafiti mbalimbali na mipango iliyopo kushughulikia dosari na changamoto zinazorudisha nyuma elimu yetu, hasa zile zinazokwamisha ufundishaji na ujifunzaji shuleni.
Tamko hili limesainiwa na,

Elizabeth Missokia Mkurugenzi Mtendaji, HakiElimu

Big results now itafanikiwa kuongeza ufaulu lakini itaua ubora wa elimu

kwa mara ya kwanza leo Marafiki wa elimu musoma tumeweza kuzungumza na baadhi ya wanafunzi kuhusu mtihani wa taifa wa kidato cha nne, majibu tuliyoyapata kwa wanafunzi yanatia matumani sana kati ya wanafunzi 70 wa shule 5 tofauti hapa musoma tuliowahoji jinsi wanavyouona mtihani wanafunzi 65 wamesema mtihani ni rahisi wanafunzi wanafunzi 5 tu wamesema mtihani ni mgumu hii inaonyesha mwelekeo wa matokeo yajayo yanaweza kuwa mazuri zaidi ikilinganishwa na alama za ufaulu jinsi zilivyolegezwa marafiki wa elimu tunawatakia wanafunzi waendelee na mtihani na wazidishe bidii wapate division 1 maana ndio yenye unafuu kwao

Jumamosi, 2 Novemba 2013

kufutwa kwa division ziro je ni mpango wa kutekeleza Big results now

hivi karibini serikali imetangaza mabadiliko ya alama za ufaulu kama inavyoonekana hapo chini

A ni 75 hadi 100; huu ni ufaulu uliojipambanua
B+ ni 60 hadi 74; huu ni ufaulu bora sana
B ni 50 hadi 59; huu ni ufaulu mzuri sana
C ni 40 hadi 49; huu ni ufaulu mzuri
D ni 30 hadi 39; huu ni ufaulu hafifu
E ni 20 hadi 29; huu ni ufaulu hafifu sana
F ni 0 hadi 19; huu ni ufaulu usioridhisha

Kimsingi alama yoyote kuanzia sifuri hadi mia moja ni ufaulu wa aina flani;

Madaraja yatakuwa kama ifuatavyo;

Division One = pointi 7 hadi 17
Division Two= pointi 18 hadi 24
Division Three = pointi 25 hadi 31
Division Four= pointi 32 hadi 47
Division Five = pointi 48 hadi 49

Yaani mtu akipata E mbili na F tano, ana division four; au akipata D moja na F sita atakuwa na division four.

swali la msingi tunalopaswa kujiuliza ni je huu ndio utekelezaje halisi wa MATOKEO MAKUBWA SASA na kama ndio utekelezaje serikali haijaweka wazi na kuwaelimisha wadau juu kusudio hasa lililopelekea kupangwa kwa alama za ufaulu marafiki wa elimu tunaamini kwamba kupangwa kwa alama za ufaulu si suruhisho la matatizo ya elimu yanayokabili nchi ila tunaamini kuwa serikali ikitekeleza malengo yaliyobainisha kwenye vipaumbele vya mpango wa big results now elimu itafanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.

Jumatatu, 28 Oktoba 2013

maafisa elimu watakiwa kuthamini michango ya walimu

mkuu wa wilaya ya Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, John Mongella, amesema mabadiliko ya haraka katika elimu yanaweza kutokea iwapo walimu watawezeshwa kitaaluma na kuwahimiza maafisa elimu kutoa motisha na kutambua mchango wa anayefanya vizuri ili kuwajengea zaidi morali.

Mongella aliyasema hayo katika hafla maalum ya kutoa zawadi na vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha tatu waliofanya vizuri mitihani ya majaribio kwa  mikoa ya Arusha na Kilimanjaro katika masomo ya Hisabati, Elimu viumbe, Kemia, Fizikia na Kiingereza iliyoandaliwa na asasi ya Asante Africa Foundation , Africaid na Chuo Kikuu cha Elimu cha Mwenge kilichopo mjini Moshi.

 “Kuendelea kwa nchi yoyote ile ni pale inapokuwa na wana sayansi wengi zaidi…mwanasiasa gani utaendesha nchi ambayo haina wanasayansi?” alihoji.
Alisema maofisa elimu wanaweza kuanzisha mradi kama huo wa kufanya majaribio ya mitihani kwa wanafunzi wa sekondari zilizopo kwenye mikoa yao au kwa kushirikiana na mikoa mingine.

“Hii ni changamoto kwa maofisa elimu, wanaweza kutenga hata Sh. milioni 10 kwa ajili ya walimu wa masomo hayo na kama wanafunzi watakuwa wamefanya vizuri wanaweza kuzawadiwa,” alisema.

Mongella alisema  hata katika programu  ya ‘Matokeo makubwa sasa’ inahitaji walimu waongezewe uwezo ili wanafunzi waweze kufanya vizuri zaidi na inawezekana kuwa hivyo kwa kuwashindanisha.

Kwa upande wake, meneja wa mradi huo wa uwezeshaji walimu wa shule za sekondari, Sokoro Munubi, alisema malengo yao yanaendana na mpango wa serikali unaosisitiza 'matokeo makubwa sasa' katika sekta ya elimu.

