Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Alhamisi, 6 Juni 2013

Marafiki wakijadili changamoto

Marafiki wa elimu wakijadiliana chini ya uongozi wa Mwalimu byabato mwenye suti ya kijivu toka Serengeti  pembeni yake ni rafiki wa elimu Nice Benedictor mwenye nguo nyekundu

Wafahamu marafiki wa elimu wanakikundi wa (SAUTI ZETU CLUB)

kutoka kushoto ni bi. Perus Masokomya mwenyekiti wa serikali ya mtaa kigera na mlezi wa kikundi cha marafiki wa elimu cha Sauti zetu club anaefuatia ni James Mwita Mboyi katibu wa marafiki wa elimu wa 3 ni Masoud jeremia  wa 4 ni Juma Richard Okumu mwenyekiti wa marafiki wa elimu musoma mwingine ni Hamisi Odemba toka kijiji cha Bisumwa wilaya ya Butiama na wa mwisho ni Japhet toka shirika la ABC