Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumapili, 3 Machi 2013

ELIMU YETU INATUPELEKA MBELE AU INATURUDISHA NYUMA

 

Leo ni siku nyingine tena ambapo tunapaswa kujiuliza maswali mengi sana mioyoni mwetu 

tujiulize ni wapi tulipotoka

wapi tulipo na wapi tunapoelekea 

tulipotoka ni pale tulipopata uhuru wetu mwaka 1961 elimu kwa wengi ilikuwa haina umuhimu wengi hawakuelewa elimu inaweza kuyasaidia maisha ya mwanadamu kwa njia ipi 

juhudi za mwalimu Nyerere na uongozi wake uliwajengea watanzania moyo wa kujua elimu ni nini faida za elimu ni zipi ,baada ya juhudi hizi za viongozi tuliweza kuyaona mafanikio kwani hata wale waliyokuwa wanadharau elimu waliweza kuona umuhimu wake na kuanza kuijali elimu

huko ndipo tulipotoka.

Tulipo leo 

ni pahali ambapo kuna matabaka ya elimu wanaotakiwa waonyeshe njia ya kuthamini elimu hawana moyo huo tena maskini wengi wanaojua umuhimu wa elimu wanashindwa kuwezesha watoto wao kusoma na kufikia malengo yao tofauti na zamani ambapo elimu ilitolewa bure na jamii zote zilipata elimu kwa usawa lakini sasa kutokana na matabaka tuliyonayo nchini mwenye pesa mwanae anapata elimu bora na maskini mwanae anategemea kupata matokeo bora ya mitihani tu.

ifike mahali tuseme kwa sauti ya pamoja kwamba sote ni watanzania sote tunaishi katika nchi moja sote tupate elimu sawa ,afya sawa na mahitaji sawasawa katika elimu

Tunapoelekea 

kama hatutachukua hatua madhubuti tunalirudisha taifa mahali ambapo hakuna maskini atakaeijali elimu kama njia ya kumkwamua na mazingira magumu.

 kwani gharama za elimu zinazidi kuongezeka , ubora wa elimu haupo tena kwa mtoto wa maskini tumeona na tunaendelea kuona watoto wengi wa maskini wanaishia kidato cha nne lakini elimu aliyoipata haikumpa stadi za kukabiliana na ugumu wa maisha

 lakini watoto wa wenye pesa wamewezeshwa kupata elimu bora na mwisho wa siku watoto wa maskini uendelea kunyonywa na watoto waliyotoka kwenye familia zenye uwezo wa kifedha ,ajira hakuna kwa wanaoshidwa kidato cha nne wanaishia kuhangaika mabarabarani na bodaboda ,wanaishia kuwa vibaka kutokana na elimu duni waliyoipata

wazazi na walezi wa watoto maskini itafika pahali sasa hawatauona umuhimu wa elimu tena na tutaendelea kuzalisha taifa la watu wajinga wanaotawaliwa na wajanja wachache wenye pesa .

Hii ni Tanzania yetu sote lazima tuseme kwa pamoja

           ELIMU SAWA KWA WOTE