harakati za marafiki wa elimu musoma wasiliana nasi kwa namba +255755 650 075 au +255786 650 075 ni jukumu letu kuboresha elimu
HARAKATI ZA MARAFIKI WA ELIMU NI NINI?
Ni harakati za watu wanaojali na wenye nia ya kuleta mabadiliko katika kuboresha elimu na demokrasia nchini. Harakati hizi zinawaleta pamoja wananchi wanaopenda maendeleo ya elimu na zinawapa fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu katika masuala yanayohusu elimu .Sera na mipango mbalimbali ikiwemo mpango wa maendeleo ya elimu ya msingi (MMEM) na mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari (MMES) inasisitiza ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wake.Hivyo wananchi wote wanawajibu wa kuchangia uboreshaji wa elimu na demokrasia nchini. kujiunga na harakati hizi za marafiki wa elimu ni bure na hakuna malipo yoyote wasiliana nasi kwa namba 0755 65 00 75 au 0786 65 00 75 au e-mail jmrchrd@yahoo.com tukuunganishe na marafiki wa elimu popote ulipo Tanzania
Jumanne, 29 Julai 2014
ZAIDI YA WANAFUNZI 860 WA SEKONDARI WILAYANI KILINDI WAMEACHA SHULE.
Wanafunzi zaidi ya 860 wa shule mbali mbali za sekondari wilayani Kilindi wameacha shule kwa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya wazazi wao kuwaozesha huku wengine wakiwekwa kinyumba na baadhi ya makundi ya vijana.
Mkuu wa wilaya ya Kilindi bwana Selemani Liwowa amesema hayo katika kikao cha baraza la madiwani ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dr . Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa watuhumiwa waliosababisha tatizo hilo wanakamatwa na kufunguliwa kesi katika vyombo vya sharia.
Akielezea mikakati waliyojiwekea na hatua zitakazochukuliwa mkuu huyo wa wilaya amesema kwanza wanataka wawarejeshe watoto hao kwa wazazi kisha watawakamata wazazi na watuhumiwa waliowakatisha masomo kwa ajili ya kuwachukulia hatua kali za kisheria zoezi ambalo linaanza utekelezaji wake baada ya sikukuu ya eid kumalizika.
chanzo ITV
Wanafunzi 140 wakwepa masomo tunduma na kujihusisha na biashsra ndogondogo.
Zaidi ya wanafunzi 140 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza
mwaka huu katika halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma wilayani
momba mkoani Mbeya bado hawajaripoti shuleni kuanza masomo na badala
yake wanadaiwa kujihusisha na biashara ndogondogo kama vile kuuza
karanga na kubeba mizigo mpakani mwa Tanzania na Zambia mjini Tunduma.
Akizungumza kwenye baraza la halmashauri ya mamlaka ya mji mdogo wa
Tunduma, mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya momba ambaye pia ni katibu
tawala wa wilaya hiyo, Mathias Mizengo amesema kuwa halmashauri ya
mamlaka ya mji mdogo wa Tunduma inakabiliwa na changamoto ya baadhi ya
vijana ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu
kutoripoti shuleni na hivyo akawataka viongozi wa mamlaka hiyo
kuhakikisha vinaja hao wanatafutwa kila mahali walipo na kuwapeleka
shuleni.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Juma Kitabuje amesema kuwa
hadi kufikia mwezi juni mwaka huu wanafunzi 144 kati ya wanafunzi 956
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika mji wa Tunduma ndio
ambao walikuwa hawajaripoti shuleni kati yao wanafunzi 70 wakiwa ni
wavulana na wanafunzi 74 wasichana huku akielezea sababu kubwa ya watoto
hao kutohudhuria masomo kuwa ni kutelekezwa na wazazi na kujihusisha na
biashara za kuuza karanga na kubeba mizigo mpakani.
Kuhusu hatua ambazo zinachukuliwa na mamlaka hiyo kuhakikisha kuwa
wanafunzi hao wanaendelea na masomo, mkurugenzi huyo amesema kuwa wazazi
wa watoto hao wamefikishwa kwenye baraza la kata na kupewa muda hadi
kufikia Agosti 25 mwaka huu kuwasaka watoto wao popote walipo na
kuwapeleka shuleni.