“Kwanza tunawajengea uwezo walimu kwa kuwapatia mafunzo ya mara kwa mara pamoja na kufanya ufuatiliaji wa mafunzo yanayotokana na walimu wao wenyewe katika maeneo ya shuleni.

Akizungumzia mafanikio ya mradi huo tangu kuanzishwa kwake, alisema umekwisha kufundisha walimu 80 wa sekondari 40 zilipo wilaya tisa za mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Alisema walimu 560 kutoka shule hizo nao wamekwisha kufundishwa na walimu wenzao katika maeneo ya shule zao na pia mradi umefadhili mitihani ya majaribio kwa wanafunzi wa kidato cha tatu na kwamba wanafunzi 4,500 walishiriki kufanya mtihani huo.
Alisema kuanzia mwakani mradi huo unatarajia kuongeza mikoa miwili lengo likiwa kufikia mikoa sita kwa baadaye.
chanzo. ippmedia.com & nipashe

madudu yagunduliwa tume ya pinda

Ripoti ya Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mapema mwaka huu, iliibua madudu mengi ambayo hayajawekwa hadharani.
Wajumbe waliounda kamati hiyo kwa nyakati tofauti waliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa waligundua mambo mengi yanayodhihirisha udhaifu mkubwa katika uendeshaji wa sekta ya elimu nchini. Sehemu kubwa ya matokeo ya uchunguzi huo inasemekana yamejikita zaidi katika kuzitupia lawama taasisi za Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Udhaifu wa kiutendaji kati ya taasisi hizo mbili unadaiwa umechangia kwa wanafunzi wengi kufanya vibaya kwenye mitihani ya Kidato cha Nne mwaka jana kiasi cha kuilazimisha Serikali kuunda tume kuchunguza tatizo kutokana na kilio kikubwa cha wadau wa elimu na wananchi.
Viongozi watatu waandamizi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi hawakupatikana kuzungumzia uchunguzi huo jana. Simu ya Waziri wa wizara hiyo, Dk Shukuru Kawambwa haikupatikana kabisa pale ilipopigwa.
Naye Naibu wake, Philipo Mulugo alijitetea kwamba alikuwa na shughuli nyingi na hivyo hakuwa na muda wa kuzungumzia suala hilo wakati Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Sifuni Mchome hakupokea kabisa simu yake.
Matokeo hayo ya mtihani wa Kidato cha Nne uliofanyika mwaka jana yanaonyesha kuwa watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 walipata sifuri, huku wanafunzi 23,520 tu ambao ni sawa na asilimia 5.16 ndiyo waliofaulu na wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakiwa wamepata daraja la nne. Katika mtihani huo, watahiniwa 397,136 walikuwa wa shule na 68,806 wa kujitegemea.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Mkuu Pinda aliamua kuunda tume iliyoanza kufanya kazi kuanzia Machi hadi Juni mwaka huu. Tume hiyo iliyokuwa inaongozwa na Profesa Mchome ilimkabidhi Waziri Mkuu ripoti Juni 15, mwaka huu.Hata hivyo, ripoti hiyo haijawahi kutolewa hadharani baada ya tume kumaliza kazi yake.
Badala yake imeshuhudiwa Profesa Mchome, ambaye alikuwa Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Vyuo Vikuu Tanzania akipandishwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Huku kwa upande mwingine, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako akichukua likizo ya muda mrefu ya mapumziko.
Madudu yaliyogunduliwa na tume
Wajumbe wa tume hiyo walisema kuwa matokeo ya uchunguzi wao yalibaini kuwa, maswali na mitihani iliyotungwa ilikuwa ni ile yenye kuzingatia maudhui badala ya kuzingatia kujenga maarifa na ujuzi.
“Tulitegemea kwa vile tangu mwaka 2006, mihutasari ya elimu ya Tanzania ilibadilika kutoka ile inayozingatia maudhui, kwenda kwenye ile inayozingatia kujenga maarifa na ujuzi basi na mtihani ungekuwa na mwelekeo huo,” alisema mmoja wa wajumbe wa tume ile.
Pia uchambuzi wa kamati ile uligundua kuwa hakukuwapo mawasiliano kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).TET, ambao ndio wasimamizi wa mitalaa ya elimu walitakiwa kuhakiki mitihani ile baada ya kutungwa na Necta, lakini hilo halikufanyika.
Chanzo kingine kililiambia gazeti hili kuwa tume hiyo ilibaini katika uchunguzi wake kuwa Necta ilitumia wataalamu wasio na juzi wa kutosha kutunga na kuhakiki mitihani. Uchunguzi huo ulibaini baadhi ya mitihani kama ya masomo ya Hisabati, Kemia na Fizikia ilikuwa na maswali yaliyohitaji muda mwingi wa kuyajibu kuliko uliopangwa.
“Hii ilifanya wanafunzi kushindwa kukamilisha kujibu maswali yote yaliyotakiwa kujibiwa kwenye mitihani hiyo. Pia tulibaini kwamba baadhi ya maswali katika mitihani ya masomo ya Fizikia na Kemia yalikuwa nje ya mihutasari iliyotumika kuwaandaa wanafunzi,” aliongeza mjumbe mwingine.Mjumbe mmoja aliongeza pia kuwa mitihani ilikuwa na misamiati migumu na hata kuwasumbua walimu walioisahihisha.
Hali hii inaweza kuwa imechangia, kwa kiasi kikubwa, kuongeza ugumu wa mitihani hiyo na hili linaweza kuchangia wanafunzi kushindwa kuelewa vizuri maswali wanayoulizwa kwenye mitihani.
Wajumbe wa tume hiyo walieleza hali hiyo imefanya imani kujengeka kuwa mitihani ya Tanzania ni migumu kuliko ya nchi nyingine.Huku kwa upande mwingine, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako akichukua likizo ya muda mrefu ya mapumziko.
Madudu yaliyogunduliwa na tume
Wajumbe wa tume hiyo walisema kuwa matokeo ya uchunguzi wao yalibaini kuwa, maswali na mitihani iliyotungwa ilikuwa ni ile yenye kuzingatia maudhui badala ya kuzingatia kujenga maarifa na ujuzi.
“Tulitegemea kwa vile tangu mwaka 2006, mihutasari ya elimu ya Tanzania ilibadilika kutoka ile inayozingatia maudhui, kwenda kwenye ile inayozingatia kujenga maarifa na ujuzi basi na mtihani ungekuwa na mwelekeo huo,” alisema mmoja wa wajumbe wa tume ile.
Pia uchambuzi wa kamati ile uligundua kuwa hakukuwapo mawasiliano kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta).TET, ambao ndio wasimamizi wa mitalaa ya elimu walitakiwa kuhakiki mitihani ile baada ya kutungwa na Necta, lakini hilo halikufanyika.
Chanzo kingine kililiambia gazeti hili kuwa tume hiyo ilibaini katika uchunguzi wake kuwa Necta ilitumia wataalamu wasio na juzi wa kutosha kutunga na kuhakiki mitihani.Uchunguzi huo ulibaini baadhi ya mitihani kama ya masomo ya Hisabati, Kemia na Fizikia ilikuwa na maswali yaliyohitaji muda mwingi wa kuyajibu kuliko uliopangwa.
“Hii ilifanya wanafunzi kushindwa kukamilisha kujibu maswali yote yaliyotakiwa kujibiwa kwenye mitihani hiyo. Pia tulibaini kwamba baadhi ya maswali katika mitihani ya masomo ya Fizikia na Kemia yalikuwa nje ya mihutasari iliyotumika kuwaandaa wanafunzi,” aliongeza mjumbe mwingine. Mjumbe mmoja aliongeza pia kuwa mitihani ilikuwa na misamiati migumu na hata kuwasumbua walimu walioisahihisha.
Hali hii inaweza kuwa imechangia, kwa kiasi kikubwa, kuongeza ugumu wa mitihani hiyo na hili linaweza kuchangia wanafunzi kushindwa kuelewa vizuri maswali wanayoulizwa kwenye mitihani. Wajumbe wa tume hiyo walieleza hali hiyo imefanya imani kujengeka kuwa mitihani ya Tanzania ni migumu kuliko ya nchi nyingine.
mwananchi.co.tz

