Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumapili, 4 Agosti 2013

SERIKALI YA KENYA YASIKIA KILIO CHA WALIMU


Chama cha Taifa cha Walimu Kenya (KNUT) kimesimamisha mgomo uliopangwa kufanyika Alhamisi (tarehe 8 Agosti) baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuahidi kujadiliana kuhusu malipo ya mshahara wa Julai wa walimu walio katika mgomo, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti.

"Tumepata ahadi za Rais mwenyewe, na matokeo yake ni tumeufuta dhamira yetu ya kufanya mgomo sasa," alisema Katibu Mkuu wa KNUT Mudzo Nzili baada ya kukutana na Kenyatta Ijumaa jioni.

KNUT ilimaliza mgomo wa wiki nne tarehe 17 Julai, lakini ilitishia kurejea katika mgomo wakati Tume ya Utumishi wa Walimu iliposema walimu waliogoma hawatapata malipo ya Julai.

"Huku ni kujaribu kuwaadhibu walimu wanaoshiriki katika mgomo kama ilivyoelezwa katika katiba; sio haki," alisema kiongozi wa KNTU wa Kaunti ya Nyandarua Michael Chege.

Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi pia alitangaza siku ya Ijumaa kwamba serikali itatoa shilingi bilioni 3.9 (dola 45,000) kulipa mishahara ya wafanyakazi na wahadhiri wa chuo kikuu na posho za nyumba ili kuzuia mgomo mpya, Capital FM ya Kenya iliripoti.