Kwa wasiomfahamu mwalimu.
![]() |
| Mwalimu JK Nyerere |
1. Ndiye rais aliyewahi kulipwa mshahara kidogo duniani
2.ndiye mtu aliyeitetea china isitengwe na UN, baada ya mataifa yote kuogopa vtisho vya marekani, wachina wanamtambua na kumheshimu sana
3. Ndiye rais pekee aliyetishia kuvunja balozi za uingereza, ujeruman na ufaransa na hata kukataa msaada wao kwa kitendo chao cha kuunga mkono serikali ya kibaguz afrika kusini
4. Ndiye rais aliyewezesha watoto wa masikin wasome bila ada na matibabu bure. Nenda nchi za kenya, afrika kusini . Kama baba yako hakushirik harakati za ukomboz ili utoke labda uwe jambaz maana huwez hata kujilipia ada
Ndiye rais pekee aliyechukia ufisadi toka moyoni.
Jumanne, 22 Julai 2014
binti aliyekeketwa alilia shule
Akiwa darasa la nne alikamatwa kwa nguvu..
Kuna mambo mengi anakumbukia msichana mwenye umri wa
miaka 12 yamemtokea maishani. Lakini tukio la siku hiyo, kuitwa na
mama yake mdogo, kisha kukamatwa kwa nguvu na kukeketwa linabaki kuwa
kovu lisilopona katika maisha yake. Ni ukatili uliopitiliza uliobadili
kabisa ndoto za maisha yake za kupata elimu.
Binti wa miaka 12 (jina linahifadhiwa) ni mtoto wa mwisho wa kike kati ya watoto nane wa mzee Isaya na Mama Gyar Baa kutoka familia moja ya kabila la Kimbulu.
Kabla hajakumbwa na mkasa uliobadilisha kabisa welekeo wa maisha yake, alikuwa mwanafunzi wa darasa la nne mwenye ndoto za kusoma hadi kufikia ukomo wa maisha yake.
Hata hivyo, ndoto hizo zilizimwa baada ya kujikuta akilazimishwa kukeketwa ikiwa ni ishara ya maandalizi ya kutafutiwa mume ili aolewe.Tukio hilo la kikatili liliathiri maisha yake.
Makazi ya familia ya binti huyo ni katika kijiji cha Konje wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kilichopo umbali wa kilometa 16 kutoka Handeni mjini.
Msichana huyo, anatoka katika familia ya wafugaji, yenye tabia ya kuhamahama ili kufuata malisho, hasa nyakati za ukame ili kuhakikisha kuwa mifugo yao haikosi chakula na maji.
Akisimulia kwa uchungu mkasa alioupata uliobadili kabisa uwelekeo wa maisha yake, msichana huyo anasema siku hiyo ya Jumanne (hakumbuki tarehe) aliitwa na mama yake mdogo (mama wa kambo). Aliitika na kutii amri kwa kwenda kusikiliza alichoitiwa akiwa hana fununu kabisa ya dhamira ya muitaji.
Anasema baada ya kufika nyumbani kwa mama yake huyo, alishangazwa kumkuta dada yake anayemfuata (jina linahifadhiwa) akiwa amefungwa mikono na miguu huku akilia kwa uchungu sana. Kilichomsikitisha zaidi ni kuona jinsi ambavyo dada yake alikuwa akivuja damu nyingi katika sehemu zake za siri.
Jambo hilo, lilimtisha sana Tansiana na kutokana na hamaki akapata wazo na maamuzi ya haraka ya kukimbia kutoka nyumbani kwa mama yake mdogo ili kujinusuru na hatari aliyoona kuwa inamkabili. Hata hivyo, hakufanikiwa kutimiza matakwa yake.
“Nilishtuka sana, kumuona dada akilia huku damu zinamtoka kwa wingi sana katika sehemu zake za siri. Lakini nilivyotaka kukimbia mama mdogo na bibi yule niliyemkuta pale nyumbani ambaye sikufahamu ametokea wapi wakanikamata na kunifunga mikono na miguu kwa kamba,” anasimulia msichana huyo kwa masikitiko.