mwanafunzi achalazwa viboko zaidi ya 100

Mwanafunzi wa shule ya sekondari Idodi wilayani Iringa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa madai ya kupigwa viboko zaidi ya 100 na mtu anayedaiwa kuwa ni mwalimu wa shule hiyo na kufungiwa katika bweni kwa siku 3 ili kuificha siri hiyo.
Tukio hilo linakuja wakati harakati mbalimbali za kijamii na asasi za kiraia zikipiga kelele kupinga vitendo vya ukatili wakati jeshi la Polisi likianzisha dawati la jinsia kwa ajili ya kutokomeza masuala hayo.
Ni mwanafunzi Lusinde Nyaulingo, wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Idodi, ambaye anaugulia maumivu makali katika Hospitali hii ya rufaa ya mkoa wa Iringa, word namba tano ya majeruhi, kutokana na ukatili uliosababisha majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake, hasa maeneo ya mapaja, makalio na mgongo, baada ya kupigwa kwa tuhuma za kuchukua simu ya mwanafunzo mwenzie, jambo linalomfanya mwanafunzi huyu apoteze muda mwingi wa masomo wakati akipatiwa matibabu ili kurudisha afya yake.
Lusinde anasema baada ya kuangushiwa kipigo hicho kikali, kilichodumu kwa zaidi ya masaa tatatu, alipoteza fahamu na kisha kufungiwa katika bweni kwa siku tatu, huku wanafunzi wenzie wakipigwa marufuku kufikisha taarifa ya ugonjwa kwa wazazi wa Lusinde.
Hata hivyo jeshi la polisi kupitia kamanda wake mkoa wa Iringa ACP Athmani Mungi limesema kuwa wanafuatilia tukio hilo ili kuhakikisha haki inatendeka, kwa kumchukulia hatua za kisheria mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kumfikisha Mahakamani. 
http://bongoleotz.blogspot.com

