Kurasa

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?

HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania

Alhamisi, 18 Julai 2013

MBUNGE WA MUSOMA MJINI VINCENT NYERERE AELEZA MAFANIKIO ALIYOFIKIA KWA UPANDE WA ELIMU

Mbunge wa Musoma Mjini Vincent Nyerere akiwa na rafiki wa elimu Juma Richard Radio Victoria Fm
Mapema hii leo katika kipindi cha radio kinachorushwa na marafiki wa elimu musoma Radio victoria fm ya mjini musoma, Mbunge wa jimbo la musoma mjini Mheshimiwa Vincent Nyerere ameeleza  yale anayoyafanya kama kiongozi wa wananchi kuhakikisha anaboresha elimu katika jimbo lake.

katika mada iliyokuwa inasema  VIONGOZI TUNAOWACHAGUA WANAJITOLEA KUBORESHA ELIMU?
Mbunge Nyerere anasema katika kipindi chake cha uongozi amefanikiwa kujenga maabara ya kisasa kwa pesa kidogo ya mfuko wa jimbo anayopata,amesema kwa mwaka anapokea kiasi cha milioni 17 mara 2 na amefanikiwa kujenga maabara yenye thamani ya shilingi milioni 68 amefanikiwa kupata kontena la vitabu lenye urefu wa futi 20 na kuvigawa mashuleni.
pia mbunge huyo anasema kwa jitihada zake pamoja na chama chake wamefanikiwa kutoa madawati kwa shule za chekechea na wametangaza tenda ya kutengeneza madawati kwa shule za msingi jimbo la musoma mjini.
katika shukurani zake mbunge Nyerere kalipongeza shirika la Haki Elimu kwa kufanikisha ujenzi wa maktaba ya kisasa katika shule ya msingi mwisenge na kuahidi kuendeleza ushirikiano na marafiki wa elimu kuhakikisha kiwango cha elimu kinaimarika jimbo la musoma mjini.

Vincent Nyerere  ni moja ya viongozi wanaoonesha nia ya kuboresha elimu!  je kiongozi wako anawajibika kuboresha elimu?