Baada ya kufungwa na kudhibitiwa kikamilifu ndipo bibi huyo asiyemfahamu akachukua kiwembe na kumkata kwenye sehemu yake ya siri kwa namna alivyojiridhisha na kusababisha atokwe damu nyingi kama ilivyokuwa kwa dada yake.
“Wakati wananikata sikusikia maumivu sana kwa sababu nilikuwa na hasira sana kwa kile kitendo nilichokiona amefanyiwa dada yangu…ndipo baada ya kupita muda kama kama saa moja hivi nikaanza kusikia maumivu makali sana kama roho inataka kutoka. Ndipo nikatambua namna gani watu wale walivyo wakali. Nilikuwa nimefanyiwa unyama wa hali ya juu bila ya ridhaa yangu. Nililia sana na kwa hakika nimemchukia sana huyo mama mdogo na sijui kama nitamsamehe,” anasema.
Akikumbukia zaidi anasema kuwa “wakati wananifanyia unyama huo, mama yangu mzazi alikuwa amesafiri kwenda Karatu na baba hakuwapo nyumbani. Aliporudi alikuta tayari tumekeketwa.”
Anabainisha kwamba, ilimchukua takriban mwezi mmoja kuuguza kidonda hicho hadi kupona. Aina ya matibabu aliyokuwa akipewa anasema kuwa, ni kupakwa maziwa na mafuta ya taa mara mbili kwa siku.Yaani asubuhi na jioni kama dawa ya kuponyesha jeraha hilo. Alipata msongo mkali wa mawazo kuhusu tukio hilo baya kabisa na la ukatili wa kupindukia.
Baba yake, licha ya kutabua unyama waliofanyiwa, lakini hakuchukua hatua zozote dhidi ya wahalifu wale.
Anasema kuwa, miongoni mwa sababu walizoelezwa zilizolazimisha wachukuliwe hatua hiyo kukeketwa ni watoto wa kike kuwafanya waachane na vitendo vya uhuni kwa kile kinachodaiwa kuwa, wasipokeketwa wanakuwa na tamaa kali ya kufanya mapenzi muda wote.
Hii ni kutokana na mila na desturi za kabila lao, kwamba iwapo binti hatakeketwa, basi ni dhahiri kwamba hatapata mume wa kumuoa na hatakuwa na heshima wala thamani anayostahili kupewa mwanamke kwenye jamii hiyo.
Kutokana na kitendo hicho, anasema kuwa ni dhahiri kwamba ameandaliwa kwa ajili ya kuolewa, hata kama jambo hilo litafanyika litakuwa ni kinyume cha ridhaa yake.
“Najua sasa hivi nasubiri tu kuolewa. Lakini ni kwamba watanilazimisha tu lakini mimi mwenyewe sipendi…napenda sana kusoma… natamani sana ajitokeze mtu wa kunisaidia katika hilo. Nipo tayari kabisa kwa hilo…na baada ya kusoma cha kwanza nitakachofanya ni kuhakikisha nazuia mila hii mbaya isiendelee kufanyika kwa wasichana wengine wa jamii hii. Kwa kweli inauma sana…tunateseka sana jamani,” anasema msichana huyo huku akibubujikwa machozi.
Msishana huyo, licha ya hatua ngumu ya maisha yake aliyopitia, lakini ana matumaini kuwa, siku moja atakuwa mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake, na kupiga vita mila na desturi ambazo zimekuwa zikitumika kumgandamiza mwanamke.
Aina hiyo ya maisha, ndiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kumfanya msichana huyo kuwa miongoni mwa wale waliokosa fursa ya kupata haki yake ya msingi hasa elimu. Alikuwa na ndoto za siku moja kupata elimu ili uwe mwanga wa uhakika kwa maisha yake na jamii yake inayomzunguka.
Pamoja na kukabiliwa na changamoto hiyo maishani, lakini binti huyo katika familia yake ana msimamo wa kupenda elimu na kujituma kwa kazi za kifamilia na kwamba iwapo atatokea mfadhili yoyote atakayekuwa tayari kumchukua na kwenda kumsomesha hata wazazi wake sasa wameutambua ukweli huo na kuwa tayari kumruhusu aende akapate elimu.