Jumatano, 23 Oktoba 2013

ripoti ya tume ya Pinda ni kitendawili haionekani




Tumeghadhabishwa na hatua ya Serikali ya kuendelea kuficha Ripoti ya Tume ya Kuchunguza Matokeo ya Kidato cha Nne iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda mapema mwaka huu. Tunasema hivyo kutokana na ukweli kwamba Tume hiyo iliundwa ikiwa ni hatua ya dharura kwa lengo la kutoa majibu ya haraka kuhusu sababu za wanafunzi wengi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana kufanya vibaya katika mtihani huo na kuamsha vilio kote nchini.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,903 sawa na asilimia 60.6 waliambulia sifuri, wakati watahiniwa 23,520 ambao ni asilimia 5.16 wakiwa wamefaulu, huku watahiniwa wengine 103,327 sawa na asilimia 26.02 wakiwa wamepata daraja la nne. Katika mtihani huo, watahiniwa 397,136 walitoka katika shule mbalimbali, huku wengine 68,806 wakiwa wa kujitegemea.
Idadi kubwa ya wanafunzi hao kufeli mitihani kiasi hicho lilionekana kama janga la kitaifa na ndiyo maana wananchi wa rika zote, wakiwamo wabunge walipaza sauti wakiishinikiza Serikali itegue kitendawili kuhusu sababu za matokeo hayo ya kutia fedheha na aibu kwa taifa letu. Ndipo Serikali ilipounda Tume ya watu 15 Machi mwaka jana na kuitaka kuwasilisha ripoti yake serikalini miezi mitatu baadaye.
Tume hiyo ilimaliza kazi yake katika muda uliopangwa na kukabidhi ripoti hiyo Juni 15, mwaka huu. Jambo la kushangaza ni kuwa, pamoja na kupita zaidi ya miezi minne tangu ripoti hiyo iwasilishwe serikalini bado Serikali imeificha makabatini kwa sababu inazozijua yenyewe. Habari zinasema kwamba Serikali inajua umuhimu wa kuitoa ripoti hiyo hadharani haraka, lakini inasita kwa sababu mengi ya matatizo yaliyoainishwa na Tume hiyo yanaonyesha bayana kwamba Serikali pia ni sehemu ya tatizo.
Hata hivyo, tunapata shida kuelewa kwa nini Serikali inaendelea kuatamia ripoti hiyo wakati ikijua kwamba Watanzania wanasubiri ripoti hiyo kwa shauku kubwa kwa mategemeo kuwa, hatua za kurekebisha makosa yaliyotokea zingechukuliwa na mamlaka zote husika kwa kuwa muda siyo mrefu wanafunzi watafanya tena mitihani ya kidato cha nne mwaka huu.
Ukimya wa Serikali unaendelea kusababisha madhara mengine kadhaa, kwa maana ya baadhi ya wajumbe wa Tume hiyo kuchoka kuisubiri Serikali iweke hadharani ripoti ya Tume hiyo. Jana gazeti hili lilichapisha habari kuhusu baadhi ya vipengere vilivyo katika ripoti ya Tume hiyo, ambapo baadhi ya wajumbe waliounda Tume hiyo walisema katika nyakati tofauti hivi karibuni kwamba waligundua mambo mengi yanayodhihirisha udhaifu mkubwa katika uendeshaji wa sekta ya elimu hapa nchini.
Hata hivyo, baadhi ya wajumbe wanasema sehemu kubwa ya matokeo ya uchunguzi huo inajikita zaidi katika kulaumu Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), badala ya kujielekeza zaidi katika kupendekeza nini kifanyike ili kurekebisha mfumo mzima wa sekta ya elimu nchini ambao umedhihirika kuwa mbovu. Tatizo hapa pengine ni muundo wa Tume hiyo yenye idadi kubwa ya watumishi wa umma na wabunge wa chama tawala.
Wajumbe hao wamesema ripoti ya Tume hiyo ni ndefu na ingefaa Serikali iiweke wazi sasa ili ifanyiwe kazi. Sisi tunaungana na wajumbe hao kuishauri Serikali kufanya hivyo sasa. Madhara ya kuendelea kuihodhi ripoti hiyo ni makubwa pengine kuliko Serikali yenyewe inavyofikiri.

souce . mwananchi

Ijumaa, 18 Oktoba 2013

wizara ya elimu na mchakato wa upangaji wa alama za maendeleo ya wanafunzi sekondari

