Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumanne, 26 Februari 2013

Choo cha shule ya msingi Kigera A na B

Hiki ndicho choo cha shule ya msingi kigera chenye jumla ya matundu 6 pamoja na choo cha walimu shule hii ina wanafunzi zaidi ya 500 ambaye imegawanywa kigera A na B kwa hali hii bado haiendani na sera ya elimu 

ni wakati wa wazazi na wanajamii kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha wanaendeleza miundo mbinu ya shule zao na si kuachia serikali pekee