“Kamwe sitasahau unyama huu…nikipata elimu lazima niwe mwanaharakati wa kupinga unyama huu ,” anasema.
Mama mzazi wa binti huyo aitwaye Gyar Baa Isaya anasema kuwa wakati binti yake anakeketwa, alikuwa safarini na hakushirikishwa na mumewe kuhusu kufanyika kwa kitendo hicho.
Kimsingi anasema, alikuwa anafahamu kuwa siku moja binti yake atalazimika kufanyiwa mila hiyo kwa sababu ni utamaduni ambao hata yeye ameupitia na hakuwa na mamlaka ya kuupinga, kwani kwa kufanya hivyo, angeweza kumsababishia matatizo mtoto wake ikiwamo kutoolewa.
“Kusema kweli kwa mila za kwetu ili uonekane ni mwanamke ambaye umekamilika ni lazima ukeketwe…vinginevyo hupati mume na unaweza kupatwa na majanga makubwa ikiwamo binti kuanza tabia mbaya kabla ya wakati wake…sasa watoto wangu wamelazimika kufanyiwa mila hiyo ingawa hawakuridhika nayo kabisa,” anasema mama huyo.
Naye dada wa msichana huyo aliyeanza kufanyiwa ukatili huo, anasema kuwa sababu kubwa ya mdogo wake kushindwa kuendelea na masomo licha ya kuwa na ndoto za kufika mbali kimaisha ni ile hofu ya kuchekwa na wenzake hasa wakati wa kuoga wakimuona amekeketwa.
“Unajua mnapokuwa rika moja mnakuwa hamuoneani aibu kabisa, hata kama kuoga mtaenda wote, sasa wenzako wakikuona uko tofauti na wao kimaumbile wanakushangaa na wengine wanakucheka. Hali hii nilipokuwa nikimwelezea mdogo wangu ilichangia kumkatisha tamaa ya kusoma kwa hofu ya kuchekwa,” anasema dada huyo ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule moja.
Hata hivyo anasema, kitendo walichofanyiwa kinadhihirisha udhalilishaji kwa mtoto wa kike na kwamba licha ya baba yao kuwa ni miongoni mwa wafugaji wenye tabia ya kuhamahama, lakini amedhamiria kuhakikisha kuwa anamaliza masomo yake.
“Baba yetu ni miongoni mwa wafugaji wenye tabia ya kuhamahama makazi, hali hii imetuathiri sana kielimu tena mimi ni nafuu kwa sababu naishi kwenye hosteli za shule. Mdogo wangu ndiyo amerudi nyuma kwani hadi sasa hasomi na aliishia darasa la nne,” anasema dada huyo.

CHANZO: Ippmedia.com
Jumamosi, 19 Julai 2014
Waliohitimu la 7 Vijibweni waitwa kuchukua vyeti
Tuhuma hizo ziliibuliwa na baadhi ya wazazi wa wanafunzi hao, wakisema wamechoshwa na ahadi za mwalimu huyo kwa zaidi ya miaka miwili sasa tangu vyeti hivyo kupotea, ziliandikwa na gazeti hili hivi karibuni.
Wazazi hao walidai mkuu huyo alihusika kwa sababu hakuwa wazi kueleza mazingira halisi ya jinsi vyeti hivyo vilivyopotea na kwamba hakupenda suala hilo lifike ngazi za juu.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, mwalimu huyo, alisema tofauti zilizojitokeza awali hadi kusababisha vyeti hivyo kuchelewa kukabidhiwa kwa wahitimu zimepatiwa ufumbuzi na vyeti hivyo vipo tayari.
Alisema baada ya mchakato wa kuviandaa vyeti hivyo kukamilika tangu juzi, klichobaki ni kuwakabidhi wahitimu hao.
“Mbona nimeanza kuwakabidhi wachache waliopata taarifa… nimeweka matangazo katika eneo linalozunguka shule kwa ajili ya kuwajulisha kuwa vyeti vyao vipo tayari ni wao wenyewe sasa.
“Niwaombe wazazi kupitia gazeti lenu wa waambie watoto wao waende shuleni hapo wakachukue vyeti vyao,” alisema Jasembe.