Ikiwa yamebaki majuma machache wanafunzi wa kidato cha nne waanze mtihani wa wa taifa, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iko kwenye mchakato wa kubadilisha mfumo wa upangaji za mitihani ya sekondari na matumizi wa alama za maendeleo ya mwanafunzi (Continuous Assessment (CA). Mfumo huo ambao unatarajiwa kuanza kutumika kwenye Mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka huu, unakuja ikiwa ni miezi michache tangu Tume ya Waziri Mkuu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kufeli kwa maelfu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2012.
Akizungumzia mchakato huo, Kamishna wa Elimu Profesa Eustella Bhalalusesa alisema kwamba hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu na kuwa haina uhusiano na taarifa ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu ambayo mpaka sasa haijawekwa hadharani.
“Mambo yanakwenda yanabadilika hata binadamu yeyote anabadilika kila siku, mfumo unaotumika sasa hivi ni wa siku nyingi,” alisema.Alisema kuwa, ili kuweza kuboresha vyema mfumo huo wameshirikisha wadau mbalimbali zikiwamo shule za sekondari.
“Kama unataka kuboresha lazima upate maoni, lengo letu ni kushirikisha shule zote za sekondari za Tanzania, ila siwezi kukuhakikishia kama zote zitashiriki kwa kuwa tunawatumia zaidi maofisa elimu mkoa na wilaya. Tumeweka pia dodoso kwenye mdandao ili watu zaidi washiriki.
Kuhusu tume ya Pinda hapa haihusiki kabisa, ile ilikuwa na mambo yake, hata bila ile tume sisi hii tungefanya tu,” alisema Profesa Bhalalusesa. Alisema kuwa, mpaka sasa wameshapokea zaidi ya asilimia 60 ya maoni hayo kutokana na lengo walilo jiwekea.
Dodoso hilo ambalo pia Mwananchi imefanikiwa kuliona, linasema kuwa serikali inakusanya maoni ya wadau wa elimu kuhusu Upangaji wa Viwango vya Alama (Grade Ranges) katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na cha sita pamoja na matumizi ya ‘Alama Endelevu ya Mwanafunzi [Continuous Assessment (CA)].
“Serikali imeamua kukusanya maoni haya kwa sababu kwa muda mrefu sasa upangaji wa viwango vya alama vinavyotumika katika mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na kidato cha sita havifanani pamoja na kwamba mitihani hiyo yote ni ya elimu ya sekondari.Pia mfumo wa elimu ya sekondari umekuwa na miundo tofauti ikiwemo ule unaotumika shuleni na ule wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),” sehemu ya dodoso inasema.
Dodoso hilo linafafanua kuwa, muundo wa kwanza ni ule wa shule ambao alama mgando (Fixed Grade Ranges) ambao alama zinazotumika kupanga madaraja: A = 81 – 100; B = 61 – 80; C = 41 – 60; D = 21 – 40 na F = 0 – 20. Muundo wa pili ulioidhinishwa kutumiwa na Necta kuanzia mwaka 2012 ni Upangaji wa Alama Mgando usiobadilika (Fixed Grade Range).Kwa kidato cha nne alama zilizotumika ni A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49 na F = 0 – 34.
Kwa upande wa kidato cha sita alama zilizotumika ni A = 80 – 100; B = 75 - 79; C = 65 – 74; D = 55 – 64; E = 45 – 54; S = 40 – 44 na F = 0 – 39. Kwa mujibu wa dodoso hilo, alama zinazopendekezwa ni A = 81 – 100, B = 61 – 80, C = 41 – 60, D = 21 – 40 naF = 0 - 20.
Utaratibu mwingine ambao washiriki wanapaswa kuchagua ni A = 80 – 100, B = 65 – 79, C = 50 – 64, D = 35 – 49 na F = 0 – 34 huku utaratibu wa tatu ukiwa A+ = 91 – 100, A = 81 – 90, B+ = 71 - 80, B = 61 - 70, C+ = 51 – 60, C = 41 – 50, D+= 31 – 40, D = 21 – 30, E = 11 – 20 na U = 0 – 10.
Akisoma Kauli ya Serikali Bungeni kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wiliam Lukuvi alisema kuwa matokeo yaliyotangazwa awali na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yafutwe na yapangwe tena kwa kutumia mfumo uliobadilika mwaka 2011 kama ilivyopendekeza tume ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Hata hivyo, baada ya kufutwa kwa matokeo hayo na kupangwa upya, Waziri wa Elimu Dk Shukuru Kawambwa alisema kuwa utaratibu uliotumika kupanga matokeo hayo mapya ni uleule uliotumika kuandaa matokeo yaliyofutwa wa Fixed Grade Ranges.
“Kuanzia sasa matokeo ya mtihani ya kidato cha nne na sita yatachakatwa kwa kutumia Fixed Grade Ranges na Standardization (alama zisizobadilika na kuuwisha alama za mitihani),” alisema Kawambwa.
chanzo.Mwananchi.co.tz

Jumatatu, 14 Oktoba 2013

mshahara wa Rais milioni 32 kwa mwezi

 

