Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Jumatano, 28 Agosti 2013

watoto wadogo nchini tanzania wanafanya kazi migodini

Shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, limefichua ushahidi zaidi kuhusu unyanyazaji wa watoto nchini Tanzania, baadhi yao wenye umri wa miaka minane ambao wanafanya kazi kwa zamu, katika migodi ya madini iliyoko chini ya ardhi, kwa saa ishirini na nne.
Shirika hilo limesema watoto hao wanakabiliwa na tishio la kuvuta hewa ya sumu inayotokana na uchimbaji wa madini ya dhahabu na wakati mwingine kuuawa wakati migodi hiyo, inapoporomoka nyingi zikiwa hazina leseni.
Tanzania ina sheria kali inayozuia watoto kufanya kazi katika machimbo ya madini lakini shirika hilo limesema, serikali ya rais Jakaya Kikwete ni sharti iimarishe juhudi zake za kuhakikisha sheria hizo zimetekelezwa.

shule aliyosoma obama picha kutoka kwa rafiki wa elimu (jakarta)

Shule aliyosoma Obama Jakarta picha kwa hisani ya rafiki wa elimu boniventure godfrey

Jumamosi, 24 Agosti 2013

KUTOKA KWA MARAFIKI WA ELIMU DODOMA

Hiki ni kibao kinacho wakumbusha wanafunzi wa shule ya sekondari Changaa kutumia lugha ya Kiswahili badala ya Kirangi wawapo shuleni hapo. Ajabu ni kuwa Ofisa Elimu Mkoa wa Dodoma eti kamshusha cheo Mkuu wa shule hiyo. Kwa maoni yangu nadhani kushushwa cheo kwa Mkuu huyo wa shule kumekuwa faraja kwake kwani wanafunzi wake hawaongei kiingereza wala Kiswahili badala yake wanatumia KIRANGI.

Jumanne, 20 Agosti 2013

ELIMU HII INAPATIKANA SEHEMU NYINGI SANA TANZANIA

Picha kwa hisani ya mwananchi communications

Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi isiyosajiliwa ya Mutukula, Kijiji cha Namalandula Mkoa wa Geita, wakiwa darasani hivi karibuni. Picha na Jacline Masinde.

Jumamosi, 17 Agosti 2013

FAHAMU VIPAUMBELE VYA MATOKEO MAKUBWA SASA KATIKA ELIMU (BIG RESULTS NOW)

Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Elimu) ulizinduliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo jana na kutaja mikakati 9 ifuatayo: Hebu pitia mikakati hii-kisha utoe maoni yako kama inajitosheleza.

1. Upangaji wa shule kwa ubora wa matokeo ya mtihani kitaifa kuanzia shule iliyoongoza hadi ya mwisho. Lengo la mkakati huu ni kuongeza uwajibikaji na ushiriki wa jamii katika usimamizi wa utoaji wa elimu bora.

2. Utoaji wa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri. Utaratibu wa kutoa tuzo kwa shule utatoa motisha kwa shule kuongeza bidii na kutoa matokeo bora zaidi.

3. Kuwa na kiongozi cha usimamizi wa shule. Mkakati huu utasaidia kuimarisha utendaji wa shule kwa kuwawezesha viongozi wa shule kutekeleza majukumu yao kikamilifu

4. Upimaji wa kitaifa wa stadi za kusoma, kuandika, kuhesabu. Lengo la mkakati huu ni kuhakikisha wanafunzi wanamudu stadi msingi za kusoma, kuandika na kuhesabu katika madarasa ya chini ya elimu ya msingi kabla ya kujiunga na madarasa yanayofuata

5. Utoaji mafunzo kwa walimu kuhusu ufundishaji mahiri wa stadi za KKK. Lengo la mkakati huu ni kuwawezesha walimu kumudu ufundishaji wa stadi za KKK katika darasa la kwanza na la pili. Mafunzo yatatolewa kwa walimu kutoka shule 6,167 za halmashauri 40.

6. Programu ya kujenga uwezo wa walimu na wanafunzi katika ufundishaji na kujifunza-Students Teachers Enrichment Program (STEP). Mkakati huu utajenga utamaduni wa kuwabaini wanafunzi wenye kuhitaji msaada katika kujifunza. Aidha, utoaji mafunzo ya walimu kwa ajili ya utekelezaji yanalenga kumpa mwalimu nyenzo na uwezo zaidi wa kufundisha na kubaini na kuzingatia maeneo yenye changamoto kwa wanafunzi.