Hivi karibuni wazazi wa watoto hao, walifikisha tuhuma hizo kwa Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile, Ofisa Elimu na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke.
Jumatano, 16 Julai 2014
SHULE YA ISANGO ILIYOKUWA IKIMILIKIWA NA JUMUIYA YA WAZAZI CCM YAUZWA KWA BEI CHEE
shule ya sekondari Isango iliyoko Kinesi Wilaya ya Rorya mkoa wa Mara imeuzwa kwa bei sawa na bure ya sh. milioni 125wakizungumza kwa nyakati tofauti mwenyekiti wa ccm na mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Rorya kupitia kituo cha radio Victoria Vfm wamedai kuwa shule hiyo imeuzwa kijanja janja kwani tangu mwenyekiti huyo wa wazazi aingie madarakati hakuwahi kuambiwa juu ya uwepo wa deni lililopelekea kuuzwa shule hiyo.
mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi alienda mbali zaidi na kusema kitendo hicho kimefanywa makusudi kwa lengo la kumharibia uwajibikaji wake kwani kadai aliyeinunua shule hiyo ni mtoto wa aliyekuwa Mwenyekiti wa wazazi ccm mkoa wa Mara.
pia kasema kuwa dalali alionyesha wazi muenendo wa rushwa, kwa kugonga nyundo ya mwisho wakati bado wateja wengine wakiendelea kupandisha dau.
baada ya hapo ametoa wito kwa wananchi kumuunga mkono ili kuhakikisha shule hiyo inarejeshwa kwa wananchi baada ya kuwaambia wananchi hao kuwa tayari wamekwisha fungua kesi mahakama ya rufaa na hivi karibuni atakwenda kuonana na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi ili kuhakikisha shule hiyo inarejeshwa mikononi mwa wananchi.
Jumatano, 9 Julai 2014
Tunataka wapate maarifa au wajue Kiingereza? makala ya Gervas Zombwe.
Tafiti zote duniani zinasema wazi kuwa binadamu yeyote
anajifunza na kuelewa kikamilifu anapofundishwa kwa lugha anayoijua
zaidi. Na uwezo wa kujenga utambuzi na kukuza vipawa umo ndani ya mila
na desturi asilia zinazofungamana moja kwa moja na lugha mama
inayomiliki maarifa na michepuo ya akili.
Kufundishwa kwa lugha asiyoielewa vizuri kunamzuia
binadamu kumiliki maarifa ya kukuza michepuo ya akili. Kweli atasoma,
atapata cheti, digrii, lakini maarifa na ubunifu viitabaki nje ya
utambuzi wake.
Ndiyo maana nchi zote zilizoendelea wanafundisha
watu wao kwa lugha zao. Huwezi kubuni kwa kutumia lugha ya jirani,
huwezi kufikiri kwa kutumia lugha ya kukopa, kuwezi kuvumbua kwa kutumia
lugha ya kigeni. Ni ndoto!
Mwalimu wa lugha, mtafiti na mtetezi wa lugha
Profesa Martha Qorro, siku zote kupitia tafiti nyingi alizofanya amekuwa
akisisitiza manufaa ya kutumia lugha ya taifa kufundishia vijana wetu.
Ili mwanafunzi afike ngazi ya juu kabisa ya
uelewa, ni lazima maarifa yapitie kwenye lugha anayoijua vizuri.
Vinginevyo atakuwa anajifunza juu juu tu na kuishia kwenye uelewa wa
hatua ya mwanzo tu. Hatua za uelewa ziko kama ifuatavyo:
Hatua ya kwanza, uwezo wa lugha ya ‘kuombea maji’.
Akilazimika kujifunzia lugha katika ngazi hii mzungumzaji inabidi
akariri karibu kila kitu kwa kuwa ana uelewa mdogo. Huchukua muda mrefu
kuelewa mambo madogo kwa kuwa lugha ni kikwazo. Haoni uhusiano kati ya
maisha yake na mambo yale anayofundishwa au anayoelezwa shuleni. Masomo
humchosha na mawazo huhama darasani.