Igunga. Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe amesema sababu ya kutaja mishahara ya viongozi wakuu wa nchi ni kuzuia mianya ya watu wachache kuiibia nchi kutokana na usiri wa jambo hilo.
Zitto alitoa kauli hiyo jana mjini Igunga, wakati akitangaza mshahara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa Zitto, kwa mwaka kiongozi huyo wa nchi analipwa Sh384 milioni ambazo ni wastani wa Sh32 milioni kwa mwezi bila kukatwa kodi.
Hatua ya Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), kutaja mshahara wa rais inakuja wiki moja baada ya kutaja mshahara wa Waziri mkuu kuwa ni Sh26 milioni kwa mwezi pasipo kukatwa kodi
Zitto alisema hoja ya msingi si kiasi wanancholipwa viongozi hao walioajiriwa na wananchi bali ni usiri unaofanywa juu ya kiwango hicho. Alisemaha ni jambo la kusikitisha kuona mwalimu anayelipwa mshahara wa Sh200,000 kwa mwezi ukikatwa kodi huku viongozi wa kuchaguliwa wakiwa wanapokea mishahara mikubwa pasipo kukatwa kodi.
Alisema katiba ya sasa Ibara ya 43(1), inaeleza kuwa rais atalipwa mshahara na malipo mengine huku ibara hiyo hiyo kifungu cha pili ikizuia mshahara na marupu rupu kupunguzwa, hali aliyoelezea kuwa ni muhimu katiba mpya ikabadilisha sheria hizo kwa manufaa ya nchi.
“Kwa hiyo hata kesho kama Dk Slaa akiwa Rais na akataka kupunguza mshahara wake kwa katiba hii hawezi na hili jambo si sahihi kwani viongozi wa ngazi hizi wanapata kila kitu bure kutoka Serikalini,” alisema Zitto.
Zitto alisema kuwa kitendo cha Serikali kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania, hakikuzingatiwa kulingana na uwazi uliowekwa kwa kuandika uwazi wa viwango vya mishahara.
Alisema kuwa waziri aliyehusika kufunguia magazeti hayo hakufikiria kwa makini kutokana na kuwa na uelewa mdogo na kuongeza kuwa hakuna kosa lolote linalopelekea kufungiwa magazeti hayo kutokana na ukweli ulioandikwa.

chanzo. mwananchi.com

Serikali yashauriwa kuruhusu walimu wa jumuiya ya Afrika Mashariki ili kukabiliana na upungufu wa walimu

Serikali  imeshauriwa kufungua milango kwa walimu wanaotoka katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kufanya kazi nchini kwa masharti nafuu.

Hali hiyo imeelezwa kuwa itachagiza kasi ya kukabiliana na upungufu wa walimu uliopo nchini na  hivyo kuboresha sekta ya elimu.

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Brilliant ya jijini Dar es Salaam, Jasson Rweikiza, aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya tatu ya shule hiyo.

Rweikiza ambaye pia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), alisema pamoja na jitihada za uboreshaji wa elimu nchini, bado uhaba wa walimu umekuwa tatizo sugu linalokwamisha azma hiyo.

 “Tunaweza kuboresha mazingira yote katika sekta ya elimu, lakini kama hatutakuwa na walimu wa kutosha, ni dhahiri kwamba ufundishaji utakwama na azma ya kupata matokeo bora ya wanafunzi haitafikiwa,” alisema.  Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Mbunge wa Sengerema (CCM), William Ngeleja.

Rweikiza alisema mazingira yaliyopo sasa yanakabiliwa na vikwazo katika kupata vibali kwa walimu hasa wanaotoka nchi za EAC kufanya kazi nchini.  Kwa mujibu wa Rweikiza, gharama za kibali kwa mwalimu mmoja kutoka nje, zinakadiriwa kufikia Shilingi milioni mbili.

Akizungumza katika halfa hiyo, Ngereja, pamoja na mambo mengine alisema wakati umefika kwa serikali kutilia mkazo namna bora za kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu.

Alisema changamoto hizo ikiwamo wa ukosefu wa walimu, zinakwamisha ama kurudisha nyuma jitihada za maendeleo ya nchi na raia wake.

Alitoa mfano kuwa hata ufanisi katika kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) utapatikana ikiwa sekta ya elimu itaboreshwa na kuwezesha kupatikana kwa wataalam.

ippmedia.com

Jumapili, 13 Oktoba 2013

je kuna athari za kumrusha mtoto madarasa

Kuna wazazi (wakishirikiana na walimu) hurusha watoto wao madarasa (mfano anamaliza darasa la 3 anarushwa kuendelea na la 5)

- Je, unadhani ni kuna athari yoyote (kielimu, mahusiano yake na wanafunzi wenzake au kisaikolojia)?
- Unadhani kuna faida kufanya hivi?




Jana nilipeleka kijana kufanya mtihani wa kuanza kidato cha kwanza, wakati niko pale kukawa na akina mama wengine. Katika maongezi mama mmoja akasema kaleta binti yake wa darasa la sita kufanya mtihani huo, akifaulu anaruka la saba na kuanza kidato cha kwanza.

Na kuwa wakati, kuna mama mmoja tunafanya naye kazi alimrusha binti yake toka darasa la tatu na kuingia la tano, maana yake hakusoma darasa la nne kabisa.

Sasa mie nataka kujua kutoka kwa wadau.

  1. Unapomrusha mtoto darasa hakuna hasara yeyote? iwe kielimu, mahusiano yake na wanafunzi wenzie na saikolijia nzima ya mtoto(Ukizingatia mchana na usiku anakula ugali-kuna sred niliona mtu kasema ugali unasababisha mtu awe kilaza)
  2. Kuna faida yeyote kurusha mtoto darasa?
souce. jamii forums
Kuna wazazi (wakishirikiana na walimu) hurusha watoto wao madarasa (mfano anamaliza darasa la 3 anarushwa kuendelea na la 5)

- Je, unadhani ni kuna athari yoyote (kielimu, mahusiano yake na wanafunzi wenzake au kisaikolojia)?
- Unadhani kuna faida kufanya hivi?

