Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatano, 8 Mei 2013

Idadi ya wanaoingia sekondari bila kujua kusoma na kuandika musoma mjini

Kutokana na changamoto mbalimbali za elimu marafiki wa elimu wameanza kufanya utafiti mdogo unaoonyesha hali ya elimu katika wilaya ya musoma mjini na changamoto zake,

katika harakati za kufanya utafiti huu marafiki wa elimu wameweza kubaini taarifa za ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba wanaojiunga na kidato cha kwanza bila kujua kusoma na kuandika.
Katika takwimu hizo zilizopatikana toka ofisi ya afisa elimu msingi na afisa elimu sekondari inabainisha kwamba kwa mwaka wa 2012 Wanafunzi waliomaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika walikuwa ni 3360.katika wilaya ya musoma mjni
hawa ni wale ambao walikuwa hawajui kabisa kusoma kuandika na kuhesabu lakini bado inabainishwa kwamba idadi inakadiliwa kufikia wanafunzi 7000 kwani inasemekana kuna baadhi yao waliyooneka hawajui kidogo kusoma.
 lakini waliyokuwa hawajui kabisa ndio 3360

Licha ya kuwa na takwimu ya kusikitisha kiasi hicho marafiki pia tulitaka kujua kwa mwaka huu wa 2013 ni wanafunzi wangapi waliyochaguliwa kwenda sekondari bila kujua kusoma na kuandika ambapo ofisi ya afisa elimu sekondari inasema kwa mwaka wa 2013 ni wanafunzi 8 pekee ndio waliyogundulika kuingia sekondari bila kujua kusoma na kuandika na hii takwimu inatokana na mitihani ya majaribio waliyopewa mara baada ya kujiunga na kidato cha kwanza.
na hakuna utafiti wa kina uliyofanyika kubaini kama wapo wasiojua kusoma na kuandika ambao wamemaliza darasa la saba na hawakuchaguliwa kwenda sekondari kama ilivyofanyika mwaka 2012 na inawezekana ikawa sababu kubwa ya kubainika wanafunzi 8 pekee.