Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Alhamisi, 18 Aprili 2013

Je viboko vinaashiria upatikanaji wa elimu bora?

picha kwa hisani ya islam mposso
 leo tuvizungumzie viboko na nafasi yake katika kuinua kiwango cha nidhamu ya wanafunzi na elimu mara nyingi tumekuwa tukiwasikia wazazi wakilaumu juu ya adhabu ya viboko kufutwa mashuleni. Tumewasikia pia walimu wakilalama sana na kudai kurejeshwa kwa viboko kwa upande wa wanafunzi wanafurahi na kusema viboko havina nafasi  kwao.

Je viboko ni sawa

katika maandiko matakatifu viboko vinaruhusiwa kama njia ya kuleta maadili kwa  mtoto.
Lakini pia ni muhimu kuangalia na kutambua jinsi ya kukitumia kiboko kumfunza mlengwa, Tanzania tuliendelea kuamini na mpaka sasa tunaamini kuwa kiboko ni njia ya kumfunza mtoto hii ni sawa kabisa.

picha kwa hisani ya Islam Mposso
Je kiboko kinasaidia

tukirudi nyuma miaka ya 2000 kurudi nyuma viboko mashuleni vilikuwa ni sehemu ya maisha ya shule.
lakini pia ukiangalia mazingira ya shule ya kipindi kile na sasa kulikuwa na tofauti kubwa sana, zamani suala la utoro kwa wanafunzi kilikuwa ni kitu cha kawaida sana na hii ilisababishwa na viboko. Lakini kwa wale waliyovumilia viboko walipata faida ya kupata elimu bora.

Hivi karibuni serikali imesema inatarajia kurejesha  adhabu ya viboko mashuleni
hapa napata mushkeli kidogo na sababu kubwa ni hali halisi jinsi ilivyo baada ya kupunguzwa kwa adhabu ya viboko mashuleni suala la utoro lilipungua kwa kiwango kikubwa sana na baadhi ya wanafunzi wakaanza kuyaona mazingira ya shule kuwa ni rafiki kwao.
Binafsi tunaamini suala si viboko suala la msingi ni kuboresha mitaala ya shule zetu. walimu kupewa mafunzo ya mara kwa mara kwa sababu mafunzo ya walimu ni wajibu wao na ni lazima wayapate ili kuendana na mabadiliko ya mitaala.
lakini pia tunapozungumzia kuongeza adhabu ya viboko mashuleni ni lazima tuwe tayali kukabiliana na ongezeko la utoro, kwa maana kwamba shule hakutakuwa mahali rafiki tena kwa wanafunzi. Lakini twapaswa pia kukubali kuwa nidhamu za wanafunzi wetu zimeshuka sana lakini hii si kutokana na viboko hii inatokana na wana jamii wenyewe kuamua kuwalea watoto wao pekee yao tofauti na malezi ya zamani ambayo mtoto alikuwa ni mali ya jamii na kila mwana jamii alikuwa na jukumu la kumsimamia mtoto wa mwenzake.
Lakini suala la viboko moja kwa moja linaingia kiafya tunapaswa kukubali kwamba watoto wa zamani walikuwa tofauti na watoto wa sasa , mtoto wa zamani aliweza kumudu fimbo zaidi ya kumi na kuendelea na masomo darasani lakini mtoto wa sasa akichapwa fimbo tano tu basi utaanza kuona mabadiliko katika mwili wake hili la kiafya halina uchunguzi zaidi lakini tunaweza kuamini kwamba miili yetu ya sasa si kama ya zamani huenda ni kutokana na vyakula tulavyo au mabadiliko ya kimazingira
marafiki wa elimu tunaamini kiboko kina nafasi ila nafasi ya mwisho kabisa kwani adhabu mbadala zipo za kutosha tunahitaji mitaala bora elimu itakuwa bora na si viboko