Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumamosi, 16 Machi 2013

Marafiki wa elimu katika picha tofauti

Marafiki wakimsikiliza kwa makini mwalimu Byabato toka serengeti

Mwalimu Byabato rafiki toka wilaya ya serengeti akielezea juu ya dhana ya marafiki wa elimu ni nini!

Rafiki wa elimu Anastazia Richard akijitambulisha katika mkutano wa marafiki wa elimu

Rafiki wa elimu akichangia mada katika mkutano wa marafiki wa elimu musoma

marafiki wa elimu wakijadiliana katika makundi juu ya mbinu za kuboresha elimu