Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatatu, 22 Julai 2013

ELIMU YA AWALI NI JUKUMU LETU SOTE KUIBORESHA

Mmoja wa wadau akiwa na bango linalohamasisha kampeni ya boresha chekechea
 PICHA ZIKIWAONYESHA WADAU WA ELIMU WAKIWA KATIKA KAMPENI YA BORESHA CHEKECHEA
Kina dada hawa wakionekana na mabango yao wakihamasisha elimu bora ya chekechea

Alhamisi, 18 Julai 2013

MBUNGE WA MUSOMA MJINI VINCENT NYERERE AELEZA MAFANIKIO ALIYOFIKIA KWA UPANDE WA ELIMU

Mbunge wa Musoma Mjini Vincent Nyerere akiwa na rafiki wa elimu Juma Richard Radio Victoria Fm
Mapema hii leo katika kipindi cha radio kinachorushwa na marafiki wa elimu musoma Radio victoria fm ya mjini musoma, Mbunge wa jimbo la musoma mjini Mheshimiwa Vincent Nyerere ameeleza  yale anayoyafanya kama kiongozi wa wananchi kuhakikisha anaboresha elimu katika jimbo lake.

katika mada iliyokuwa inasema  VIONGOZI TUNAOWACHAGUA WANAJITOLEA KUBORESHA ELIMU?
Mbunge Nyerere anasema katika kipindi chake cha uongozi amefanikiwa kujenga maabara ya kisasa kwa pesa kidogo ya mfuko wa jimbo anayopata,amesema kwa mwaka anapokea kiasi cha milioni 17 mara 2 na amefanikiwa kujenga maabara yenye thamani ya shilingi milioni 68 amefanikiwa kupata kontena la vitabu lenye urefu wa futi 20 na kuvigawa mashuleni.
pia mbunge huyo anasema kwa jitihada zake pamoja na chama chake wamefanikiwa kutoa madawati kwa shule za chekechea na wametangaza tenda ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi jimbo la musoma mjini.
katika shukurani zake mbunge Nyerere kalipongeza shirika la Haki Elimu kwa kufanikisha ujenzi wa maktaba ya kisasa katika shule ya msingi mwisenge na kuahidi kuendeleza ushirikiano na marafiki wa elimu kuhakikisha kiwango cha elimu kinaimarika jimbo la musoma mjini.

Vincent Nyerere  ni moja ya viongozi wanaoonesha nia ya kuboresha elimu!  je kiongozi wako anawajibika kuboresha elimu?

Jumatano, 17 Julai 2013

BAADHI YA SHULE MKOANI MARA ZAKOSA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO




Machungu ya matokeo mabovu ya kidato cha nne 2012 yanaanza kuonekana bayana. Kama ilivyotarajiwa, wanafunzi waliokuwa wamefaulu vizuri walikuwa wachache-kiasi kwamba wasingetosheleza mahitaji ya wanaotakiwa kujiunga na kidato cha 5. Mpaka sasa, shule binafsi saba za sekondari Mkoa wa Mara zimetangaza rasmi kuwa mwaka huu hazitaweza kuwa na wanafunzi wa kidato cha tano. Shule hizo ni:

Makoko Semonary, Kowaki Girls, JK Bukanga, Isenye, Kibara, Ellys na Busegwe.

Hizi ni baadhi tu ya shule zilizotoa taarifa rasmi. Hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Baadhi ya shule zimefuta combination kadhaa-kutokana na kukosa wanafunzi. Hali hii iturejeshe kwenye hatua madhubuti za kuchukua ili wanafunzi walioko shuleni sasa wapate kilicho bora zaidi katika kujifunza na kujiandaa kwao. Wakiandaliwa vizuri, watafaulu vizuri-na miaka ijayo tukaondokana na tatizo hili la kukosa wanafunzi. Hata hivyo, ni heri kukosa wanafunzi wenye sifa kuliko kung'ang'ania kushusha alama za ufaulu ili tuwapate wengi wakajaze nafasi. Watanzania tuvumilie hali hii-ila tuendelee kushikamana kudai kilicho bora zaidi kwa watoto wetu na elimu yetu.

