Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania
Jumatano, 11 Juni 2014
changamoto ya elimu toka Geita
Walimu
97 katika shule ya msingi Nyankumbu na Mkombozi katika Wilaya ya Geita,
wanatumia tundu moja la choo ambacho kipo kwenye nyumba ya mwalimu huku
wanafunzi wa shule hizo 3,563 wakitumia matundu 14 ya choo na kuhofiwa
kutokea magonjwa ya milipuko.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni