Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumapili, 10 Machi 2013

UMUHIMU WA ELIMU YA AWALI NA DARASA LA KWANZA ILIVYO SASA NA ZAMANI

Watanzania wenzetu tunapaswa kujiuliza juu ya elimu yetu ya darasa la awali na darasa la kwanza  miaka ya 80 mpaka 90 mwanafunzi wa darasa la kwanza alikuwa anafundishwa  masomo matatu tu yaani Kusoma,Kuhesabu na Kuandika.

nyakati hizo mwanafunzi wa darasa la kwanza alikuwa na uwezo mzuri wa kuweza kuandika mwandiko mzuri kusoma vizuri kwa kuungaunga  manene kama mama baba kaka nk.

pia waliweza kuhesabu moja mpaka mia vizuri kabisa 

waliweza kusoma hadithi fupi fupi vizuri japo kwa kusitasita lakini hali hiyo ilikuwa ikionyesha matumani kwamba wafikapo darasa la pili basi wangejimudu vizuri.

baada ya kuizungumzia elimu ya darasa la kwanza sasa niizungumzie elimu ya darasa la awali kabla hatujaiona hali ya elimu ya sasa ilivyo.

darasa la awali kwa kipindi hicho ilikuwa ni lazima kabla ya mwanafunzi kuingia darasa la kwanza hii ilikuwa inampa mwanafunzi uwezo wa awali wa kuyazoea mazingira ya shule kuzielewa stadi za awali na kuweza kujimudu aingiapo darasa la kwanza.

                        TANZANIA YA LEO

Mwanafunzi wa darasa la kwanza anafundishwa masomo manne hadi matano umuhimu wa elimu wa awali authaminiwi tena walimu wa kuwamudu wanafunzi wa madarasa ya awali na darasa la kwanza ni wachache sana .

Mwanafunzi wa darasa la kwanza hana tofauti hata kidogo na mwanafunzi wa darasa la awali hali hii upelekea watoto kusukumwa na kuamini kwamba wataelewa mbele kwa mbele lakini mara nyingi huko mbele tunapotegemea wataelewa tu ndipo tunapofika mahala ambapo hakuna mitihani ya kujipima tena .

na mwisho wa siku tunazalisha taifa la watoto wanaomaliza darsa la saba bila kujua kusoma wala kuandika

yatupasa kwa dhati ya mioyo yetu kuhakikisha kwamba mitaala haibadilikibadiliki wanafunzi wa darasa la kwanza wanajifunza kuandika kusoma na kuhesabu(kkk) na si kulundikiwa masomo mengi tofauti na uwezo wao hatuwezi kumfundisha mwanafunzi wa darasa la kwanza kiingereza wakati mazingira halisi ya anapotoka ni waswahili hucheza na watoto wa kiswahili masaa yote.

ni lazima tumfundishe stadi za awali kwanza tangu darasa la awali mpaka darsa la tatu na afikapo darsa la 3 ndipo aanze kuchanganyiwa masomo kwani hukuta sasa hata akili yake inaanza kupanuka 

NI JUKUMU LETU SOTE TUTAFAKARI KWA PAMOJA