7. Ujenzi wa miundombinu muhimu ya shule. Lengo la mkakati huu ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na upatikanaji wa vifaa muhimu shuleni.

8. Utoaji ruzuku ya uendeshaji wa shule. Utekelezaji wa mkakati huu utawezesha uboreshaji wa upatikanaji vitabu vya kiada na vifaa vya kufundishia na kujifunzia shuleni.

9. Utoaji wa motisha kwa walimu. Mkakati huu utawezesha kuwatambua walimu, kutatua changamoto zinazowakabili na kuwapa motisha za kifedha na zisizo za kifedha kwa kujali maslahi na madai yao ya kimsingi.

Jumapili, 11 Agosti 2013

WALIMU NA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI BISUMWA NA CHANGAMOTO ZA MAJENGO BORA

CHOO CHA WALIMU SHULE YA MSINGI BISUMWA

NYUMBA YA MWALIMU SHULE YA MSINGI BISUMWA

Harakati za marafiki wa elimu leo zinatufikisha katika kijiji cha bisumwa ni kijiji kilicho jirani na manspaa ya Musoma Mjini lakini kwa sasa kijiji hiki kiko ndani ya wilaya mpya ya Butiama
marafiki wa elimu tulifanikiwa kuitembelea shule mojawapo katika kijiji hiki na kujionea hali halisi ya madarasa na vyoo picha hapo juu ni choo tegemezi ya walimu wa shule ya msingi Bisumwa.
Choo hiki kina matundu mawili peke yake hakina milango na wala hakiko katika hadhi ya kujisaidia walimu.

maswali tuliyoondoka tukijiuliza vichwani mwetu ni je walimu wanajisaidiaje katika choo hiki ilhali milango yake imeangalia madarasani, lakini kitu cha ajabu katika shule hii ni uwezo mzuri wa wanafunzi wake kujieleza kwa ufasaha pale wanapoojiwa na marafiki wa elimu.
madarasa ya shule hii pia yamechakaa kweli kweli na si salama tena kwa wanafunzi.  lakini licha ya changamoto hizo walimu na wanafunzi wa shule hii ni wanasema wao wanaangalia mbele katu hawatarudi nyuma kuwapatia wanafunzi elimu bora licha ya changamoto hizo.
DARASA MOJAWAPO SHULE YA MSINGI BISUMWA

Ijumaa, 9 Agosti 2013

MADARASA BORA KWA ELIMU BORA

moja ya darasa katika shule ya msingi bisumwa
Hiyo picha hapo juu ni moja ya darasa mojawapo katika shule ya msingi Bisumwa ni kilomita takribani 10 kutoka musoma mjini

Jumapili, 4 Agosti 2013

SERIKALI YA KENYA YASIKIA KILIO CHA WALIMU

Chama cha Taifa cha Walimu Kenya (KNUT) kimesimamisha mgomo uliopangwa kufanyika Alhamisi (tarehe 8 Agosti) baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuahidi kujadiliana kuhusu malipo ya mshahara wa Julai wa walimu walio katika mgomo, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti.

"Tumepata ahadi za Rais mwenyewe, na matokeo yake ni tumeufuta dhamira yetu ya kufanya mgomo sasa," alisema Katibu Mkuu wa KNUT Mudzo Nzili baada ya kukutana na Kenyatta Ijumaa jioni.

KNUT ilimaliza mgomo wa wiki nne tarehe 17 Julai, lakini ilitishia kurejea katika mgomo wakati Tume ya Utumishi wa Walimu iliposema walimu waliogoma hawatapata malipo ya Julai.

"Huku ni kujaribu kuwaadhibu walimu wanaoshiriki katika mgomo kama ilivyoelezwa katika katiba; sio haki," alisema kiongozi wa KNTU wa Kaunti ya Nyandarua Michael Chege.

Waziri wa Elimu Jacob Kaimenyi pia alitangaza siku ya Ijumaa kwamba serikali itatoa shilingi bilioni 3.9 (dola 45,000) kulipa mishahara ya wafanyakazi na wahadhiri wa chuo kikuu na posho za nyumba ili kuzuia mgomo mpya, Capital FM ya Kenya iliripoti.