Mwanafunzi, Ezra Gerald Wabamba, aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika
Shule ya Sekondari Ihungo, mkoani Kagera, amekatisha maisha yake kwa
kujinyonga akiwa hospitalini na kuacha ujumbe mzito juu ya chanzo cha
kifo chake.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Gilles Muroto,
mwanafunzi huyo alifikishwa hosptalini hapo Septemba 11, mwaka huu na
kulazwa ili kupatiwa matibabu.
Alisema Ezra alijinyonga saa 1:30 asubuhi katika mti ulikuwa umbali wa
hatua 73 kutoka kwenye wodi ya wagonjwa namba tatu aliyokuwa amelazwa,
kwa kutumia shuka yake binafsi.
Alisema baada ya maiti yake kugundulika na kufanyiwa upekuzi kwenye
mifuko yake ya nguo kulikutwa Sh. 3,900, funguo mbili za Solex na
kipande cha karatasi chenye ujumbe.
Alisema ujumbe huo ulisomeka: “Haiwezekani binadamu kuhudumiwa kama
mbwa, yaani nafika hospitali naeleza hali yangu halafu daktari
ananiandikia kulazwa bila ya kupimwa, sasa sijui watatibu nini?, kwa
kweli siwezi kuvumilia yaani wenzangu wanasoma halafu mimi nimekalishwa
tu hapa hospitalini bila ya kujua wananitibu nini, inaniuma sana mpaka
kufika hatua hii ya kujiondoa duniani, ni kwasababu ninaona wanachezea
ndoto zangu, mimi siwezi kuona ndoto yangu inazimwa wakati ninatakiwa
niwepo shuleni nikamilishe ndoto zangu, mjitahidi tukutane mbinguni.”
Mwanafunzi huyo alimalizia ujumbe huo kwa maeneo ya kiingereza yaliyosomeka: “ Respect my family and brother Henry.”
Kamanda Muroto alisema katika tukio hilo hakuna aliyekamatwa ila
uchunguzi juu ya kifo cha mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma masomo ya
mchepuo wa kemia, bailojia na jiografia (CBG) unaendelea, ili utaratibu
wa kuukabidhi mwili wa marehemu kwa familia yake yenye makazi yake
mkoani Tabora ufanyike.
Juhudi za kumpata Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Kagera, Dk. Thomas
Rutachunzibwa, ili kupata ufafanuzi wa kifo hicho chenye mazingira tata
hazikufanikiwa kutokana na kuwa nje kiofisi, ingawa Katibu wa hostali
hiyo, Justus Benges, alithibitisha tukio hilo kutokea hospitalini hapo.
Alisema mwanafunzi huyo alikuwa akiendelea na huduma ya matibabu kutokana na kugundulika na ugonjwa wa malaria kali.
Mazingira ya kifo cha mwanafunzi huyo yameleta sintofahamu katika jamii
ya wakazi wa mji wa Bukoba, huku baadhi wakihusisha kuwapo huduma mbovu
inayotolewa na hositali hiyo pamoja na lugha zisizorafiki kwa wagonjwa.
Imebainika kuwa marehemu tangu alazwe hospitalini hapo, alikuwa
akihudumiwa kwa kupelekewa chakula na wanafunzi marafiki zake ambao
walikuwa wakitoka shuleni.
chanzo Ippmedia.com
harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni