Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Ijumaa, 7 Juni 2013

Lugha za asili na elimu vijijini!

picha kwa hisani ya maisha plus
Kuna maeneo mengi nchini bado yana changamoto za elimu hasa lugha za kufundishia kuchangia kushuka kwa kiwango cha elimu ,kwa asilimia kubwa watafiti wengi wa elimu nchini wanabainisha kwamba endapo kiswahili kikitumika kufundishia elimu ya awali hadi vyuo vikuu basi tunaweza kuepukana na elimu mbovu inayokabili taifa letu.
changamoto hizi pia zipo maeneo ya vijijini katika nchi yetu katika utafiti mdogo uliyofanywa na marafiki wa elimu waliopo maeneo ya Buhemba,Bisumwa  wilayani Bunda na waliopo Majita, Mgango na Bwai wilaya ya musoma mjini inaonyesha kwamba wanafunzi wengi wanaenda mashuleni wakiwa wanazijua lugha za asili.
hali hiyo upelekea walimu wengi kuwa na wakati mgumu kwani walimu wengi wanatoka maeneo tofauti na hawazifahamu lugha hizo za asili,  walimu hao waliozungumza na marafiki wa elimu wa maeneo hayo wanasema ni mazingira magumu mojawapo ya kazi yao hivyo serikali ingeangalia namna ya kusaidia hali hiyo,
kwani wengi wanadai uchukua hatua tena ya kuanza kufundisha kiswahili ili waanze kwenda sawa na wanafunzi hao.