Jumatatu, 8 Julai 2013

TUKIWEKEZA KWENYE ELIMU YA MEMKWA TUTAFANIKIWA

Watanzania tunaiona elimu ya MEMKWA  kama haina msaada kabisa kwetu lakini ifike mahali tukumbuke kwamba mwalimu Nyerere alipigana kufa na kupona kuhakikisha tunafuta ujinga nchini na mbinu kubwa aliyotumia ni kuhakikisha walikosa elimu wanapata elimu bila kujali umri wao na akafanikiwa kwa kiwango kikubwa sana.
tofauti iliyopo sasa serikali na wanajamii hawaichukulii elimu hiyo kama ukombozi wa kututoa kwenye ujinga tena na mwisho wa siku tunaendelea kuzalisha taifa la wasiojua kusoma na kuandika
kwa pamoja tupaze sauti na kusema  TUKIWEKEZA KWENYE ELIMU YA MEMKWA TUTAFUTA UJINGA NCHINI

Jumapili, 7 Julai 2013

DONDOO ZA BAJETI YA TAIFA 2013/2014



1. Bajeti nzima ni Trilioni 18.2; ambapo Trilioni 11.1 sawa na 61% zitakusanywa kutoka kwenye mapato ya ndani (GBS itakuwa ni Trilioni 1.16, pia wafadhili watatoa Trilioni 2.7 ni misaada na mikopo kwa ajili ya miradi ya maendeleo)
2. Trilioni 5.7 zitatumika kwenye shughuli za maendeleo (ambapo Trilioni 2.7 zitatoka kwa wahisani; na Trilioni 3 zitatoka kwenye vyanzo vya ndani)
3. Matumizi ya kawaida ni Trilioni 12.5 (Trilioni 4.8 zitatumika kulipa mishahara na stahili za wafanyakazi; mfuko mkuu wa serikali umetengewa Trilioni 3.3 (kupunguza deni la Taifa) na matumizi mengineyo yatachukua Trilioni 4.5
4. Vipaumbele vya bajeti ni: Miundombinu, Kilimo, Viwanda, Raslimali-watu, Utalii na Huduma za jamii
5. Deni la Taifa lafikia Trilioni 21
6. Kodi ya sigara, soda na bia imeongezeka kwa asilimia 10
7. Nia ya serikali ni kukuza pato la Taifa kufikia 7.2% mwakani (toka 7.0% mwaka huu); pia kudhibiti mfumuko wa bei toka 8.3% sasa na kufikia 6% mwakani
8. Kodi ya mishahara(PAYE) kupungua kwa asilimia 1; toka 14% na kuwa 13%
9. Kodi ya Mafunzo (Skill Development Levy) imepungua toka asilimia 6 mpaka 5
10. Watumiaji wa simu kutozwa 14.5% (ambapo asilimia 2.5 ya pesa hizo zitagharimia elimu)
11. Kutakuwepo na tozo mpya ya mafuta ya petrol y ash 50 kwa lita kugharimia umeme vijijini
12. 10% itatozwa kama kodi kwenye commission ya kusafirisha fedha kwa njia ya simu za mikononi
13. Ongezeko la mishahara kwa wafanyakazi? KIMYA
14. Waziri hakuzungumza kuhusu bajeti ya elimu itakuwa kiasi gani (alijikita zaidi kwenye maeneo yaliyofanyiwa marekebisho baada ya bajeti za wizara mbalimbali kujadiliwa-la orodha ya vipaumbele aliyoitoa..hivyo-itakuwa inafanana na kiasi kilichopitishwa kwenye bajeti ya elimu cha shilingi bilioni 689.7 (bilioni 98.7 ni matumizi ya kawaida ya idara; bilioni 72.6 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo; na bilioni 518.4 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya taasisi (zikiwemo bilioni 306 za mikopo ya elimu ya juu). Pia tukumbuke kwamba sehemu nyingine ya pesa za elimu ziko TAMISEMI