Hatua ya pili, uwezo wa kumpa mtu maelekezo ya
namna ya kufika sehemu fulani. Uelewa wa juu juu wa mambo
yanayozungumzwa au kufundishwa kwa lugha hiyo. Tabia ya kukariri bado
inaendelea, ingawa imepungua kwa kiasi kikubwa. Uwezo wa kuandika
sentensi fupi fupi sahihi na kuuliza maswali rahisi. Kuna uwezekano
mkubwa wa kutoelewa au kuelewa vibaya maana iliyokusudiwa. Uhuru wa
fikra haupo!
Hatua ya tatu, uwezo wa kufikiri, kutafakari,
kujadili, kuchambua na kuchanganua masuala na dhana mbalimbali
yanayozungumzwa au kufundishwa kwa lugha husika. Mzungumzaji anakuwa na
uwezo mkubwa wa kutumia lugha kama nyenzo ya kuvumbua mambo mapya. Ana
uhuru wa kutumia lugha husika na yote atakayoelezwa katika kujikomboa
kimawazo.
Katika hatua hii, lugha siyo kikwazo katika
kuelewa, kupambana na changamoto za maisha. Hahitaji kukariri; bali
hutumia uelewa wake katika kujibu maswali au kutoa maelezo juu ya yale
anayoyaelewa. Ni katika hatua hii ya uelewa ndiyo wanafunzi wanapoweza
kujifahamu, kujitambua, kuwa mbunifu, kutumia fursa, kujiendeleza,
kutafiti na kutatua changamoto zinazomzunguka. Wanafunzi wetu wengi
shuleni na vyuoni hawafiki hatua hii. Ushahidi unaonyesha shule za
sekondari hawajifunzi na kupata maarifa kutokana na lugha. Kwa mfano,
tafiti nyingi (Mlama na Matteru 1978, Criper and Dodd 1984, Roy-Campbell
and Qorro 1987, Rubagumya, Jones and Mwansoko 1998, Qorro 1999,
Mwinsheikhe 2003, Puja 2003, Brock Utne 2004, Vuzo 2005) zimeonyesha
kuwa wanafunzi wengi katika shule za sekondari na vyuo nchini Tanzania
wana uwezo wa hatua ya kwanza au ya pili ya uelewa wa lugha inayotumika
kufundishia.
Kwa kung’ang’ania kutumia lugha wasiyoelewa,
tunawafundisha wanafunzi wetu kushindwa! Wengi wao wanajifunza
kutodadisi, kutofikiri, kutokuuliza maswali, kunakili na kukariri, kuwa
waoga, kutojiamini, kukubali kila hali na kukata tamaa kwa kauli ya
“yote maisha”. Ni vyema tukajiuliza, kuandaa vijana wasioweza kuelewa,
kujadili, kufikiri, kuchambua na kuchanganua masuala na dhana mbalimbali
zinazofundishwa ni kwa masilahi ya nani? Ni wazi kwamba tunahitaji
elimu ya kujikomboa na kwamba ili kufanikisha elimu ya kujikomboa
shuleni na vyuoni, ni lazima wanafunzi watumie lugha ambayo wao na
walimu wao wana uelewa wa hali ya juu.
Katika hali ambayo wanafunzi wana uelewa mdogo wa
lugha, wanafunzi wengi, hasa wasichana, huwa wanyonge na kwa muda mwingi
hunakili maandiko ya mwalimu (mengine yakiwa na makosa) kwa kadri
watakavyoweza kuyasoma. Maandiko hayo kwa sehemu kubwa wengi
hawayaelewi.
Badala ya kujifunza masuala ya msingi, wanafunzi
wanaishia kukariri maneno kwa lugha wasiyoelewa na muda mwingi unapotea
na ari ya kusoma inapungua. Elimu hii ya kunakili na kukariri haiwapi
uwezo wa kujikomboa bali huenda kinyume na makusudio.Kama tunataka maendeleo ya kweli, Waafrika ni lazima wachukue mamlaka
juu ya taratibu zinazotumika kuendesha elimu yao. Lazima wafundishe
watoto wao kwa lugha wanazoelewa ili kuwaandaa kuwa wadadisi wa kutafuta
majibu ya matatizo yanayoikabili jamii. Ikumbukwe kuwa lengo kuu la
elimu ni maendeleo siyo umahiri wa lugha fulani. Ni falsafa mbadala!
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)