Fuatilia mjadala huu => http://bit.ly/1gz2VIm


Jumamosi, 12 Oktoba 2013

DAWATI NI ELIMU

The "Dawati ni Elimu"” charity walk was held on 12 October from Mnazi Mmoja to Bunge Primary School led by the first lady of United republic of Tanzania Mama Salma Kikwete.
“The First of its kind mayoral ball aims to raise TZS 4.98 Billion towards providing 30,487 desks to primary and secondary schools in Ilala Municipality by end of financial year 2013/14. 100% of all funds shall proceeds towards realization of this project.
Dawati Ni Elimu is a project by Hon Jerry Silaa, Mayor of Ilala Municipal council toward the build up of the annual Mayors ball.
The Charity walk was sponsored by TSN Group, Eventlites, Continental Outdoor, A1outdoor and Vodacom and Managed by 361 degrees.
ABOUT DAWATI Ni ELIMU.

DAWATI Ni ELIMU is a project towards the Mayors ball that aims to solve the issue of shortage of desks in primary and secondary schools in Ilala municipality where by currently there is a lack of 30,487 desks. The project is an initiative under the office of the mayor of Ilala Municipal Council, this project seeks to raise a sum of 4.98 Billion Tanzanian shillings with the emphasis that the society can contribute and make change to solve the challenges by calling upon organisation and individuals to contribute to this noble cause.
 

Sasa kwa nini elimu ikumbwe na ufisadi hivi?


Ufisadi shuleni haukumbi tu Afrika bali Ulaya pia kuna tatizo hilo
Ufisadi katika sekta ya elimu, ni tatizo sugu na bila shaka unahujumu hadhi ya elimu na uwepo wa shule na vyuo vikuu kote duniani . Hii ni kwa mujibu wa taarifa za ripoti ya kimataifa.
Shirika la kimataifa la Transparency International limechapisha utafiti unaoonyesha kuwa mwanafunzi mmoja katika kila wanafunzi sita, alilazimika kulipa rushwa ili apokee huduma za elimu.
Katika baadhi ya sehemu za Kusini mwa jangwa la Sahara na barani Asia, ufisadi unaowalazimisha wazazi kulipa kiwango kidogo cha pesa kwa nafasi ya shule ambayo alipaswa kuipata bila malipo.
Nako barani Ulaya hasa Mashariki mwa Ulaya, watu wanalazimika kulipa rushwa ili waweze kupata nafasi katika chuo kikuu.
Shirika hilo la mjini Berlin linalojulikana , kwa kuchunguza viwango vya pesa zinazotozwa kwa njia isiyo halali katika zaidi ya nchi 100, ilizingatia zaidi ya nyumba
114,000 kwa mahojiano.
Katika baadhi ya nchi ripoti hiyo inasema kuwa karibu thuluthi tatu ya watu nchini Cameroon na Urusi, wanaona mfumo wao wa elimu kama uliokumbwa na ufisadi si haba.
Hali halisi za shule barani Afrika
Nchini Urusi ufisadi umekithiri katika mfumo wake wa elimu
Madai ya ufisadi yalichocheza maandamano ya walimu nchini Brazil.
Matokeo ya utafiti yanaonyesha viwango vya juu sana vya rushwa katika sekta ya elimu.
Na nchini Pakistan, kulikuwa na onyo la maelfu ya shule hewa bila ya wanafunzi ingawa zilikuwa zinazopokea ufadhili wa kuwalipa walimu hewa.
Mapengo katika sekta ya elimu Kenya yalisababisha kupoteza kwa vitabu milioni 11. Nachini Tanzania , katika utafiti wa shule 180, iligunduliwa kuwa ufadhili haukuwafikia wanafunzi na shule husika.
Nchini Ugiriki, kulikuwa na tatizo la mapendeleo katika kutoa nafasi za kazi na watu kupandishwa cheo katika vyo vikuu.

Sasa kwa nini elimu ikumbwe na ufisadi hivi?

Wazazi wanawataka watoto wao wapate elimu nzuri na wanaweza kuhadaiwa na maafisa wanaodhibiti mifumo ya elimu hasa katika mataifa ya kiafrika ambako nafasi zaidi zinahitajika za watoto kusoma.
Nchini Nigeria dola milioni 21 zilipotea kwa miaka miwili
Pia yote haya yanahusu pesa nyingi za serikali zinazotolewa kwa shule za serikali. Nchini Nigeria ripoti hiyo imesema kuwa dola milioni 21 za kimarekani zilizonuiwa kwa matumizi ya shule, zilipotea kwa kipindi cha miaka miwili.
Lakini ni tatizo tu kwa mataifa yanayostawi au wale wanaotoa huduma muhimu za shule.
Hitaji la nafasi nyingi kusoma katika vyuo vikuu pia imekuwa fursa kwa watu kujipatia pesa nyingi sana kwa kutoza ada zisizohitajika.
Kutokana na pesa nyingi zinazohitajika, watu wanalazimika kununua hati bandia za kuonyesha kuwa wamefuzu shahada na tatizo hilo liko nchini Marekani na pia katika mataifa ya kiafrika ikiwemo Kenya.
Shirika la kimataifa la Transparency International linasema kuwa ufisadi umeathiri pakubwa elimu na hata kushusha hadhi ya elimu wanayopokea wanafunzi siku hizi kote duniani.
Hata hivyo kuna habari njema kwenye ripoti hiy: juhudi za kupambana na uifisadi shuleni.
Nchini Chile mafunzo ya kupambana na rushwa yamejumlishwa kwenye mtaala wa shule na nchini Bangladesh walimu hulazimika kuapa kuwa na maadili mema.
Kuwepo kwa simu za mkononi pia kumesaidia watu kuweza kuripoti visa vya ufisadi shuleni.
Pia kuna juhudi za kimataifa kuchunguza matumizi ya pesa za shule.
Lakini ufisadi ungali unaathiri sana bajeti za shule.

chanzo. bbcswahili.com

Jumatano, 9 Oktoba 2013

Mishahara ya viongozi tunaowachagua ni changamoto kupatikana kwa elimu ya bure nchini



HATIMAYE Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe, ameweka wazi mshahara wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

Zitto ameutaja mshahara huo wa Pinda anayejitambulisha kama ‘mtoto wa mkulima’ juzi mjini Mpanda na jana wilayani Sikonge wakati akihutubia mikutano ya hadhara katika ziara ya Kanda ya Magharibi kwa ajili ya ujenzi wa chama.

Alisema Pinda anapokea jumla ya sh milioni 26, ambazo ni kiasi kikubwa kulinganisha na uchumi wa nchi.

Akichanganua alisema Pinda anapokea sh mil. 11.2 kama mbunge, sh mil. 8 kwa nafasi ya waziri na kiasi kinachosalia kufikia sh mil. 26 kwa nafasi yake ya uwaziri mkuu.

Alisema sababu hiyo ya mishahara mikubwa isiyokatwa kodi ndiyo huwafanya viongozi wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa wakali pale vyombo vya habari vinapotaka kuwafahamisha wananchi namna watumishi wao wanavyojilipa.

“Nimeanza na mshahara wa waziri mkuu pia siku zijazo nitataja na wa rais, kwa kuwa amesaini makubaliano na Serikali ya Marekani kuendesha nchi kwa uwazi, na moja ya uwazi ni kwa muajiri kujua kiasi anachomlipa mwajiriwa wake,” alisema Zitto.

Hatua ya Zitto imekuja baada ya kuwapo mvutano mkubwa kuhusiana na kile kinachodaiwa ‘usiri’ wa mishahara ya watumishi wa umma, wakati ni haki ya walipa kodi kujua kile wanachowalipa walioomba kuwaongoza.

Kodi ya laini za simu

Akizungumzia sakata la kodi katika laini za simu, Zitto alisema CCM ina ajenda ya kisiasa kwa ajili ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Alisema serikali baada ya kubaini watu wengi wanapeana taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi, hususan katika masuala ya kisiasa, wakaona njia sahihi ya kudhibiti ni kuwatoza kodi ya laini ili kupunguza hatari ya mawasiliano hayo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.

“Sikuwepo bungeni wakati wabunge wa CCM wanapitisha kadhia hiyo ya kuwanyonya wananchi, wenzangu wakaniambai tukasema hapana, kwa maana tuliona hii leo kuna Watanzania wengi wasio na uwezo wa kuhudumia simu kwa kiasi cha sh 1,000 kwa mwezi,” alisema Zitto.

Akijibu maswali ya wananchi mjini Mpanda waliotaka kujua sababu ya kupunguza makali bungeni, Zitto alisema hakuna makali yaliyopungua bali ni mitazamo ya watu.

Alisema kwa kushirikiana na wabunge wenzake wa upinzani wamekuwa wakisimamia hoja zenye manufaa kwa wananachi huku wabunge wanaojipambanua kuwa majasiri kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwaunga mkono wazi wazi.

Akiwa wilayani Sikonge, Zitto alisema Watanzania hawawezi kujivunia uhuru huku mama zao, watoto wao na wazee wao wakiwa hawana uhakika wa kupata huduma bora ya afya, elimu na maji safi.

Alisema kwa sasa Tanzania ni taifa moja lililogawanyika katika nchi mbili za wenye fedha na wasio na fedha.

Alisema nchi ya wenye fedha, familia zao husoma katika shule bora, zenye mazingira bora na walimu wazuri, hutibiwa katika hospitali zenye hadhi na huduma muhimu na ikibidi nje ya nchi, huku nchi ya wasio na fedha familia zao wakiishi kwa shida, kusoma katika majengo ya shule na walimu wasiopata mishahara ya kuridhisha na hospitali zisizokuwa na huduma muhimu licha ya kuchangia kiasi cha fedha kwa ajili ya bima ya afya.

(chanzo Tanzania daima)